Mwanamume wa Burundi ambaye aliamua kuvaa kama mwanamke

Na Gildas Yihundimpundu

Mwandishi Bujumbura

Samweli Minani amejitenga kabisa na jinsia ya kiume kwa kuvaa nguo za kike, na kwa tabia kama za wanaume.

Mwanamume huyo, ambaye ana umri wa zaidi ya miaka 40, anasema: “Kuna nyakati ambapo mimi hutembea na kusikia watu wakiniambia ‘'toka shetani!’

“Warundi wengine ni ‘hatari’ kweli wengine wananiambia ‘'toka shetani !,wengine wanasema ‘hilo ni PD’,...[lipenzi la jinsi moja] sijui maana yake ni nini, hata siwaelewi, japo tu ni neno ambalo kwa kweli halinifariji."

Mwanaume huyo hathamini watu wanaomwita majina ambayo wazazi wake walimpa. Anajiita Bebi (Mtoto). Mara nyingi watu ambao hawamuiti hivyo huwa hawajibu.

Hapa ni Kamesa, kwenye vilima vya Bujumbura. Ni saa tatu asubuhi tumekuja kuzungumza na mwanaume aliyechagua kuishi maisha yanayofanana na ya wanawake.

Akiwa nyumbani, amevaa sketi yenye mpasuo na blauzi fupi ambayo wasichana wanapenda kuiita "TOP".

Alitoka nayo ndani ya nguma huku akiwa na brashi, wanja, lipstiki nyekundu, poda, na vifaa vingine vya urembo ambavyo kwa kawaida hutumiwa na wanawake au wasichana.

Alionekana mwenye tabasamu , "Karibu." alinikaribisha.

Mara akaketi mbele ya mlango na kuanza alianza nilibaini kuwa alikuwa na vidole vyenye kucha ndefu zilizokuwa zimepakwa rangi nyekundu.

Ni vigumu sana kumtofautisha na wanawake. Mtuonekano, kutembea kwake , na hata sautisauti,... Hata hivyo ni mtu mwenye mke na watoto wanne.

Ilikuwaje akawa hivi?

Samuel Minani anaishi katika vilima vya jiji la Bujumbura. Ni moja wapo ya maeneo yaliyokumbwa na vita vikali vilivyotokea nchini Burundi kuanzia 1993 hadi 2000

Anaamini kwamba vita hivi ni sehemu ya kile kilichomfanya awe hivi anavyoonekana leo. Anasema kuwa ilifika wakati askari au watu wenye silaha walikuja na kuwachukua wavulana na wanaume na kuwadhuru.

Katika kuishi kwake alivaa nguo za kike. Alisema: "Wakati ulifika, unajua mambo ya vita, wakaja na kutukuta mahali tulipokimbilia, nikasikia sauti ikiniambia nijifiche.

"Nilihisi labda wakati wangu wa kufa umefika. Kwa hiyo nilihitaji kujibadilisha kuwa mama. Basi nilifanya hivyo na hilo liliniokoa. Walipoona sisi sote ni kina mama walirudi nyuma..."

Tangu wakati huo, hajavua nguo za kiume tena.

Kazi ya nyumbani

Baada ya Minani kumaliza kupika aliungana na mkewe kuchuma mboga za kupika.

Wanazichambua huku wakiwa wameketi kwenye uzio, na watoto wao kando yao.

Minani, ambaye ni 'Baby', anasema kuwa yeye hupenda kusaidia kazi za nyumbani kila mara.

Alisema, "Ninakili, natandika kitanda, kufua nguo, kuwaogesha watoto, na uwaweka kitandani ... kama unavyojua kazi ya nyumbani."

Mwanaume huyu anasema kwamba wakati anahitaji kucheza, anapenda michezo ya wanawake, na kwamba haoni aibu nayo.

Alisema, "Mimi pia hucheza michezo ya akina mama. Vitu vinavyoitwa Horos, n.k... Ninahisi kama kuishi katika 'mitindo' hii hakunisumbui."

Anasema mara nyingi yeye na mkewe huwa wanagawana nguo na hata kushirikikishaba kubeba wanayobeba wanapokwenda kwenye sherehe japo kila mmoja ana lake.

Anasema huwa wanahakikisha wamenunua mikoba mizuri ya bei ya juu na bora zaidi, ya kudumu. "Tunajipenda, tunai hadhi yetu wenyewe''

"Kuna wakati unakuta nimevaa nguo zake na yeye anavaa zangu. Na linapokuja suala la kusafisha nguo mimi ndiye ninayezitunza..."

Kazi ya kitaaluma

Minani ni mtaalamu wa kutengeneza simu, redio na vifaa vingine vya kielektroniki.

Lakini hufanya shughuli hizi akiwa amevaa kama mwanamke. Inawafanya baadhi ya wateja wasiomfahamu kushangaa.

Anasema kuna wakati anapanda hadi juu y nyumba ya mteja kutengeneza umeme au kuning'iniza vifaa vya kunasa nishati ya jua vya sola, huku watu wankimshangaa sana. Baadhi hufidhani ni mwanamke ambaye alikuwa amepanda juu.

Lakini anasisitiza kuwa kazi hiyo anaifaya kwa ajili ya kuitunza familia yake.

"Ni zawadi ambayo nimekuwa nayo tangu nikiwa mtoto," alisema.

Je, majirani wanamwonaje?

Japokuwa wanaamini wanaishi naye vizuri, majirani wa Minani wanaongea na unaweza kuhisi kuna kitu hawaelewi kuhusu tabia yake.

Sabina Nahimana anaishi takriban mita 40 kutoka kwa nyumba ya Minani. Anasema kwamba alishangaa sana kuona mwanamume akivaa kama mwanamke.

Anasema, "Tunaishi naye vizuri kusema kweli. Lakini nilishangaa sana nilipomwona. Mwanaume atengeneza nywele saluni , anajipaka wanja na poda,na kuvaa gauni ...

“Ni kweli nina tatizo, huwa nafikiria kwanini alifanya hivyo, sipati jibu...

"Mimi kusema kweli kijana anayetaka kuninichumbia akiwa amevalia hivyo, siwezi kumkubali."

Na majirani wengine wa 'Baby' wanaonekana kuhisi vivyo hivyo.

Mke wake wa kwanza alitalikiwa. Walikuwa na watoto wawili. Sasa yuko na Denise Irambona. Pia wana watoto mbili pamoja.

Wakati katika jamii watu wanaanza kuzungumza kuhusu mumewe, kwa Irambona hilo sio tatizo.

“Nilianza kumuona akiwa amevaa na nikamuuliza kwa nini amevaa, akanijibu kuwa anahisi anataka kuvaa.

“Nikamuuliza itakuwaje maana yeye ni mwanaume, akaniambia hiyo ni ‘style’ yake, nikamruhusu.

"Kuna watu waliniambia nitalikiane naye, nikasema, 'Kwa nini kwa sababu ya hilo?' yuko hai, ana nguvu, amevaa, anahemea.' Na tunaishi vizuri."

Inavyoonekana, inaweza kuchukua muda mrefu kwa watu wa Kamesa kumuelewa 'Baby'.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi