Rekodi ya gari lenye kasi zaidi duniani yavunjwa - Je, gari hilo lina nguvu kiasi gani?

Chanzo cha picha, Buggatti
Wiki hii katika ulimwengu wa magari: Bugatti imeweka rekodi mpya ya gari la wazi lenye kasi kubwa zaidi duniani, Cadillac imezindua gari lake jipya aina ya SUV (gari maridadi) linalotumia umeme. Gari hilo la kampuni ya Xiaomi limevunja rekodi ya Porsche, huku Donald Trump akimteua Mkurugenzi mtendaji wa kwanza wa kampuni ya magari ya Hyundai ambaye sio raia wa Korea.
Kampuni ya Bugatti ilivunja rekodi ya gari la wazi na la kasi zaidi duniani kwa kusajili kasi ya kilomita 91.453 kwa saa. Rekodi hii iliwekwa na Bugatti Mistral W16 barabarani nchini Ujerumani mbele ya wamiliki maarufu wa magari.
Mistral ni mfano wa mwisho wa Bugatti ambayo ina injini yenye silinda kumi na sita. Bugatti ilizindua gari hili mnamo 2022 na ni magari 99 tu ya aina yake yaliyotengenezwa.
Injini ya Mistral ina nguvu ya horse power 1600. Bugatti hapo awali ilikuwa imetumia injini hii katika mfano wa "Chiron Super Sport" na kurekodi kasi ya 482.8 km / kwa saa mnamo 2019.
End of Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, BUGATTI
Ingawa muundo wake kwa kawaida unafanana na ule wa Chiron Supercar Mistral inaonekana tofauti kabisa na ilitengenezwa kwa dhana za Bugatti na mifano ya miundo ya jadi.
Wakati huo huo wakati Mistral ilizinduliwa, vyombo vya habari vilitangaza bei yake ya msingi kama euro milioni tano (karibu dola milioni tano na elfu 300), lakini Bugatti inasema thamani ya gari iliyovunja rekodi wiki iliyopita ni euro milioni 14 (karibu dola milioni 14 na milioni 700).
Mmiliki wa mistral hii, ambayo imetajwa " kushikilia rekodi ya ulimwengu", ni mfanyabiashara wa Uingereza mwenye asili ya India aitwaye Reuben Singh. Bwana Singh ana mifano mingine ya Bugatti katika kampuni yake ya magari ambayo pia yamevunja rekodi ya kasi.

Chanzo cha picha, BUGATTI
Rekodi hiyo iliwekwa na Andy Wallace, dereva rasmi wa Bugatti, ambaye ameshinda shindano la magari la saa 24 . Baada ya kuweka rekodi ya mzunguko mwingine zaidi , aliondoka na mmiliki gari hilo kwenye barabara ya mashindano, na Bugatti inasema Singh alikuwa "dereva mweye kasi zaidi duniani" bada ya kuzunguka mzunguko mmoja mbele ya magari mengine.
Rekodi ya awali ya gari la wazi zaidi duniani ilikuwa 427.4 km / kwa saa, ambayo iliwekwa na Hennessy Venom GT Spyder mwaka 2016.

Chanzo cha picha, Cadillac
Gari la Cadillac lenye uwezo wa kuwabeba watu saba
Cadillac itaongeza SUV (gari maridadi) jipya la umeme linaloitwa "Vistiq" kwenye bidhaa zake kuanzia mwaka ujao. Vistic ni muundo wa tano wa umeme wa gari la Cadillac.
Vipengele vya gari hili ni sawa na mfano wa Lyric na ina safu tatu za viti kama Escalade.
Vistic ina motors mbili za umeme ambazo hutoa jumla ya nguvu za horse power 615. Gari huharakisha kutoka sifuri hadi maili 60 kwa saa kwa sekunde 3.7 .

Chanzo cha picha, CADILLAC
Ina sauti 23 tofauti mbali na vifaa vya mfumo ambao unafuta kelele za kusumbua.
Vistic pia ina vifaa vya mfumo wa "Super Cruise" wa GM, ambao unamruhusu dereva kuondoa mikono yake kwenye usukani kwenye njia fulani.
Katika hali hii, dereva lazima awe makini na wakati gari linatambua kuwa anaondoa macho yake barabarani, humuonya.

