Je, msuluhishi wa zamani wa Mandela anaweza kumvutia Donald Trump?

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Afrika Kusini amekabiliwa na changamoto kali kabla - alikuwa mpatanishi mkuu wa chama cha Nelson Mandela cha African National Congress (ANC) wakati wa mazungumzo ya kumaliza utawala wa weupe walio wachache mapema miaka ya 1990 - lakini katika mkutano wake ujao katika Ikulu ya White House atahitaji haiba yake yote.
Cyril Ramaphosa anataka kurekebisha uhusiano uliovunjika wa taifa lake na Marekani - na ujuzi wake maarufu wa mazungumzo utawekwa kwenye mtihani anapojaribu kumshawishi kiongozi huyo mwenye nguvu zaidi duniani.
Rais wa Marekani, Donald Trump na timu yake wamekuwa kimya kuhusu safari hiyo, huku Waziri wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akikataa Jumatatu kutoa maelezo yoyote au hata kukiri hadharani kwamba ziara hiyo inafanyika.
"Uhusiano wa kibiashara ndio muhimu zaidi - hilo ndilo limetufikisha hapa," Ramaphosa alisema mjini Washington siku ya Jumanne. "Tunataka kutoka Marekani na makubaliano mazuri ya kibiashara. Tunataka kuimarisha mahusiano hayo na tunataka kuunganisha uhusiano mzuri kati ya nchi zetu mbili."
Wawili hao wamekuwa wakizozana kwa miezi kadhaa, huku Trump akisisitiza mara kwa mara kwamba jumuiya ya Waafrikana inakabiliwa na "mauaji ya halaiki" - madai ambayo yameongezwa na mshauri wake wa karibu Elon Musk, bilionea wa teknolojia mzaliwa wa Afrika Kusini.
Mvutano uliongezeka siku chache baada ya Trump kuchukua madaraka kwa muhula wake wa pili mwezi Januari wakati Rais Ramaphosa alipotia saini kuwa sheria mswada wenye utata unaoiruhusu serikali ya Afrika Kusini kunyakua ardhi inayomilikiwa na watu binafsi bila kulipwa fidia katika hali fulani, wakati inachukuliwa kuwa "sawa na kwa maslahi ya umma".
Hili lilichangia tu kuchafua taswira ya uchumi mkubwa zaidi barani Afrika machoni pa utawala wa Trump ambao tayari umekasirishwa na kesi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Mwezi Februari, rais wa Marekani alitangaza kusitishwa kwa misaada muhimu kwa Afrika Kusini na akajitolea kuwasaidia watu kutoka jamii ya Waafrikana, ambao wengi wao ni uzao wa Wazungu wa walowezi wa mapema wa Uholanzi na Wafaransa, kuishi Marekani kama "wakimbizi".

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Balozi wa Afrika Kusini mjini Washington, Ebrahim Rasool, pia alifukuzwa mwezi Machi baada ya kumshutumu Trump kwa "kuhamasisha ukuu wa wazungu"
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Rasool ani "mwanasiasa mbabe" ambaye "hakubaliwi tena katika nchi yetu kuu".
Kuwasili kwa kundi la kwanza la Waafrikana nchini Marekani wiki iliyopita kulizidisha mzozo huo , huku Trump akizidisha maradufu madai yake kwamba wakulima wa kizungu walikuwa "wanauawa kikatili" na "ardhi yao inachukuliwa" , jambo ambalo ambayo limekuwa likikanushwa mara kwa mara na serikali ya Afrika Kusini.
Kulingana na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Afrika Kusini Anthoni van Nieuwkerk, uamuzi wa Ramaphosa kwenda Ikulu ya White House ni "mkakati hatari" hasa kutokana na msimamo mkali wa hivi karibuni wa Trump.
Msemaji wa Ramaphosa, Vincent Magwenya, aliiambia BBC kwamba inatumainiwa kuwa safari hiyo "itaanzisha mchakato wa kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia" na "kuweka msingi" wa kuboresha uhusiano wa kibiashara.
Ikizingatiwa kwamba yote yalikuwa yamethibitishwa kwa taarifa fupi, ujumbe wa Afrika Kusini - ambao unajumuisha mawaziri wakuu wanne wa baraza la mawaziri - walikuwa na muda mchache wa kuanzisha "programu rasmi", alisema.
Lakini alisema kuna uwezekano wa kulenga kupanua Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika (Agoa), kipande cha sheria cha Marekani kilichodumu kwa miaka 25 kinachohakikisha upatikanaji bila ushuru kwa watumiaji wa Marekani kwa baadhi ya bidhaa kutoka Afrika.
Afrika Kusini ni mojawapo ya wauzaji wakubwa wa nje chini ya Agoa, ikipata mapato ya takriban $2.7bn (£2bn) mwaka 2023, zaidi kutokana na mauzo ya magari, vito na chuma.
Kuna wasiwasi kwamba mpango huo unaweza usirudishwe upya wakati utakapokuja kukaguliwa baadaye mwaka huu au kwamba ikiwa ni hivyo, Afrika Kusini inaweza kuondolewa katika mkataba huo mpya.
"Kwa kukosekana kwa muendelezo huo au upanuzi wa Agoa, tuko tayari kuwasiliana na utawala wa Trump kuhusu mfumo mpya wa uhusiano wa kibiashara ambao tunaamini utakuwa wa manufaa kwa pande zote," Bw Magwenya alisema.

