Serena Williams atangaza 'kuondoka' kutoka mchezo wa tenisi

serena

Chanzo cha picha, Getty Images

Serena Williams amesema kuwa amepanga kujiuzulu mchezo wa tenisi, akisema kuwa atakuwa "anaondoka " katika mchezo huo baada ya shindano la tenisi la US Open.

Akiandikia jarida la Vague mshindi huyo wa taji la Grand Slam mara 23 amesema anaondoka kufanya ’’mambo mengine’’ ambayo ni muhimu ", akiongeza kuwa hapendi neno "kustaafu".

Katika ujumbe huo ulioambatanishwa kwenye Instagram , aliandika kwamba "ameanza kuhesabu siku kabla ya kujiuzulu".

"Nitakuwa na furaha wiki hizi chache zijazo ," alisema Serena mwenye umri wa miaka 40.

Serena

Chanzo cha picha, Getty Images

Williams alirejea katika Wimbledon mwezi Juni baada ya kujiengua kutokana na jeraha la muda mrefu ambalo liliibua tetesi za kustaafu kwake.

Alisema kuwa atacheza katika US Open, wambako alishinda mataji sita miongoni mwa mataji yake makuu, baadaye mwezi Agosti.

Williams ameshinda mataji makuu kuliko mwanamke mwingine yoyote katika enzi ya Open na ni mchezaji wa pili bora kuwahi kushuhudiwa, baada ya Margaret Court ambaye alishinda mara 24.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Instagram ujumbe