Huenda Trump akavuna mabilioni ya dola kupitia mtandao wake wa kijamii, kwa nini?

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Donald Trump anaonekana kuhangaika kutafuta pesa za kulipa faini ya ulaghai ya dola milioni 464. Je, soko la hisa linaweza kumuokoa?

Trump Media, ambayo inasimamia mitandao wa kijamii Truth Social, iko tayari kujumuishwa kwenye soko la hisa, na wanahisa wa Digital World Acquisition Corp wakitarajiwa kupiga kura siku ya Ijumaa iwapo watainunua.

Bw Trump angekuwa na hisa ya angalau asilimia 58 katika kampuni iliyounganishwa, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 3 kwa bei ya sasa ya Digital World.

Digital World, au DWAC, ndiyo inayojulikana kama SPAC, au biashara iliyoundwa ili kununua kampuni nyingine na kuiweka wkeny soko la hisa.

Ni hali ya kushangaza inayoweza kutokea kwa Bw Trump kwa kubadilishana biashara ambayo mkaguzi wake wa hesabu alionya mwaka jana kuwa ilikuwa katika hatari ya kufeli.

Licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi zinazohusiana na mpango huo, ikiwa ni pamoja na kesi ambazo hazijatatuliwa kutoka kwa washirika wa zamani wa biashara. Pia kuna malipo ya dola milioni 18 ambayo Digital World ilikubali kulipa mwaka jana ili kutatua malipo ya ulaghai kuhusu jinsi mpango wa kuunganisha ulivyotekelezwa.

Waungaji mkono wa Digital World - ambao wengi wao ni wawekezaji binafsi badala ya makampuni ya Wall Street, wengi waaminifu wa Trump - wanaonekana kutokuwa na hofu.

Ikiwa ununuzi utaidhinishwa, hali ambayo inatarajiwa, hisa zitaanza kuuzwa kwenye soko la hisa la Nasdaq chini ya DJT.

Pia uanaweza kusoma:
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mkataba huo hauwezi kutatua mara moja matatizo makubwa zaidi ya kifedha ya Bw Trump, kama vile adhabu yake inayohusu ulaghai huko New York.

Rais huyo wa zamani amezuiwa kuuza hisa zake kwa angalau miezi sita - ingawa kampuni hiyo mpya inaweza kumpa msamaha.

Bw Trump anaweza kujaribu kupata mkopo, kwa kutumia thamani ya hisa. Lakini katika kesi hii, wachambuzi walisema benki pengine inaeweza kumkopesha kiwango cha chini cha thamani ya hisa kwenye karatasi, kutokana na hatari zinazowezekana za biashara.

Hilo halijawazuia baadhi ya wafuasi wake wakitumai uungwaji mkono wao utasaidia.

Bw Nedohin, ambaye anajitambulisha kwenye tovuti yake kama "kiongozi wa ibada" wa Kanada na na anayejiita Kapteni DWAC kwenye Truth Social, alikataa kuhojiwa.

Lakini kwenye tamasha lake wiki hii aliwataka wawekezaji kuidhinisha mpango huo, akikisia kuwa unaweza kumsaidia rais katika vita vyake vya kisheria.

"Ikiwa muunganisho utakamilika Ijumaa saa 10 asubuhi na Trump ghafla ana hisa milioni 120 za DJT ambazo zina thamani ya dola bilioni tatu, nne, tano, kumi nani anajua? Anaweza kujiinua kwa urahisi kupata mkopo," alisema.

Hatari kwamba wanahisa wa Digital World watapoteza pesa kwenye uwekezaji wao ni mkubwa, kulingana na wachambuzi.

Hisa katika kampuni kwa sasa zinafanya biashara kwa karibu dola 43 kila moja.

Hiyo ni chini kutoka kwa kiwango cha juu iliyofikia baada ya mipango ya kununua Trump Media kutangazwa.

Lakini bado ina maana kwamba Trump Media ina thamani ya zaidi ya dola bilioni 5, ambayo ni nyingi kutokana na kwamba ilileta mapato ya dola milioni 3.3 tu katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka jana na kupoteza karibu dola milioni 50.

Muungano huo utailetea Trump Media zaidi ya dola milioni 200 pesa taslimu ambazo zinaweza kutumia kwa ukuaji na upanuzi.

Lakini kwa Truth Social, ambayo ilizinduliwa kwa umma mnamo 2022, ikijitangaza kama mbadala kwa mitandao mikubwa ya kijamii kama Twitter na Facebook, bado ni ndogo.

Makampuni ya nje yanakadiria Truth Social ilipokea takribani watu milioni 5 walioitembelea mnamo Februari.

Kwa kulinganisha, X ya Elon Musk, iliyokuwa Twitter, na iliyothaminiwa hivi karibuni na mwekezaji mmoja kwa takriban dola bilioni 14, ilipokea zaidi ya watu milioni 100.