Tetesi za soka Ulaya Jumatano: United na Chelsea zamtaka Mgambia

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United na Chelsea zinafikiria kumsajili beki wa Tromsø mwenye umri wa miaka 19, raia wa Gambia, Abubacarr Sedi Kinteh. (Mail)

Klabu ya Al-Ittihad inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah msimu huu wa kiangazi, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 yuko tayari kujiunga nao. (Foot Mercato)

Kiungo wa Nottingham Forest Morgan Gibbs-White anaweza kuondoka klabuni hapo msimu huu wa kiangazi, huku Aston Villa ikimuona mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 26 kuwa chaguo linalofaa kwao. (Teamtalk)

Beki wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 32, anakaribia kusaini mkataba mpya na Manchester United. (Mail)

Real Madrid inatafuta beki wa kati, na nahodha wa Tottenham Cristian Romero anaonekana kama chaguao mojawapo. Mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 27 pia amewahi kuhusishwa na klabu za Barcelona na Atletico Madrid. (Mundo Deportivo)

Bayern Munich imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa England Harry Kane kuhusu mkataba mpya, na ina imani kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atasaini. (Sky Sports)

Liverpool ipo mbele kati ya klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 19, raia wa Ufaransa, Eli Junior Kroupi, kwa ajili ya usajili wa kiangazi. (Caught Offside)

Leeds United inapanga kuwasilisha dau la pauni milioni 30 kumsajili kipa wa Manchester City mwenye umri wa miaka 23, James Trafford. (Teamtalk)

Brighton ilikubali ofa kutoka Nottingham Forest mwezi Januari kwa ajili ya kumuuza beki wa England mwenye umri wa miaka 34, Lewis Dunk, lakini mchezaji huyo alichagua kubaki klabuni hapo. (Sky Sports)

Crystal Palace inaweza kupunguza bei yake ya pauni milioni 30 kwa mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta msimu huu wa kiangazi, huku Manchester United ikionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Football Insider)

Juventus na klabu nyingine za Serie A zitapata ugumu kumudu mshahara wa kiungo wa Newcastle United Sandro Tonali. Mchezaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 25 pia anafuatiliwa na klabu za Manchester United na Arsenal. (The Athletic)