Kwa picha: Wiki ya Afrika katika picha: 18-24 Machi 2022

Mkusanyiko wapicha bora za wiki kutoka Barani Afrika na maeneo mengine:

Short presentational grey line
Mwanamke anachanganya kinywaji katika eneo la Adjame, Abidjan, Ivory Coast - Jumapili Machi 20

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Katika mji wa Abidjan huko Ivory Coast , mwanamke anaandaakinywaji suku ya Jumapili.
The Real Boys wanafanya mazoezi kwenye studio ya densi mjini Abidjan, Ivory Coast- Jumamosi Machi 19 2022

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku moja kabla, Kundi la densi Real Boys nchi Ivory Coast, lilikuwa linafanya mazoezi mjini Abidjan.
Puppets backstage at the Carthage International Puppet Arts Festival in Tunis, Tunisia - Tuesday 22 March 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vigaragosi vinakaribia kuchukua nafasi kubwa katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, Jumanne…
Mtoto akimtazama kikaragosi wakati wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa la Vikaragosi la Carthage huko Tunis, Tunisia - Jumamosi 19 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mji huo umekuwa mwenyeji wa Tamasha la Sanaa la Kimataifa la Carthage ...
Mgeni akipiga picha na vinyago wenye miguu mirefu kwenye Tamasha la Sanaa la Vikaragosi la Carthage mjini Tunis, Tunisia - Jumamosi tarehe 19 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tukio hilo limerudi baada ya kuahirishwa kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la coronavirus.
Magari ya classic yakishiriki katika Tamasha la Kimataifa la Majumba ya Jangwa huko Tataouine, Tunisia - Jumatano 23 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tamasha la jangwani limekuwa likifanyika katika mji wa kusini mwa Tunisia wa Tataouine, huku Jumatano ikishuhudia msururu wa magari ya zamani.
Mwanamke aliyebeba nyasi kavu akionekana kwenye mitaa ya Harar, Ethiopia - Jumamosi 19 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku ya Jumamosi, mpiga picha alinanasa maisha katika mitaa ya mji wa Harar wenye shughuli nyingi nchini Ethiopia…
Mwanamume ameketi karibu na mikokoteni miwili kando ya barabara ya Harar, Ethiopia - Jumamosi 19 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hapa mtu anapumzika kando ya barabara siku hiyo hiyo.
Waendesha baiskeli wawili wanakimbia katika milima juu ya Somerset West, Cape Town, Afrika Kusini - Jumatatu 21 Machi 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waendesha baiskeli wanaoshiriki katika mbio za The Cape Epic hupita kwenye mashamba ya mizabibu takriban kilomita 60 kutoka mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini siku ya Jumatatu.
Watu wakichuma chai kwenye shamba karibu na Limuru, Kenya - Alhamisi 24 Machi 2022

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku ya Alhamisi, wavunaji chai wanaonekana kazini karibu na mji wa Limuru nchini Kenya.
Mtoto wa tembo akijifunika kwa udongo katika kituo cha watoto yatima cha wanyama hao karibu na mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mtoto wa tembo akijifunika kwa udongo katika kituo cha watoto yatima cha wanyama hao karibu na mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili.
People pictured on the banks of the River Loya, DR Congo - Saturday 19 March 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku moja kabla, watu wanapigwa picha kwenye kingo za Mto Loya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako waasi wanapigana.
Wafuasi wakiwa na mashabiki walio na bango la Rais wa CAR Faustin Archange Touadera kwenye mkutano huko Bangui, CAR - Ijumaa 18 Machi 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ya Ijumaa, wale wanaohudhuria mkutano wa kisiasa wa kumuunga mkono rais huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), wanapumzika.
Wajenga misuli wawili katika michuano ya Ashoor Classic huko Tripoli, Libya - Jumamosi 19 Machi 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku iliyofuata, wajenga misuli walionyesha medali zao kwenye michuano ya Ashoor Classic katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Mwanariadha wa Liberia Ebony Morrison akiruka juu ya kikwazo katika Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Ndani mjini Belgrade, Serbi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku hiyo ya Jumamosi pia, Ebony Morrison wa Liberia alifikia alama bora ya kibinafsi katika nusu fainali ya mbio za mita 60 kuruka viunzi katika mashindano ya Ridha ya Dunia inayochezwa ndani mjini Belgrade.
Ronald Ssegawa, 22, akionyesha vidole viwili alivyopoteza sehemu yake baada ya kuteswa huko Kampala, Uganda - Jumatatu 21 Machi 2022

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku ya Jumatatu, mfuasi wa upinzani nchini Uganda mwenye umri wa miaka 22 anaonyesha vidole viwili alivyopoteza - anadai baada ya kuteswa na maafisa wa usalama. Shirika la Human Rights Watch lilitoa ripoti siku iliyofuata na kulaani serikali kwa kutowajibisha maafisa kwa unyanyasaji huo.
A roadside vendor in Lagos recharges his clients' smartphone in Lagos, Nigeria - Tuesday 22 March 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Muuzaji kando ya barabara huko Lagos akichaji simu za wateja wake siku ya Jumanne. Kupotea kwa umeme ni jambo la kawaida katika jiji hilo la Nigeria.
People looking at the scene of a fire in Apongbon market under Eko Bridge in Lagos, Nigeria - Wednesday 23 March 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku iliyofuata, watu walionekana wakitazama tukio la moto uliozuka katika sehemu ya soko la Lagos chini ya moja ya madaraja makuu matatu ya jiji hilo...
Wazima moto kwenye Daraja la Eko, Lagos, Nigeria - Jumatano 23 Machi 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ilisababisha shughuli katika Daraja la Eko kukwama huku wazima moto wakijitahidi kudhibiti moto huo.
A smiling woman carrying aid supplies in Niamey, Niger - Wednesday 23 March 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, In Niger on the same day, a woman in the capital, Niamey, is pictured with food distributed by a Turkish group ahead of the Muslim holy month of Ramadan.
A chapati chef in Kigali, Rwanda - Wednesday 23 March 2022

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Na siku ya Jumatano pia, mpishi alipigwa picha akipika chapati katika mgahawa wake katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Picha zote zina haki miliki.