Kahawa au chai, ipi ina manufaa zaidi kwenye miili yetu?

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kuna vyakula vinavyoonekana kuwa pinzani: ketchup au mayonnaise? Burger au pizza? Na moja ya mijadala hii ya gastronomiki inaweza kutokea tangu mwanzo wa siku: ni bora kunywa asubuhi, kikombe cha kahawa au kikombe cha chai?

Katika nchi za Magharibi, kwa mfano, mara nyingi tunachagua kahawa. Hii inaonekana katika vyombo vya habari, ambapo ni kawaida kuona habari zilizochapishwa kuhusu manufaa kiafya.

Lakini vipi kuhusu "mpinzani" wake chai? Hatupaswi kusahau kwamba tunazungumzia juu ya kinywaji cha pili kinachotumiwa zaidi duniani kote, kwamba ni maarufu sana katika Asia na nchi kadhaa za Amerika ya Kusini.

Je, ni manufaa sawa kwa mwili? Je, ina athari sawa na kahawa?

Unaweza kusoma

Kahawa ina kafeini na chai, theine?

Na suala kuwa kahawa ina kafeini na chai, theine... Si kweli. Mara nyingi sisi hutumia neno hili kurejelea kafeini iliyopo katika chai, lakini kisayansi haipo hivyo.

Maharage ya mmea wa kahawa, ambayo huenda yanatoka kaskazini mwa Ethiopia, huchakatwa na kuchomwa kutengeneza kinywaji hicho.

Mbali na kafeini, ina viambata vingine, kama vile asidi ya chlorogenic, ambayo athari zake za antioxidant husaidia kulinda seli kutokana na uharibifu wa oksidi na inaweza kuwa na athari za kupinga uchochezi.

Kafeini inajulikana kwa athari zake za kichocheo kwenye mfumo mkuu wa neva, kusaidia kuboresha umakini. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kikombe cha kahawa kinaweza kuboresha utendaji wa utambuzi na kumbukumbu ya muda mfupi.

Hatahivyo, matumizi ya kupita kiasi yanaweza kusababisha athari mbaya, kama vile woga, kukosa usingizi au mapigo ya moyo kuongezeka, kwa hivyo inashauriwa kudhibiti matumizi yako.

Kwa upande mwingine, tuna chai, kinywaji kinachotoka China ambacho kimeshinda sayari nzima.

Kuna aina kadhaa, zinazojulikana zaidi ni chai ya kijani, chai nyeusi, chai nyeupe, na chai ya oolong, zote zinatokana na mmea wa Camellia sinensis. Kama tulivyosema hapo awali, ina kafeini, ingawa kiasi halisi kinategemea aina ya chai na njia yake ya kuitayarisha.

Tabia ya chai ya kijani

Chai ya kijani, haswa, inajulikana sana kwa kuwa na antioxidant, kutokana na polyphenols, kama vile catechins inayoimarisha afya, kuzuia na kutibu magonjwa.

Utafiti umeonesha kuwa hutoa athari ya kinga kwenye mfumo wa moyo na mishipa na inaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa sugu kama vile shinikizo la damu au kisukari cha aina ya 2.

Pia, tofauti na kahawa, chai ya kijani ina L-theanine, asidi ya amino ambayo inakuza utulivu bila kusababisha usingizi. Hii huleta hisia ya "tahadhari tulivu," ambayo inaweza kuwa nyepesi kuliko ile inayozalishwa na kahawa.

Hatimaye, baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya kawaida ya chai ya kijani yanaweza kupunguza hatari ya aina fulani za saratani, kama vile saratani ya matiti na kibofu, ingawa matokeo yake bado hayajakamilika.

Faida za chai nyeusi

Chai nyeusi, kwa upande mwingine, ina caffeine zaidi kuliko chai ya kijani. Imeoneshwa kusaidia kuboresha utendakazi wa utambuzi na kumbukumbu kama ilivyo kahawa, ingawa kwa kiasi kidogo sana.

Aidha, inajulikana kwa athari zake nzuri kwa afya ya moyo na mishipa, kwani matumizi ya mara kwa mara yanaweza kusaidia kupunguza viwango vya mafuta mabaya (LDL) na kuimarisha hali ya mishipa ya damu.

Athari hizi zinaweza kulinganishwa, na hata kuongezea, na faida zinazotolewa na kahawa katika suala la afya ya moyo na mishipa, kwa taratibu tofauti.

Kuwa mwangalifu, sio kila kitu wanachoita "chai" ni chai

Kuna mimea na maandalizi ambayo kitamaduni au maarufu kama "chai" ambayo sio ya jenasi ya Camellia: chai ya mwamba, aina maalum ya chai ya kijani kibichi au chai ya oolong inayopatikana kwenye maeneo ya milima yenye miamba, hasa nchini China. Chai ya rooibos, chai ya chamomile, chai ya punda, chai ya linden, chai ya mint, chai ya hibiscus, chai ya lemon verbena, chai ya rosemary, chai ya elderberry, nk.

Mimea hii haina kafeini au ina sifa za kusisimua kama vile chai halisi (C. sinensis), ingawa inathaminiwa kwa sifa mbalimbali za dawa au ladha yake.

Ipi bora.., Chai au kahawa?

Vikombe vyote viwili vya kahawa na chai ni chaguo nzuri. Kama tulivyosema, zote mbili zina kafeini kwa viwango tofauti, ambavyo huathiri jinsi zinavyoathiri kiwango cha nishati na mkusanyiko.

Ingawa kahawa hutoa kichocheo cha haraka na chenye nguvu zaidi, chai, hasa chai ya kijani, hutoa kichocheo laini na cha muda mrefu, na faida za kiafya kutokana na antioxidant na L-theanine.

Kwa hiyo, kwa wale ambao wanatafuta mbadala wa chini ya makali ya kahawa au wanataka kupata faida ya antioxidant inayopatikana, chai pia inaweza kuwa chaguo bora.