Mama yake Foley: 'Saa nne na mwanamgambo aliyemuua mwananangu’

Foli
Maelezo ya picha, Diane Foley (kulia) alikutana na Alexanda Kotey (kushoto), mmoja wa wajumbe wa kundi la Islamic State ambao walihusika na kifo cha mtoto wake wa kiume.

Wanaume wawili ambao walisaidia kumuua mwandishi wa habari Mmarekani James Foley kama sehemu ya kampeni ya ugaidi wa kundi la Islamic State wanakabiliwa na sheria nchini Marekani. Mmoja wao anahukumiwa kwa mauji tarehe 19 Agosti. Mama yake james aliketi ana kwa ana naye.

 Ilikuwa ni asubuhi yenye baridi katika jimbo la Virginia mwaka jana wakati Diane Foley alipoketi mkabala na mwanaume aliyemteka na kumuua kijana wake, akimuangalia usoni moja kwa moja wakati walipokuwa wamekaa katika chumba cha mahakama ambako baadaye alifungwa kifungo cha maisha jela.

Alipoingi katika chumba hicho, Alexanda Kotey alikuwa tayari ameketi katika chumba hicho ambacho kilikuwa na shughui nyingi za na kelele za mawakala wa FBI na mawakili wa utetezi pamoja na watu wengine waliokuwa wakifuatilia kesi.

Lakini wakati alipoketi chini , "ilikuwa ni kama nilikuwa nimeketi mimi tu na yeye. Tuliangaliana na kusema 'hello'".

 Mawazo na uzito wa kihisia kutokana na namna alivyohisi alipokuwa naye vilimfanya ajihisi mchovu alipokuwa akielezea muda aliokuwa ameketi na muuaji wa mwanaye

"Halikuwa jambo rahisi kulifanya, lakini ilikuwa ni muhimu ," alisema. "Jim angependa mimi nifanye hili."

 "Jim" likuwa mwanaye wa kiume, mwandishi wa habari wa Marekani James Foley.

Mauaji yake katika mwaka 2014 mikononi mwa tawi la kikundi cha ugaidi kinachofahamika kama 'Isis Beatles' yalifahamika kpte duniani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Kikundi hicho hutekeleza ugaidi katika maeneo ya Iraq na Syria, na kuwalazimisha mamilioni ya watu kuishi chini ya utawala wa kikatili.Wakati kikundi hicho kilipotawala zaidi kati ya miaka ya 2014-2017 kilikuwa ndio kikundi cha kigaidi kinachoogopwa zaidi duniani.

Kifo cha James, ambacho kilitangazwa kwenye Twitter tarehe 19 Agosti, 2014, na kimekuwa ni moja ya vifo vilivyotambuliwa zaidi na vyenye picha za kudumu zaidi katika nyakati hizi: Kijana mdogo aliyepiga magoti akiwa amevalia vazi la ovaroli la rangi ya chungwa katika jangwa. Mwanaume aliyekuwa amevalia barakoa iliyofunika uso mzima akiwa amesimama kando yake huku akiwa ameshikilia kisu. Ukataji wa kichwa ulifanyika huku picha ya video ikichukuliwa kwa kamera.

 Video ilikuwa na kichwa cha habari "Ujumbe kwa Marekani ."

Miaka saba baadaye, Waingereza wawili - Elshafee El Sheikh, 33, na Kotey, 38 – wamepatikana na hatia ya mauaji katika mahakama ya Marekani kwa kuhusika kwao katika mauaji tawi la IS.

El Sheikh anatarajiwa kuhukumiwa Virginia siku ya Ijuamaa. Mwezi Aprili, Kotey alifungwa maisha jela, na Diane alikutana naye.

 Saa nne walizoketi naye, kwake zilikuwa ni uthibitisho waimani yake, kusamehe na kujitolea kwa kile ambacho sasa kimekuwa kazi ya maisha yake baada ya kusikitishwa na kifo cha mwanaye wa kiume - kuwafungua mateka kote duniani.

 Sio maisha ambayo aliyatarajia Diane, mwenye umri wa miaka 72 sasa angeyaishi.

 Kabla ya kutoweka kwa James nchini Syria katika mwaka 2012, amekuwa akifanya kazi kama muuguzi (nesi), lakini katika wiki kadhaa baada ya kutoweka, aliacha kazi yake.

 Haikuwa mara ya kwanza kutekwa nyara wakati akiripoti taarifa.

