Vilabu vyamwaga mabilioni, dirisha la usajili EPL likivunja rekodi ya £3bn

Muda wa kusoma: Dakika 5

Vilabu vya Ligi Kuu England vimetumia fedha nyingi kuliko wakati wowote ule kwenye dirisha moja la usajili, baada ya matumizi ya dirisha hili la kiangazi lililofungwa usiku wa jana kuvuka pauni bilioni 3.

Jumla ya pauni bilioni 2.73 zilikuwa zimetumika hadi kufikia tarehe 31 Agosti, lakini usajili wa dakika za mwisho ukiongozwa na usajili wa Alexander Isak kutoka Newcastle kwenda Liverpool kwa ada ya rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 125, zimefanya jumla ya matumizi kufikia pauni bilioni 3.087.

Matumizi haya ni makubwa zaidi ikilinganishwa na dirisha la kiangazi lililopita, ambapo vilabu vya ligi kuu vilitumia pauni bilioni 1.96 pekee.

Kiwango cha matumizi katika dirisha hili pia ni kikukubwa zaidi kuliko matumizi yote ya usajili katika ligi ya ujerumani (Bundesliga), Hispania (La Liga), Ufaransa (Ligue 1) na Italia (Serie A).

Nani alimmwaga pesa zaidi?

Liverpool wamevunja rekodi ya usajili katika dirisha hili kiangazi. Kikosi cha kocha Arne Slot kimemsajili Isak na kupelekea matumizi yao ya usajili kwa dirisha hili tu la kiangazi kufikia pauni milioni 415 na kuweka rekodi mpya ya kiasi kikubwa zaidi kutumika na klabu moja kwenye dirisha moja la usajili.

Rekodi ya awali ilikuwa ya Chelsea, waliotumia pauni milioni 400 katika dirisha la usajili la kiangazi mwaka 2023.

Hii si tu kwamba ni zaidi ya klabu yoyote ya Ulaya, bali karibu sawa na jumla ya matumizi ya ligi zingine zote za Ulaya.

"Liverpool imeonyesha nguvu kubwa," alisema kipa wa zamani wa Manchester City Joe Hart.

"Usajili na pesa walizotumia ni za ajabu, na wamewaleta baadhi ya wachezaji bora kabisa."

Chelsea na Arsenal pia walifanya usajili mkubwa ili kuimarisha vikosi vyao na kupambana zaidi kwa ubingwa, ambapo Chelsea walitumia pauni milioni 285 na Arsenal milioni 255 mtawalia.

Lakini Chelsea pia walifanikiwa kuuza wachezaji kukusanya pauni milioni 288 kutokana na mauzo na kujipatia faida ya pauni milioni 3, huku Arsenal wakifanikiwa kupata pauni milioni 9 pekee kutokana na mauzo ya wachezaji wake, na hivyo kutumia jumla ya pauni milioni 246.

Nani kaenda wapi siku ya mwisho ya usajili Ulaya?

Dirisha la uhamisho wa majira ya joto - limefungwa Jumatatu, Septemba 1 kwa vilabu vya Ligi Kuu ya England. Mbali na kuvunja rekodi ya matumizi limeshuhudia pia nyota kadhaa wakishindwa kuhama timu zao kwa sababu mbalimbali.

Aston Villa hawakupokea ofa kutoka Manchester United kwa ajili ya kipa wa Argentina Emiliano Martinez licha ya mchezaji huyo mwenye miaka 32 kuhusishwa sana na uhamisho wa kuelekea Old Trafford.

Liverpool walikataa kumruhusu Joe Gomez, 28, kujiunga na AC Milan baada ya mpango wao wa kumsajili beki wa England Marc Guehi, 25, kutoka Crystal Palace kuvunjika.