Chanzo cha picha, Cadillac

Chanzo cha picha, Cadillac
Cadillac inasema kuwa tofauti na magari mengi yenye viti vitatu, imetoa huduma nyingi kwa abiria watatu. Wana mahali pa kuweka kikombe, wanaweza kuchaji simu zao na kubadilisha hali ya hewa ndani ya gari kwa kuongeza joto au baridi. Paa la juu ya safu ya tatu limetengenezwa kwa glasi.
Bei ya Vistic ni $ 78,790. Gari hili linashindana na gari la muundo wa Tesla - Tesla Model X na Volvo EX90, zote mbili zina bei ambayo ni ghali zaidi kuliko Cadillac Vistic na huduma sawa kwa watumiaji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzuri wa Xiaomi katika jumba la michezo la Nurburgring
Li Jun, mkurugenzi wa Xiaomi jumba la maonyesho ya magari la Guangzhou Auto Show, alisema muundo wa magari yake ya sport ya SU7 Ultra ulifikia kasi ya juu ya 71.359 km / kwa saa katika jaribio la ubora wake lililofanyika nchini China.
Xiaomi pia ilionyesha sampuli ya majaribio ya SU7 Ultra kwenye maonyesho ya hivi karibuni ya Guangzhou, ambapo ilivunja rekodi ya mzunguko wa Porsche Taycan katika jumba maarufu la michezo la Nurburgring nchini Ujerumani.
Nurburgring ni moja ya maeneo yanapofanyika mashindano magumu zaidi ya mbio za magari ulimwenguni. Watengenezaji wa magari hutumia viwanja vya jumba hili kujaribu uwezo wa magari yao, na rekodi nzuri za magari hayo hubeba heshima nyingi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni ya Xiaomi, ambayo ni maarufu kwa simu zake za mkononi na vifaa vya nyumbani, ilizindua gari lake la kwanza linaloitwa SU7 miezi minane iliyopita. Muundo wa gari hilo aina ya sport la SU7 Ultra utazinduliwa mwaka ujao na Xiaomi inataka kushindana na Porsche. Ndio sababu kuvunja rekodi ya Porsche huko Nurburgring ni muhimu sana kwa Xiaomi.
Rekodi hiyo ilishikiliwa na David Pittard, ambaye alishinda mbio za saa 24 za Nurburgring waka 2023. Bwana Pittard aliweza kuendesha SU7 Ultra kwa dakika sita, sekunde 46 na sekunde 874. Rekodi ya Porsche Taycan GT Turbo ni dakika saba na sekunde saba.
Xiaomi SU7 Ultra ina injni tatu za umeme ambazo hutoa jumla ya nguvu za horse power 1,548. Gari hilo lina kasi ya kuanzia 0 hadi 100 km / kwa saa kwa sekunde 1.97, na Xiaomi inasema kuwa SU7 Ultra ina uwezo wa kasi ya kuanzia sifuri hadi 200 km / kwa saa moja na chini ya sekunde sita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Muundo wa kawaida wa SU7 umekuwa ukiuza vizuri kwa miezi minane iliyopita, na Xiaomi inasema imeuza zaidi ya magari 100,000. Bei ya rahisi ni Yuan 215,900 (chini ya $ 30,000), na magari yake ya muundo wa gharama kubwa zaidi na huduma mpya na teknolojia yanauzwa kwa yuan 299,900 ($ 41,500).
Hivi karibuni, maoni ya Mkurugenzi Mtendaji wa Ford Jim Farley kuhusu SU7 yamegonga vichwa vya habari. Bwana Farley alisema katika mahojiano kwamba amekuwa akiendesha gari aina ya SU7 kwa takriban miezi sita ili kuwachunguza washindani wake wa kiwanda. Alikataa kuzungumzia kuhusu gari hilo, lakini alisema hakutaka kulirejesha.

Chanzo cha picha, Reuters
Hyundai ilimteua Jose Muñoz, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo. Bwana Muñoz ni mtendaji wa kwanza asiye raia wa korea kuteuliwa katika wadhifa huu, na inasemekana kuwa lengo la uteuzi wake ni kuiandaa Hyundai kwa urais wa Donald Trump.
Bwana Muñoz ni raia wa Uhispania na Marekani. Kabla ya kujiunga na Hyundai, alikuwa mkurugenzi wa Nissan katika Amerika ya Kaskazini.
Mnamo 2019, alikua mkurugenzi wa Hyundai na wa kwanza nchini Marekani , na kuanzia mwaka 2022 alichukua jukumu la kitengo cha kimataifa cha Hyundai.
Sera za Donald Trump zitakuwa na athari kubwa kwa Hyundai. Trump anapanga kupunguza ruzuku ya serikali ya dola 7,500 kwa magari ya umeme na kuongeza ushuru wa kuagiza magari ya kigeni.

Chanzo cha picha, Reuters
Utekelezaji wa sera hizi utaiweka kampuni ya Hyundai katika hali ngumu, na hivyobasi inatarajia kupunguza uwezekano wa mgogoro kwa kukabidhi usimamizi wa kiwanda kwa Bw. Muñoz. Wakati huo huo, Hyundai ilimteua Sung Kim, mwanadiplomasia wa Korea na Marekani, kuwa rais wa kampuni hiyo.
Hyundai na Kia ni wauzaji wa pili kwa ukubwa wa magari ya umeme nchini Marekani baada ya Tesla. Kia hutengeneza baadhi ya bidhaa zake nchini Mexico. Trump ametishia kuweka ushuru wa asilimia 200 kwa magari yanayoingizwa kutoka Mexico. Kutumia ushuru huu kutakuwa na athari mbaya kwa biashara ya Kia huko Amerika.
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla












