Ujerumani imethibitisha kuwa itaipatia Ukraine vifaru vya Leopard 2

Chanzo cha picha, Reuters
Baada ya wiki za kusitasita, Ujerumani imekubali kupeleka mizinga 2 ya Leopard nchini Ukraine, katika kile ambacho Kyiv inataraji kuwa itakuwa hatua ya kubadilisha hali kwenye uwanja wa vita.
Kansela Olaf Scholz alitangaza uamuzi wa kutuma vifaru 14 - na kuruhusu nchi nyingine kutuma vyao pia - katika mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumatano.
Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden pia unatarajiwa kutangaza mipango ya kutuma angalau vifaru 30 vya M1 Abrams.Msemaji wa Kremlin hapo awali alisema mizinga hiyo "itawaka kama mingine yote".
Dmitry Peskov alisema kulikuwa na makadirio ya kupita kiasi ya uwezo ambao vifaru vitaleta kwa jeshi la Ukraine, na kuita hatua hiyo "mpango uliofeli".
Lakini maafisa wa Ukraine wanasisitiza kuwa wanahitaji haraka silaha nzito zaidi, na wanasema vifaru vya kutosha vya vita vinaweza kusaidia vikosi vya Kyiv kunyakua eneo la nyuma kutoka kwa Warusi.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani alisema uamuzi wa kusambaza mizinga hiyo "unafuata njia yetu inayojulikana ya kuunga mkono Ukraine kwa uwezo wetu wote".
Ujerumani pia iliruhusu nchi zingine kutuma mizinga yao ya Leopard 2 kwa Ukraine - ambayo ilikuwa imewekewa vikwazo hadi sasa chini ya kanuni za usafirishaji.
Marekani na Ujerumani walikuwa wamepinga shinikizo la ndani na nje kutuma mizinga yao kwa Ukraine kwa muda.Washington ilitaja mafunzo ya kina na matengenezo yanayohitajika kwa Abrams ya teknolojia ya juu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wajerumani walivumilia mijadala ya kisiasa ya miezi kadhaa kuhusu wasiwasi kwamba kutuma mizinga kungeongeza mzozo huo na kuifanya Nato kuwa mshirika wa moja kwa moja kwenye vita na Urusi.
Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba tangazo kuhusu usafirishaji wa Abrams kwenda Ukraine linaweza kuja mara tu Jumatano, huku maafisa ambao hawakutajwa wakitajwa kusema angalau 30 zinaweza kutumwa.
Hata hivyo muda bado haujabainika, na inaweza kuchukua miezi mingi kwa magari ya kivita ya Marekani kufika uwanja wa vita.Maafisa wa Ujerumani waliripotiwa kusisitiza kuwa watakubali tu uhamisho wa Leopard 2 kwenda Ukraine ikiwa Marekani pia itatuma M1 Abrams."Ikiwa Wajerumani wataendelea kusema tutatuma au kuachilia Leopards kwa masharti ambayo Wamarekani wanatuma Abrams, tunapaswa kutuma Abrams," Seneta wa Kidemokrasia Chris Coons, mshirika wa Biden, aliiambia Politico Jumanne.
Uingereza tayari imesema itatuma vifaru vya Challenger Two kwa Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uchambuzi wa Jonathan Beale, Mwandishi wa masuala ya ulinzi
Ukraine bado haina uwezekano wa kupata vifaru 300 vya kisasa vya vita ambavyo inasema inahitaji kushinda vita hivyo.
Lakini ikiwa nusu dazeni ya mataifa ya Magharibi kila moja yatatoa vifaru 14, basi hiyo italeta jumla ya karibu vifaru mia - ambavyo vinaweza kuleta mabadiliko.
Vifaru vya Magharibi - ikiwa ni pamoja na Challenger 2 ya Uingereza, Leopard 2 ya Ujerumani na Abrams iliyotengenezwa Marekani - vyote vyanaonekana kuwa bora kuliko vile vya enzi ya Soviet, kama T-72 viinavyopatikana kila mahali.
Silaha hizo zitawapatia wanajeshi wa Ukraine ulinzi zaidi, kasi na usahihi.
Lakini vifaru hiyo vya kisasa vya Magharibi sio silaha ya ajabu au ya kubadilisha mkondo wa vita peke yake. Kwasababu itategemea kile kinachotolewa pamoja navyo.
Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na mabadiliko ya silaha nzito zinazotolewa na Magharibi - ikiwa ni pamoja na mamia ya magari ya kivita, mifumo ya vifaru na risasi.
Vikiunganishwa pamoja, ni aina ya vifaa vya kijeshi vinavyohitajika kupiga kuisukuma nyuma Urusi na kuteka maeneo ya Ukraine inyokalia.
Ikiwa wanajeshi wa Ukraine wanaweza kupewa mafunzo na silaha kutolewa kwa wakati, wanaweza kukabili mashambulizi yoyote ya majira ya joto. Hatahivyo kipengele muhimu kinachokosekana katika makabiliano hayo ni uwezo wa angani.
Ukraine imekuwa ikiomba magharibi kuwasilisha ndege za kibvita za kisasa tangu vita hivyo vianze , lakini kufikia sasa hakuna hata moja iliowasili.
Bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya Ujerumani. Kansela wa taifa hilo anatarajiwa kulihutubia bunge la Ujerumani Jumatano asubuhi.
Hata hivyo, Marie-Agnes Strack-Zimmermann wa chama cha kiliberali cha FDP, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya bunge la Ujerumani, aliunga mkono suala hilo
"Uamuzi ulikuwa mgumu, ulichukua muda mrefu sana, lakini mwishowe haukuweza kuepukika," alisema, akiongeza kwamba ungekuja kama afueni kwa "watu wa Ukraine waliopigwa na Urusi".

Mataifa washirika yalikuwa yamechanganyikiwa kwa kile wanachokiona kama kusita kwa Wajerumani kutuma magari hayo ya kivita katika siku za hivi majuzi.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius awali alisema kuwa Berlin iliyaruhusu mataifa mengine kuwafunza raia wa Ukraine kutumia vifaru vya Leopard 2, lakini hawakujitolea kutuma vyao.
Mkuu wa wafanyikazi wa rais wa Ukraine, Andriy Yermak, Jumanne alitoa wito kwa nchi za Magharibi kuipa Kyiv mamia ya vifaru kuunda "ngumi nzito" dhidi ya Urusi.
"Vifaru ni mojawapo ya vipengele vya Ukraine kurejea katika mipaka yake ya 1991," aliandika kwenye Telegram baada ya kuibuka kwa ripoti za Ujerumani kukubali kutuma mizinga.
Anatoly Antonov, balozi wa Urusi mjini Washington, aliandika kwenye Telegram: "Ikiwa Marekani itaamua kusambaza vifaru vyake , basi kuhalalisha hatua hiyo kwa hoja kuhusu 'silaha za kujihami' hakika haitakuwa ukweli.
"Hii itakuwa uchochezi mwingine wa wazi dhidi ya Urusi."












