Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Chelsea wataka £65m kwa ajili ya Nkunku

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea itataka ada ya pauni milioni 65 kwa mshambuliaji Christopher Nkunku, 27, huku Bayern Munich ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anayeripotiwa kutokuwa na furaha Stamford Bridge. (Athletic)
Arsenal wapo kwenye mazungumzo kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25, katika mkataba wa pauni milioni 51 msimu wa joto. (Mail)
Marcus Rashford, 27, angependelea kuhamia Barcelona kabla ya chaguo jingine mwezi huu iwapo mshambuliaji huyo ataondoka Manchester United. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 26 na Ufaransa Randal Kolo Muani . (Gazzetta dello Sport)
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 37, anaweza kujiunga tena na Barcelona kwa mkopo wakati wa msimu wa nje wa Ligi Kuu ya Soka mara tu atakaposaini mkataba mpya na Inter Miami. (El Nacional)
Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 70 kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25. (Anfield Watch)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Andre Silva, 29, kwa mkopo kutoka RB Leipzig kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu. (Guardian)
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Aston Villa wamekataa dau la pauni milioni 40 kutoka kwa West Ham kumnunua mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 21. (Sportsport)
Kiungo wa kati wa Arsenal na Italia Jorginho, 33, ambaye mkataba wake unaisha msimu wa joto, analengwa na klabu ya Brazil Flamengo. (Sky Sports)
Beki wa kati wa Ufaransa Axel Disasi, 26, ndiye mchezaji wa hivi punde zaidi ambaye anaweza kuondoka Chelsea kutokana na kukosa muda wa kucheza. (Mirror)
Newcastle wamekuwa wakimtafuta mlinzi wa kati wa England na AC Milan Fikayo Tomori, 27. (Football Insider)
Celtic ni moja ya vilabu kadhaa vinavyotaka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Muingereza Louie Barry, 21, kwa mkopo, lakini timu hiyo ya Premier League inatathmini chaguo lao. (Sky Sports)
West Ham wako kwenye mazungumzo na Marseille kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Elye Wahi, 22. (ESPN)
The Hammers pia wamemuongeza Finn Jeltsch, 18 wa Nurnberg, kwenye orodha yao ya matamanio ya msimu wa joto lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza na Bundesliga kumnasa mlinzi huyo wa Ujerumani. (Florian Plettenberg)
Mtendaji mkuu wa Saudi Pro League Omar Mugharbel anasema "ni suala la muda" kabla ya klabu kutoka ligi hiyo kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Junior, 24. (Marca)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United na Uhispania Ander Herrera, 35, anatazamiwa kujiunga na klabu ya Argentina Boca Juniors kutoka Athletic Bilbao ya La Liga. (Fabrizio Romano)
Sheffield United wametoa ofa ya pauni milioni 7 kumnunua mshambuliaji wa Leicester kutoka Jamhuri ya Ireland Tom Cannon, 22, ambaye yuko kwa mkopo Stoke. (Football Insider)












