Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Cristiano Ronaldo kusitisha mgomo wake Saudia
Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusitisha mgomo wake katika klabu ya Al-Nassr na kucheza tena katika klabu hiyo ya Saudi Pro League siku ya Jumamosi.
Fowadi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41 amekosa mechi mbili kwa sababu hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa. (Sky Sports)
Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford Barcelona inategemea uchaguzi wa rais wa klabu hiyo mwezi ujao.
Mkataba wa pauni milioni 26 kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United kwa mkopo, 28, ndio kiini cha ombi la Joan Laporta kuchaguliwa tena. (Times - Subscription Required}
Manchester United itamlenga mshambuliaji wa Everton na Senegal Iliman Ndiaye, 25, ikiwa Rashford atahamia Barcelona kwa mkataba wa kudumu. (Caught Offside),
Bournemouth inapanga kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Eli Junior Kroupi, 19, kandarasi mpya yenye unono mwingi kwa nia ya kuzuia kutakiwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, vikiwemo Chelsea, Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain. (Sun),
Manchester City wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Elliot Anderson, 23. (Teamtalks)
Bayern Munich hawatarajii kumsaini fowadi wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, na hivyo kuongeza matumaini ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Christian Falk),
AC Milan wana imani kuwa Fulham watatoa chaguo la pauni milioni 21 kumnunua winga wa Nigeria Samuel Chukwueze, 26, ambaye yuko kwa mkopo Cottagers. (Gazzetta - In Italy)
Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Rocco Reitz, 23, ambaye thamani yake ni takriban £35m. (Fichajes - In Spanish)
Mchezaji mwengine anayelengwa na Manchester United, Sandro Tonali wa Newcastle United, huenda akawa na bei ya hadi £100m. Kiungo huyo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 25 pia anavutia klabu za Arsenal, Manchester City na Juventus. (Talksport),