 Mwezi Machi 2011 James na wafanyakazi wenzake walitekwa ntara nchini Libya na utawala wa Kanali Muammar Gadaffi, lakini aliachiliwa baada ya siku 44 baadaye. Mara hii, mambo yaliisha tofauti.

James aliondoka kuelekea Syria mwezi wa Oktoba 2012 kuripoti mzozo uliokuwa ukiongezeka. Akifahamu uwezekano wa hatari, alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na familia yake.

 Lakini kufikia Novemba, sherehe ya Thanksgiving ilipita bila kuwasiliana naye na Diane hakupata mawasiliano kutoka kwa kijana wake. Baada ya mwezi mmoja baadaye ndipo alipopokea ujumbe wa barua pepe. Ulikuwa ni kutoka kwa watekati wa James.

 Kikundi cha kigaidi kilisema kwamba iwapo familia ya James ilitaka arudi, watatakiwa kuiambia serikali ya Marekani iwaachilie wafungwa maarufu wa Kiislamu au watoe Euro milioni 100.

Madai sawa na hayo pia yaliyolewa kwa familia ya mateka wengine wa Kimarekani ambao walitekwa na kikundi hicho cha ugaidi -wanaharakati wa haki za binadamu Kayla Mueller na Peter Kassig, na mwandishi wa habari Steven Sotloff.

 Wiki na miezi ikaendelea, lakini familia ilikuwa na matumaini kwamba James "angekuja nyumbani wakati wa Krismasi ",anasema Diane.

 Familia ya Forleys waliambiwa na serikali ya Marekani wasifanye mashauriano. Kulingana na Diane, hata walitishiwa na waendesha mashitaka iwapo wangejaribu kuchangisha kikombozi wenyewe, ingawa wizra ya mambo yan je ya Marekani inakanusha hili.

 Miezi ikasonga na kisha familia ya Foleyikapokea ujumbe mwingine uliowatisha kwa kifo cha James kutokana na mashambulio ya ndege za Marekani. "Atanyongwa kutokana na uchokozi wa nchi yako dhidi yetu ," ulisema ujumbe.

Alielezwa kuhusu mauaji ya James na mwandishi.

"Nilifikiri ni mzaha fulani wa kikatili," alikumbuka.

 Wiki kadhaa baada ya mauaji ya James, kitengo hicho cha ugaidi kiliendelea kumtesa, kumpiga na kuwanyima chakula na hatimaye kuwauwa Peter na Steven. Kayla alifariki mwaka 2015 – mauaji yake hayakuwahi kuonyeshwa kwenye video.

Mwaka ule, ndege zisizokuwa na rubani za Marekani zilishambulia na kumuua Mohammed Emwazi, mwanamgambo ambaye alionekana kama kiongozi mkuu wa kikundi hicho. Lakini ilichukua muda hadi mwaka 2018 kwa wengine wawili, Elsheikh na Kotey, tkukamatwa na kikundi cha wanamgambo wa Kikurdi kinachoungwa mkono na Marekani nchini Syria, na baadaye kuchukuliwa katika mahabusu ya Marekani.

 Mwanaume mwingine, Aine Davis, alikuwa katika jela ya Uturuki na sasa yuko Uingereza, ambako alikamatwa kwa mashitaka ya ugaidi.

Familia za wale waliotekwa nyara walishinikiza wawili hao wahamishiwe nchini Marekani na kushitakiwa katika mahakama ya shirikisho badala ya kushikiliwa katika mahabusu ya kijeshi katika Guantanamo Bay..

 Njia ya kutafuta haki imekuwa ngumu, anasema. "Imechukua karibu miaka 10 kupata wakati huu."

James Foley, mwana wa kiume wa Diane, alikuwa mwandishi wa habari
Maelezo ya picha, James Foley, mwana wa kiume wa Diane, alikuwa mwandishi wa habari

Kesi ya Kotey, tofauti na ya El Sheikh, haikwenda mahakamani. Badala yake alikirimashitaka manane juu ya utekeji, mateso na kuwakata vichwa mateka wa IS Syria, na kukubali kukutana na familia za wahanga, Diane alikubali.

 Katika chumba kile kidogo huku akimtazama kwa mshangao .

"Alikuwa anatisha, lakini bila shaka, kwasababu nilijua niko salama, na kwamba asingeweza kunidhuru tena, nilikuwa na nguvu kiasi ," alisema Diana.

