Je ni kwanini wanafunzi hawa wanaletewa mbwa shuleni?

mtoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Huenda unajiuliza je ingewaje kama ningeenda shule kusoma na mbwa wangu?

Mkuu wa shule ya moja ya mshingi nchini Uingereza amewavutia wengi kwa kumuweka mbwa darasani.

Karen Towns, ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Randailo Elementary iliyopo Carmadenshire, Wales, amekuwa mstari wa mbele katika kuwaweka mbwa katika madarasa kwa kipindi cha muongo mzima uliopita ili wasaidie kuboresha afya ya wanafunzi.

Mbwa wake binafsi wa nyumbani wa mwalimu Towns, kwa jina Millie, aina ya West Highland Terrier, kila mara huwa na wanafunzi wakati wanapokuwa darasani ili kusidia kudhibiti hisia zao.

"Kuna utani usemao kwamba usiwaajiri watu wasiopenda mbwa," Mwalimu Towns aliiambia BBC.

"Waalimu wote walimtaka mbwa," aliongeza.

"Tumepata ule utulivu, hali ya unyumbani kusema kwenye unasaidia sana wanafunzi kuhusika na kutiwa hamasa ya kwenda shule. Hilo ndio lengo letuu kuwa na mbwa katika kila darasa ."

"Mahudhurio ya wanafunzi yamekuwa bora zaidi na tabia za wanafunzi zimekuwa bora zaidi," Towns alisema."Wafanyakazi pia hutumia mbwa katika kuimarisha hali zao pia. Kwa mfano, mara nyingine utawasikia wakisema, nilikuwa na siku ngumu leo, ninaweza kucheza na mbwa?' Hivyo ndivyo ilivyo, kwa hiyo la muhimu ni kwamba kuna faida nyingi sana za kuwa na mbwa katika shule."

mbwa
Maelezo ya picha, Shule ya msingi ya

Mwanafunzi kutoka shule ya msingi ya Randallo alisema kuwa mbwa walimsaidia kuondoa wasi wasi alipojiunga na shule hiyo katika siku ya kwanza ya shule.

Hata kucheza na mbwa Millie na kumsomea kitabu imedhihirisha kuwa njia yenye ufanisi ya kuwafanya wanafunzi watulie katika masomo yao na kuelezea hisia zao.

 Samia alianza kuhudhuria shule baada ya familia yake kuhamia katika eneo la Landalo hivi karibuni.

“Nilipoenda kwa mara ya kwanza shuleni, nilifurahi, lakini nilikuwa na uoga pia , alisema Samia. “Lakini nilikutana na Rosie shuleni, na mbwa yule alinifanya nisijihisi mpweke sana na kujihisi mwenye furaha zaidi.”

"Ninadhani ni jambo la kufurahisha kusema kweli kuwa na mbwa shuleni, kwasababu kucheza naye wakati umesikitika kidogo inakufanya ujihisi vyema."

Mwalimu mkuu Karen Towns
Maelezo ya picha, Millie akiwa pamoja na Mwalimu mkuu

Mbwa wa Mwalimu mkuu Karen Towns Millie kila mara yuko pale kutoa usaidizi kwa wanafunzi.

Mwalimu Towns anasema mbwa walitoa usaidizi kwa wanafunzi hususan wale wanaohitaji usaidizi wa ziada wakiwemo mwanafunzi msichana mwenye umri wa miaka 10 mwenye tatizo la kiafya la autistic ambaye awali alikataa kuhudhuria shule kwasababu hapendi mbwa.

Mwalimu Towns humtoa mbwa Millie kwa watoto baada ya kuwahakikishia wazazi wa wanafunzi kwamba njia ya mbwa itafanya kazi.

"Sasa Millie amekuwa sehemu ya maisha ya mwanafunzi," Towns ansema na kuongeza kuwa. "Millie ni sababu pekee inayowafanya wanafunzi waende shule."

Dr. Helen Lewis, ambaye ni profesa msaidizi wa elimu Chuo kikuu cha Swansea , alifanya utafiti kuhusu matumizi ya mbwa katika shule akitumia waalimu zaidi ya 1000 kote duniani.

"Baada ya COVID-19 na sheria ya kukaa nyumbani, baadhi ya watu walijipata katika matatizo makubwa katika maisha ya kijamii," Lewis alisema.

Mbwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa wa kutuliza mawazo hutumiwa katika vyuo vikuu na vyo vingine nchini Marekani

"Baada ya hilo, shule nyingi zilisema, 'Ukweli kwamba mbwa atakuwa darasani leo ni jambo lililowafanya watoto kushiriki masomo kwa ari zaidi ,'" alisema.

Mbwa wote waliopelekwa katika shule ya msingi ya Randallo walipewa mafunzo ya kuishi katika mazingira yanayochosha kiakili na yenye kelele.

Shirika la misaada linaloendeshwa na Wakfu wa Kidwelly's John Burns limebobea katika utoaji wa mafunzo ya mbwa ili wawasaidie watoto kusoma.

"Bila shaka, mbwa wanapaswa kufurahia kutembelea shule," alisema Katie Gardner, mmoja wa wakufunzi wa mbwa.

“Shule zote tunazoshirikiana nazo zinaelewa kuwa mbwa hupitia mafunzo ya wiki 16. Tunawaambia wahudumu wetu wa kujitolea kuwa mafunzo yanaweza kwa zaidi ya wiki 16. Hatmaye wanagundua kuwa mbwa anafaa kwa ajili ya shule. Kwasababu inawezekana."

Wanafunzi wakicheza na mbwa waokwa jina Allie
Maelezo ya picha, Wanafunzi wakicheza na mbwa waokwa jina

Sheria ya jimbo la Carmadenshire State inaunga mkono mpango wa mbwa shuleni.

Waziri wa elimu Glinging Davis alisema: " Shule ya msingi ya Randailo imefanikiwa kufanya shughuli nyingi katika kanda. ..

Msemaji wa serikali ya Wales aliongeza kuwa: "Shule zinaweza kupanga kuweka Wanyama wanaofugwa nyumbani shuleni kulingana na tathmini yao wenyewe ya hatari."