Serena Williams kuikabili Uholanzi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa Tenisi mkongwe wa Marekani Serena Williams ameitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Marekani ya Fed Up dhidi ya Uholanzi.
Serena, mchezaji namba moja wa zamani, ambaye hivi karibuni alibahatika kupata mtoto (Alex Olympia) mwezi Septemba, hivi karibuni alirejea tena dimbani mjini Dubai mwezi ulipopita.
Wakati wa ufunguzi wa michuano ya wazi ya Australia alisema asingeweza kurejea tena kushiriki mashindano.
Serena ataungana na wachezaji wengine kikosini akiwemo dada yake Venus,Coco Vandeweghe, Nahodha wao Kartny Rinald anatarajia kuwaita kikosini wachezaji wanne kwaajili ya Michezo mitano ambayo itafanyika kaskazini mwa mji wa Karolina.