 "Alikuwa tayari amefanya mabaya zaidi na alikuwa tayari amemchukua mpendwa wangu."

 Ilikuwa ni wakati was aa nne za kuketi naye, alisema kwamba alikuja kumhurumia gaidi ambaye sasa anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

 "Nilitaka Kotey kukabiliana na tisho la ugaidi ambao aliufanya," alisema, kwa kumueleza kuhusu mwanaume aliyemuua, ambaye alikuwa ndiye mwanaye mkubwa kati ya watoto watano.

 "Ili aelewe uzuri aliouangamiza na ni kwanini watu kama James walikuwa Syria.

 Ni kwasababu walijali na walitaka kuripoti ukweli kwa dunia.

Koteylisikiliza kimya na halafu pia alizungumzia kuhusu familia yake

"Alisema kuwa amekuwa akimuomba Mungu wake amsamehe. Alinionyesha picha ya familia yake, ana watoto wadogo ambao huenda asiwahi kuwaona tena. Ilinifanya nigundue ni kwa kiasi gani alipotea kufuatia chuki na propaganda. Ilinifanya nimhurumie."

Lakini hakumwambia Diane kamwe mahali ilipo miili ya mateka ambao yeye na washirika wake waliwazika.

 Hadi leo hawajawahi kupatikana.

"Na hakuwahi kusema pole. Aliwa mwenye huzuni na mwenye heshima kwangu na kuzungumzia kuhusu majuto aliyonayo ", lakini hakuomba mshamaha, alisema Diane.

 Wakati alipogeuka kuondoka kwa mara ya mwisho, Diane alikuwa na ujumbe kwa mtu aliyemuua mwanaye. "Nilimwambia kwamba natumai wakati mmoja sote tutaweza kusameheana," alikumbuka.

 Anakumbuka kuwa alimtazama na kusema : "Sio lazima nikusamehe kwa chochote."

 Anasema ni katika Imani yake ya Kikatoliki -ambayo ni msingi wa nguvu alizo nazo na hilo ndilo limemfanya aendelee na maisha

"Najua sio lazima anisamehe kwa lolote, lakini katika wakati ule …Sijui."

Alikuwa kimya, akitafuta maneno ya kusema.

 "Ninahisi tu kama, binadamu, hakuna yeyote aliye mkamilifu. Sote huwa tunafanya vitu ambavyo tunavijutia." "Iwapo nitawachukia, watakuwa wameshinda. Wataendelea kuniteka kwasababu siko tayari kuwa tofauti na jinsi walivyokuwa kwa mpendwa wangu. Tunapaswa kuomba kwa ajili ya ujasiri wa kuwa kinyume ."

 "Ni safari ngumu kuelekea msamaha, na sio jambo ambalo limeisha lakini hilo ndilo ninalotaka kufanya."

Foli

Katika wiki tatu baada ya mauaji ya James, Diane alianzisha kitu fulani, ambacho anasema sasa kinampa malengo ya maisha yake: Wakfu James W Foley Legacy. Unaitaka serikali kufanya juhudi zaidi kuwasaidia Wamarekani waliotekwa njyata katika nchi za ng’ambo.

Kazi yake imemfanya nguvu ya kisiasa – familia nyingine za mateka zimemuelezea Diane kama "asiyesimamishwa".

 "Serikali inapaswa kuwasaidia wananchi wetu wanaposafiri katika mataifa mengine," alisema.

 "Wanahitaji kuwa vitu vingi vya kutumia : vikwazo, misaada ya kibinadamu, chanjo au visa, chochote kinachofungua njia za kibinadamu ili tuweze kuzuia tisho la utekaji nyara wa kimataifa ."

 Lakini kwa yote hayo, maumivu hayajaisha kwake na kwa familia yake, anakiri.

"Ni vigumu sana kwa makaka na madada wa Jim, na mume wangu. Sote katika familia tuna msongo wa mawazo na kiwewe ."

Daughter of ISIS 'Beatles' victim: 'I will never forgive'
Maelezo ya picha, Binti wa mhanga wa ISIS 'Beatles' anasema hatawahi kusame

Kama sehemu ya sharti la kutoka katika mamlaka za Uingereza , Kotey na Elsheikh hawatahukumiwa kifo.

 "Ninashukuru kwa hilo," Bi Foley alisema. "Wana kipindi cha maisha yao kilichobaki cha kufikiria kile walichokifanya.

"Wamekosa uhuru wao, uraia wao, familia zao. Chuki yao haikushinda ."