Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Tottenham wakubaliana na Bayern Munich kumnunua Mathys Tel kwa dau la £50m
Tottenham wamekubali mkataba wa £50m na Bayern Munich kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Mathys Tel, 19. (L'Equipe - kwa Kifaransa), nje
Hata hivyo, Manchester United inalenga kumuuza winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho na kumleta Tel kwa mkopo (Independent}
Tel angependelea kuhamia Old Trafford kuliko Arsenal, Chelsea na Tottenham na anasubiri kuona iwapo nia ya United ni thabiti kabla ya kufanya uamuzi.{i Sport}
Al-Nassr wanapanga kutoa ofa ya pili na ya mwisho kwa winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma mwenye umri wa miaka 27 yenye thamani ya £90m. (CBS Sports)
Arsenal wamemzuia beki wa kushoto wa Scotland Kieran Tierney, 27 kuelekea Celtic msimu ujao. (Telegraph – Subscription Required)
Mshambulizi wa Paris St-Germain na Uhispania Marco Asensio, 29, ni mmoja wa wachezaji washambuliaji ambao Aston Villa wanavutiwa kuwasajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Mail)
Mshambuliaji wa Uingereza Ollie Watkins atakuwa tayari kujiunga na Arsenal mwezi huu lakini Aston Villa wamedhamiria kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Mail)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ureno Joao Felix, 25, analengwa na mkufunzi wa Villa Unai Emery. (Express)
Al-Hilal wametoa "ofa kubwa" kwa winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, kama mbadala wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 32. (Marca)
Monaco wanakaribia kuafikiana na Ajax kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson, 34. (Fabrizio Romano)
Everton wanatathmini dau la kuchelewa la kumnunua mshambuliaji wa Brighton mwenye umri wa miaka 20 na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson. (i Sport)
Chelsea wanavutiwa na mlinda lango wa Borussia Dortmund na Uswizi Gregor Kobel, 27, ingawa kuna uwezekano wa kuhama katika msimu wa joto. (Independent)
Kiungo wa kati wa Wolves Muingereza Luke Cundle, 22, anakaribia kukamilisha mkataba wa kudumu na Millwall. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla