Afrika wiki hii kwa picha

G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Muajiriwa wa ukumbi wa sinema nchini Ufaransa. Pathé akitembea katika ukumbi wa filamu mpyauliofunguliwa katika mji mkuu wa Senegal Darak, Ijumaa . Ukumbi huu umeelezewa kama ukumbi mkubwa zaidi wa sinema Afrika Magharibi

Hizi ni baadhi ya picha bora zaidi kutoka bara la Afrika na nje yake:

G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mvulana wa Afrika Kusini akivuta baiskeli katika tukio lililoandaliwa na wahudumu wa Soweto Street Fighters crew Jumamosi, ambapo mamia ya vijana katiika mji wa Soweto wanakusanyika kushindana katika mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na na ni nani anayeweza kudensi vyema, na ni nani mwenye baiskeli yenye muonekano mzuri zaidi ya wengine
G

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kuna shughuli zaidi nchini Tunisia siku hiyo kwani shirika la sanaa la Istambali linafanya onyesho katika mji mkuu Tunis linaloitwa Mouldia, kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Mohammad, linafahamika kama Mawlid...
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kulikuwa na sherehe zaidi za Mawlid nchini Morocco, ambako wanawake hawa walihudhuria sherehe ya kidini katika al-Aarouikatika jimbo la kaskazini-mashariki la Nador
G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku iliyofuatia, ya Jumapili, wanamitindo hawa wa kiume walishiriki katika maonyesho ya mitindo kwa ajili ya mwanamitindo Stefano Ricci, katika hekalu ya Pharaoh Hatshepsut katibu na mto Nile nchini Misri. Stefano Ricci anaadhimisha miaka yake 50 katika uanamitindo.
G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika onyesho hilo hilo, wanamitindo hawa walionyesha mitindo nadhifu
G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimkaribisha mwenzake wa ghana, Nana Akufo-Addo, katika Kasri la Élysée siku ya Alhamisi. Siku moja kabla , Bw Akufo - Ado alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari kutoka chuo kikuu cha Sorbonne katika mji mkuu Paris kwa kazi yake kama rais, ikiwa ni pamoja na kuendeleza maadili ya kidemokrasia nchini Ghana.
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muimbaji Muingereza mwenye asili ya Ivory Coast , Ivorian Doll, anajiandaa kupiga picha katika tukio la kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya la Off-White - nembo iliyoanzishwa na marehemu mbunifu Mmarekani, Virgil Abloh - kwa nembo ya viatu vya kifahari -Church.
G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kulikuwa na kupendeza wakati muongozaji Mmarekani mwenye asili ya Nigeria, Chinonye Chukwu (wa pili kushoto), akiwa amesimama pamoja na mchezaji filamu Mmarekani mjini California siku ya Jumamosi katika upigaji picha za filamu inayoitwa Till, ambayo inahusu mama yake Emmett Till - kijana wa kimarekani mwenye asili ya Afrika ambaye aliuliwa nchini Marekani katika mwaka 1955 baada ya mwanamke mzungu alimshutumu kwa kumsumbua.
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke huyu akihudhuria sherehe ya kuhamishwa kwa shaba za Benin katika Makumbusho ya Kitaifa ya sanaa za kiafrik Jumanne mjini Washington DC. Shaba hizo ambazo ni kazi za usanii za kihistoria- ziliibiwa na Waingereza kutoka Nigeria katika karne ya 19.
G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanaume huyu anakula wali na ndizi za kupikwa katika soko la mji mkuu wa Nigeria, Abuja
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni wakati wa mbwembwe katika tukio la mieleka katika mji mkuu wa Libya, Tripoli
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kulikuwa na michezo kidogo ya kuigiza na furaha zaidi Jumatatu huku wasichana hawa wakidensi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Uganda...
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jumanne mfanyakazi wa shirika la Msalaba mwekundu wakiwa wamesimama na zana za kujikinga kabla ya kumzika mtu katika mlipuko wa Ebola nchini Uganda ambao umesababisha vifo vya watu 19, kulingana na takwimu rasmi za serikali ya nchi hiyo ...
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku iliyofuatia wafanyakazi hawa wa kujitolea wanaonekanakutoa mafunzo ya jinsi ya kufanya mazishi ya wathiriwa wa Ebola burials for victims of Ebola.
G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kuna matukio ya rangi za kuvutia wakati mwanaume huyu alipokuwa akipeperusha tiara Jumapili tarehe 28, katika tamasha la kimataifa la upeperushaji wa tiaraambapo washiriki wanachangisha pesa kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na matatizo ya afya ya akili