Miaka 65 ya BBC Swahili:Mimi, Kikeke tulikuwa watangazaji wa kwanza wa michuano ya Kombe la Dunia kwa Kiswahili
Miaka 65 ya BBC Swahili:Mimi, Kikeke tulikuwa watangazaji wa kwanza wa michuano ya Kombe la Dunia kwa Kiswahili
Ni miongoni mwa mambo anayojivunia nayo Charles Hillary aliyewahi kufanya kazi na Idhaa ya Kiswahili ya BBC Akiwa ni miongoni mwa watangazaji mashuhuri sana hasa katika matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu.
Charles Hillary alikua miongoni mwa watangazaji wa Kwanza kutangaza matangazo ya mpira wa miguu kwa kiswahili moja kwa moja kutoka uwanjani na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu visiwani Zanzibar Lakini anakumbuka nini hasa siku yake ya kwanza alipojiunga na BBC Swahili?
Tulipata nafasi adhimu ya kutembelea Ikulu ya Zanzibar. Scolar Kisanga amezungumza naye.



