Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu siri za rangi mkojo wako
Sio jambo zuri la kuzungumzia , lakini hatuwezi kukataa kwamba ni miongoni mwa maisha yetu kujifunza ni nini kinachofanyika kabla ya mkojo kutoka mwilini mwetu.
Hivyobasi tunaanza kwa kuangazia eneo ambalo mkojo huanza kutengenezwa: figo
Kwa wanadamu figo zina ukubwa wa ngumi, rangi nyekundu, na zipo katika upande wowote wa mgongo, chini kidogo ya kiuno.
Moja ya kazi zake kuu ni kudhibiti kiasi na muundo wa maji ya mwili.
Kwa kufanya hivyo, figo huchuja kiasi kikubwa cha plasma: kati ya mililita 1,000 na 1,500 za damu hupita kupitia figo kwa dakika.
Baada ya kufyonza tena zaidi ya kile kilichochujwa, kuna suluhisho lililokolea la taka ya kimetaboliki ambayo tunaijua kuwa mkojo, ambayo lazima iondolewe.
Kwa maneno mengine, figo zinafanya kazi kwa bidii ili kuondoa taka au sumu, na kushikilia maji unayohitaji ili mwili wako ufanye kazi.
Mkojo ni mchanganyiko wa hizo sumu na maji ya ziada.
Zinapomaliza kazi yao, mhusika mkuu mwingine wa hadithi hii anaingia katika eneo: kibofu.
Inakaribia kupasuka!
Vibofu vina uwezo mkubwa wa kufura.
Tazama jinsi kibofu hiki kutoka kwa nguruwe kinavyofura :
- Anza na ukubwa wa sura ya tunda la pear.
- liInapojaa, nyuzi za uso huvimba.
- Shinikizo linazidi kuongezeka...
- Mpaka sensa zinapokwambia kwamba unapaswa kwenda bafuni.
Kwa nini mkojo wako una rangi tofauti?
Unachokula na kunywa kinaweza kubadilisha rangi ya mkojo wako au wakati mwingine kuonyesha kuwa hali sio nzuri .
Wekundu wa uwa la Waridi
Mkojo wa rangi ya uwa la waridi au mwekundu unaweza kukufanya usiwe na wasiwasi, lakini sababu inayowezekana zaidi ni kwamba ulikula kitu chekundu kwa hivyo usijali.
Hata hivyo, kitu kingine ambacho kinaweza kugeuza mkojo wako rangi hiyo ni damu. Katika hali nyingi, hakuna sababu ya kuwa na wasiwas, lakini ni bora kuona daktari, hasa ikiwa itaendelea hivyo kwa zaidi ya siku moja na unasikia maumivu unapokojoa .
Njano Nyepesi
Hii ndio rangi bora zaidi!
Rangi ya njano hutolewa na asidi ya uric. Lakini jinsi mkojo wako unavyozidi kuwa mweusi, ndivyo asidi ya uric inavyoongezeka. Ndiyo maana njano nyepesi ni rangi ya sawa.
Nyeupe ya uwazi
Ikiwa mkojo wako umepauka sana au hauna rangi kabisa, unaweza kuwa umekunywa maji mengi sana.
Katika hali mbaya, kunywa maji mengi kunaweza kuwa kubaya, kwani maji hayo huchukua pamoja na vitu muhimu ambavyo mwili unahitaji, kama vile chumvi.
Njano iliokolea/machungwa
Ikiwa mkojo wako una rangi kama ya asali, ni ishara kwamba haujapata maji ya kutosha.
Kadri rangi hiyo inapozidi kuwa kali inamaanisha kiwango cha juu cha asidi ya uric, na hiyo si nzuri, hivyo unapaswa kunywa maji Zaidi.
Rangi ya Kijani
Hii inaweza kuwa matokeo ya aina ya chakula ulichokula.
Kwa watu wengine, asparagus husababisha mkojo kugeuka kijani na kuwa na harufu kali.
Kitu kingine ambacho kinaweza kusababisha mkojo wako kuwa kijani, au mawingu, ni maambukizi.
Pia, unaweza kuhisi kuchomeka unapoenda bafuni.
Kwa kawaida, hii ni ishara kwamba kitu si sahihi na unahitaji kuchunguzwa.
Povu
Ikiwa mkojo wako unatoa povu kama vile soda unapoanguka kwenye choo, huenda unakojoa haraka sana, au kuna sabuni ndani ya maji.
Lakini ikiwa daima ni povu, nenda kwa daktari, kwa sababu unaweza kuwa na shida na figo zako.
Je unahisi kwenda msalani?
Je, ni kawaida kukojoa mara ngapi kwa siku?
Mara tatu au chini yake
Hii ni ya chini na inamaanisha kuwa labda hunywi maji ya kutosha wakati wa mchana, haswa ikiwa mkojo wako ni mweusi sana.
Mara nne hadi nane kwa siku
Hii ni kawaida na inaonyesha kuwa labda unachukua kiasi sahihi cha maji.
Zaidi ya mara tisa
Hii ni zaidi ya kawaida, lakini ikiwa unakunywa sana, utahitaji kuondokana na maji mengi. Ikiwa hautumii sana, ni bora kwenda kwa daktari.