Waliosajiliwa Ligi Kuu England

Reiss Nelson [kutoka Arsenal - kwenda Brentford] kwa mkopo

Oleksandr Zinchenko [kutoka Arsenal - kwenda Nottingham Forest] mkopo

Igor Julio [kutoka Brighton – kwenda West Ham United] kwa mkopo

Dilane Bakwa [kutoka Strasbourg – kwenda Nottingham Forest]

Bertrand Traore [kutoka Ajax – kwenda Sunderland]

Harvey Elliott kutoka [Liverpool – kwenda Aston Villa] kwa mkopo

Senne Lammens [kutoka Royal Antwerp – kwenda Manchester United] £18.1 milioni

Yoane Wissa [kutoka Brentford – kwenda Newcastle] £55 milioni

Kevin [kutoka Shakhtar – kwenda Fulham] £34.6 milioni

Brian Brobbey [kutoka Ajax - kwenda Sunderland] £21.6 milioni

Jadon Sancho [kutoka Manchester United – kwenda Aston Villa] mkopo

Alexander Isak [kutoka Newcastle - kwenda Liverpool] £125 milioni

Merlin Rohl [kutoka Freiburg – kwenda Everton] kwa mkopo

Cuiabano [kutoka Botafogo – kwenda Nottingham Forest]

Samuel Chukwueze [kutoka AC Milan - kwenda Fulham] kwa mkopo

Randal Kolo Muani [kutoka PSG – kwenda Tottenham] kwa mkopo

Piero Hincapie [kutoka Bayer Leverkusen – kwenda Arsenal] mkopo

Lutsharel Geertruida [kutoka RB Leipzig – kwenda Sunderland] mkopo

Jaydee Canvot [kutoka Toulouse – kwenda Crystal Palace]

Veljko Milosavljevic [kutoka Red Star Belgrade – kwenda Bournemouth] £13 milioni

Tolu Arokodare [kutoka Genk – kwenda Wolves] £24 milioni

Facundo Buonanotte [kutoka Brighton – kwenda Chelsea] kwa mkopo

Victor Lindelof [kutoka Manchester United – kwenda Aston Villa] bure

Alex Jimenez [kutoka AC Milan – kwenda Bournemouth] kwa mkopo

Waliokwenda kimataifa kutoka England

Jamie Vardy [kutoka Unattached – kwenda Cremonese] bure

Nicolas Jackson [kutoka Chelsea – kwenda Bayern Munich] kwa mkopo

Cyriel Dessers [kutoka Rangers – kwenda Panathinaikos]

Abu Kamara [kutoka Hull – kwenda Getafe] kwa mkopo

Jakub Kiwor [kutoka Arsenal – kwenda Porto] kwa mkopo

Fabio Vieira [kutoka Arsenal – kwenda Hamburg] kwa mkopo

Musa Drammeh [kutoka Heart of Midlothian – kwenda Torreense]

Ben Chilwell [kutoka Chelsea -kwenda Strasbourg]

Antony [kutoka Man Utd – kwenda Real Betis] £21.65 milioni

Odsonne Edouard [kutoka Crystal Palace – kwenda Lens]

Rasmus Hojlund [kutoka Man Utd – kwenda Napoli] kwa mkopo

Jeremy Sarmiento [kutoka Brighton – kwenda Cremonese] kwa mkopo

Darko Churlinov [kutoka Burnley – kwenda Kocaelispor]

Martial Godo [kutoka Fulham - kwenda Strasbourg]

Eric da Silva Moreira [kutoka Nottingham Forest – kwenda Rio Ave] kwa mkopo

Emerson Palmieri [kutoka West Ham – kwenda Marseille]

Sambi Lokonga [kutoka Arsenal – kwenda Hamburg]

Bilal El Khannouss [kutoka Leicester – kwenda Stuttgart] kwa mkopo

Norman Bassette [kutoka Coventry - kwenda Reims] kwa mkopo

Oscar Cortes [kutoka Rangers – kwenda Sporting Gijon] kwa mkopo

Abdoulaye Kamara [kutoka Portsmouth – kwenda FC Saarbrucken] bure

Tariq Lamptey [kutoka Brighton – kwenda Fiorentina]

Szabi Schon [kutoka Bolton – kwenda ETO Gyor] kwa mkopo.