Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Je, Liverpool itafanikiwa kumsajili Guehi?

Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool ina nia ya kumsajili beki wa Crystal Palace wa Uingereza Marc Guehi, 24. (Daily Mail)

Liverpool bado haijapokea ombi lolote la kwa ajili ya mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, ambaye ni mchezaji wa hivi punde zaidi wa Ligi ya Premia kuhusishwa na mabingwa wa Serie A Napoli. (Liverpool Echo)

Chelsea inataka kuvuruga mpango wa klabu ya Newcastle wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro, 23. (Sun)

Winga wa Chelsea na England Noni Madueke, 23, anafuatiliwa na klabu kadhaa msimu huu wa kiangazi, ikiwa ni pamoja na Arsenal. (Telegraph - usajili unahitajika), nje

Nottingham Forest inakaribia kukamilisha dili la pauni milioni 30 la kuwasajili wachezaji wawili wa Botafogo ambao ni mshambuliaji Igor Jesus ,24, na beki Jair Cunha, 20. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mshambuliaji wa Sporting na timu ya taifa ya Uswidi Viktor Gyokeres, 27, anakaribia kujiunga na Arsenal badala ya Manchester United. (Sportsport)

Mshambulizi wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 22, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa Liverpool Ijumaa ya leo. (ESPN)

Brighton imepokea ofa ya pauni milioni 25.6 kutoka kwa Napoli kwa ajili ya kiungo wa Denmark Matt O'Riley, 24. (Sky Sports)

Klabu za Napoli na AC Milan zinavutiwa na mshambuliaji wa Juventus na Italia Federico Chiesa, 27. (Kiss Kiss Napoli - kwa Kiitaliano)

Sunderland iliyopanda daraja hivi karibuni inataka kumsajili beki wa zamani wa Southampton Duje Caleta-Car kutoka Lyon. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia mwenye umri wa miaka 28 alicheza mara 13 kwenye EPL msimu wa 2022-23. (Newcastle Chronicle)

Everton Imeanza kujadili mkataba na beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ana miaka miwili zaidi katika mkataba wake wa sasa lakini David Moyes anataka kuwa naye kwa muda mrefu. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Ghana Thomas Partey, 32, anatarajiwa kuondoka Arsenal tarehe 30 Juni baada ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya kukwama. (ESPN)

Winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Gittens, 20, ana nia ya kujiunga na klabu ya Chelsea msimu huu wa kiangazi na anasalia kuwa shabaha yao kuu katika nafasi hiyo(Standard)

Manchester United inasubiri kuona kama itafanikiwa kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ureno Joao Palhinha, 29, kwa mkopo baada ya kuamua kutotumia pesa nyingi kumnunua kiungo wa Atalanta Mbrazil Ederson, 25. (Givemesport)

Beki wa Liverpool na England Joe Gomez, 28, ananyatiwa na Crystal Palace, Leeds United na West Ham na klabu iko tayari kumruhusu kuondoka. (TBR Football)

Mshambulizi wa Slovenia Benjamin Sesko, 22, anataka kipengele cha kutolewa katika kandarasi yake kutumika ikiwa atajiunga na Arsenal kutoka RB Leipzig msimu huu. (The Transfers Podcast)

Napoli na Inter Milan zina nia ya kumsajili kiungo wa Poland mwenye umri wa miaka 17 Antoni Burkiewicz kutoka Rakow Czestochowa. (Teamtalk)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi