Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini maegesho ya magari yamekuwa 'lulu' ya nishati ya umeme wa jua?
Na Chris Baraniuk, BBC
Eneo hili la maegesho ya magari lina zaidi ya magari na nafasi za wazi. Kuna safu kubwa za paneli za nishati ya jua zilizofungwa kwenye nguzo kubwa za chuma nyeusi, paneli zinazoleta kivuli kwa magari yaliyoegeshwa chini yake.
Nje ya ofisi za mmoja wa watengenezaji wakubwa wa magari Kusini mwa Uingereza, sasa kuna paneli zaidi ya 2,000 kwa ujumla zenye uwezo wa kuzalisha karibu megawati 1 (MW) za umeme wa jua.
Umeme huo unatosha kuendesha na kuwasha kwenye mamia ya nyumba.
"Wanaonekana kustaajabisha," asema Guy Chilvers, meneja wa maendeleo ya biashara wa SIG, kampuni inayosambaza nishati ya umeme wa jua.
Miundo hii hufanya eneo la maegesho ya magari kuvutia zaidi, anasisitiza.
Maegesho ya magari yanayotumia jua huwezesha uzalishaji wa umeme katika maeneo ya wazi yaliyo karibu kama vile hospitali, vituo vya ununuzi au ofisi.
Katika harakati za kuongeza uzalishaji wa nishati safi, Bunge la Seneti la Ufaransa liliidhinisha sheria hivi majuzi ambayo inalazimisha kwa maegesho yote yaliyopo na yale mapya ya magari yenye maeneo makubwa kufunikwa na paneli za jua.
Kwa muktadha huu, Uingereza kwa sasa ina mifumo ya jua yenye uwezo wa 15GW kwa jumla huku mahitaji yakiwa ni 40GW ifikapo 2030 ili kufikia malengo halisi, kulingana na Mamlaka ya Nishati ya jua ya Uingereza.
Kwa namna yoyote unavyotazama, kuna nafasi nyingi za wazi katika maegesho ya magari zinazoweza kuwekwa paneli za jua na watu wanaanza kutambua hili.
"Ni wazimu kabisa," anasema Bw Chilvers, akirejelea kisanduku chake. Bw Chilvers na wenzake husanifu na kujenga miundo ya chuma inayovuta miale ya jua ambayo huungwa na paneli.
Makampuni pinzani ambayo yalizungumza na BBC pia yalielezea mahitaji makubwa ya maegesho ya magari ya nishati ya jua.
Praxia Energy, iliyoko Uhispania, hutoa takriban 3MW ya mitambo ya jua ya maegesho ya magari nchini Uingereza kila mwaka na inasema inatarajia hii kukua mara kumi ifikapo 2028.
Msemaji wa kampuni ya Veolia anasema kampuni hiyo hivi majuzi iliweka mfumo wa miale ya jua wa uwezo wa 1.1MW katika maegesho ya magari ya Hospitali ya Eastbourne na kampuni hiyo imesajili ongezeko la mahitaji ya miundombinu ya jua nchini Uingereza hivi karibuni.
Maegesho makubwa zaidi ya magari yenye paa zenye paneli za umeme wa jua nchini Uingereza ni ile iliyo kwenye kiwanda cha magari cha Bentley huko Crewe, ambacho pneli hizo zina uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 2.7MW.
Bw Evans anasema kwa sasa anatafiti miradi minne mipya inayotarajiwa na wateja ambayo inaweza kuhitaji zaidi ya megawati 5.
Paneli za miale ya jua kwenye maegesho ya magari zinaweza pia kutumika kuchaji magari ya umeme (EV). Hii inafanya kazi vyema katika ofisi, ambapo magari ya wafanyakazi yanaegeshwa nje kwa saa nyingi. Vituo vya ununuzi, viwanja vya mpira, vituo vya burudani na sinema pia ni sehemu zinazofaa, kwa kuwa magari huwa yameegeshwa kwa saa mbili au zaidi ili kuruhusu chaji kuingia vya kutosha, anasema Bw Evans.
Moja ya changamoto kubwa inayokabili miradi mingi ya nishati mbadala kwa sasa ni ukosefu wa miundombinu ya kuunganisha nishati hiyo na gridi ya taifa, kwani nishati ya ziada inayozalishwa na paneli za jua, kwa mfano, lazima ishughulikiwe na gridi ya taifa. Uwekezaji wa mabilioni ya pauni umesitishwa kwa sababu ya suala hili, kulingana na utafiti wa BBC.
"Nimekuwa na sehemu ya kuegesha magari yenye paa la paneli ya jua inayozalisha umeme, maegesho mazuri tu ya magari, kwa ajili ya kiwanda lakini kimekataliwa kwa sababu hakiwezi kupata muunganisho wa gridi ya taifa," asema Bw Chilvers.
Msemaji wa mamlaka ya Nishati ya Jua Uingereza pia anaangazia tatizo hili, akisema kuwa maegesho ya magari yanayotumia miale ya jua kuwa jambo la kawaida yatasalia kuwa "matarajio ya mbali" hadi suala hilo litakapotatuliwa.
Wakati huo huo Mdhibiti wa sekta ya nishati Ofgem anatafuta njia za kuharakisha uunganishaji wa Gridi ya Taifa pia ina mpango wa kuboresha zaidi mchakato huo.