Chanzo cha picha, Reuters
Kuhusu kudorora kwa uhusiano kati ya Pretoria na Washington, alisema Afrika Kusini inatumai kuwa na "majadiliano ya wazi na yenye kujenga ".
Jambo la kushangaza Waziri wa Kilimo John Steenhuisen ni sehemu ya wajumbe. Chama chake cha kisiasa cha Democratic Alliance ni sehemu ya serikali ya mseto ya Afrika Kusini na kimekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za uwezeshaji za ANC, kikisema zinaongoza kwa urafiki na ufisadi. ANC inakanusha hili.
Akizungumzia kesi ya ICJ, ambapo Afrika Kusini iliishutumu Israel mnamo Desemba 2023 kwa kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza - madai ambayo Israel inakanusha, Bw Magwenya alikiri kuwa huenda "ilisababisha mjadala mkali".
"Kiutaratibu, hatuwezi kuondoa suala hilo [na] litabaki kwenye mzozo.
"Lakini, kuhusiana na mzozo wa kibinadamu na kuna makubaliano na Rais Trump na tutazingatia zaidi kile tunaweza kufanya pamoja katika maeneo ambayo tunakubaliana."
Siku ya Ijumaa, Trump alikiri kuwa "watu wengi wanakufa njaa" huko Gaza kufuatia hivi majuzi Israel ya kuzuia usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo - maoni ambayo yamesababisha "kiasi cha chakula" kuingia Gaza.
"Ikiwa ujumbe wa Afrika Kusini hauwezi kuushawishi utawala wa Trump wa haki ya Afrika Kusini kutekeleza uchaguzi wake wa sera ndani na kimataifa ... basi wakati wa Ofisi ya Oval itatumiwa na Trump kumdhalilisha Ramaphosa na kumsomea kitendo cha ghasia," anasema Profesa Van Nieuwkerk msomi wa Chuo Kikuu cha Afrika Kusini alisema.
"Hilo ni jambo la pili ambalo hatulitaki."
Anatumai kuwa ujumbe wa Afrika Kusini umewasili Marekani na "pendekezo la kuvutia", na kuongeza: "Mazungumzo hayawezi kuanza katika Ofisi ya Oval, mbele ya kamera. Wakati huo wa moja kwa moja lazima uwe hitimisho la mazungumzo ambayo yanapaswa kutokea mapema."
Katika matokeo haya, anasema Afrika Kusini ina uwezo mkubwa: Ramaphosa, anayejulikana kwa ujuzi wake wa mazungumzo na uchangamfu.
Anajua vitufe vya kubonyeza na kutafuta mwafaka kuhusu gofu kunaweza kuwa bembea anayocheza - mzee huyo wa miaka 72 tayari amemualika kiongozi huyo wa Marekani kwa duru ya kirafiki ya mchezo wa gofu wakati wa Mkutano wa G20 unaofanyika Afrika Kusini mwezi Novemba.
"Iwe watu kama Cyril Ramaphosa au la, tunapaswa kukiri kwamba alikuwa mmoja wa wahusika wakuu katika mabadiliko kutoka kwa ubaguzi wa rangi hadi demokrasia. Alifanikisha hilo kwasababu ya utu na mtindo wake," Prof Van Nieuwkerk alisema.

Dk Lubna Nadvi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini cha KwaZulu-Natal, anakubali rais wa Afrika Kusini ana utu wa "kushughulikia hali ikiwa mambo yatatoka nje".
"Ninatarajia kuwa mkutano huu wa ana kwa ana utaruhusu uhusiano kuimarishwa, ili ukweli kuwekwa mezani," alisema, akiongeza kuwa "propaganda" ambazo zilimshawishi Trump zinapaswa kushughulikiwa.
Ilikuwa muhimu kwa timu ya Ramaphosa kuifanya Marekani "kukubali kwamba Afrika Kusini ni nchi huru na ina haki ya kuchukua maamuzi inayotaka kuchukua," Dk Nadvi alisema.
Bw Magwenya pia alitoa hoja kwamba Afrika Kusini haitaelekea kwenye mkutano wa Jumatano "na bakuli la kuomba".
"Kama vile Afŕika Kusini inahitaji kufikia moja ya soko kubwa zaidi duniani... Maŕekani kwa usawa inahitaji baadhi ya bidhaa na bidhaa kutoka Afŕika Kusini."
Kwa sasa Afrika Kusini inasafirisha aina mbalimbali za madini kwenda Marekani, ikiwa ni pamoja na platinamu, chuma na manganese, pamoja na mawe ya thamani, metali na matunda.
"Eneo lake la kimkakati la kijiografia" pia lilifanya "kuvutia" kwa Amerika, Prof Van Nieuwkerk aliongeza.
Akichora hali mbaya zaidi, mchambuzi huyo alisema: "Kuna wahusika ambao wangependa kuona tunashindwa na kisha kuingilia kati na ... kuondoa jukumu letu barani Afrika. Hii ndio bei tutakayolipa ikiwa itaenda vibaya katika Ofisi ya Oval".
Lakini Bw Magwenya alikuwa na uchungu kueleza kwamba mkutano wa Ikulu haukuwa "mkingo" wa kupata suluhu.
"Inachowakilisha ni mwanzo wa mchakato wa kusuluhisha mkwamo uliopo na kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia," alisema.
"Iwapo mkutano huo una matokeo mabaya au chanya, itakuwa fursa kubwa kwetu kuanza kurejesha uhusiano."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












