Fahamu toleo jipya la gari la kifahari zaidi duniani

Chanzo cha picha, MERCEDES-BENZ
Wiki hii katika ulimwengu wa magari kuumetoka taarifa kuhusu toleo jipya la magari (Suv) ya meme ya Benz ya kifahari zaidi duniani, toleo jipya la magari ya ya BMW, toleo jipya la gari la umeme la Audi na mpango wa renault wa kupunguza wasiwasi wa wanunuzi wa magari yao ya umeme.
Injini pacha za umeme
Wakati wa uzinduzi wa aina zao za magari ya kifahari ya umeme, Mercedes-benz na BMW walitoa picha na maelezo ya vifaa vya magari haya.
EQS ni gari la umeme la kifahari zaidi yanayotolewa na Benz. Gari hilo litatengenezwa rasmi nchini Marekani na litauzwa baadaye mwaka huu.

Chanzo cha picha, MERCEDES-BENZ
Magari haya ya EQS yametumia mfano wa awali wa Benzi aina ya Sedan. Benz itatengeza EQs zenye muundo wa mashine moja ama mbili za kuendeshea za umeme, inayoweza kuzalisha nguvu ya umeme ya mpaka 750HP
Iko tofauti ya Benz za awali na Hii mpya, ambapo katika hili jipya, dashbodi yake ina urefu wa inchi 56. Abiria anayekaa kando ya dereva mbele anauwezo wa kuangalia TV wakati wote gari ikiendelea na safari, tofauti na magari mengi, wanaokaa siti za nyuma ndio wanaoweza kutazama TV.
Wakati huo huo, kuna kamera zinazuatilia mwenendo wa dereva, na ikiwa kuna sehemu yoyote ambayo dereva hapaswi kutazamwa basi itajifunga ama kujizima, ili kutoharibu umakini wa dereva anapoendesha.

Chanzo cha picha, BMW
Kuna uwezekano wa toleo hili la EQS, BMW ikawa gari la kifahari zaidi za aina yake kuwahi kutolewa dunaini. Mbali na kuwepo kwa mifumo ya petroli, BMW 7 pia itatolewa na mifumo ya umeme. Kiwanda chake cha Ujerumani wiki iliyopita kilitoa picha za toleo jipya iliyopewa jina la i7.
Toleo hilo limerembwa zaidi hasa kwenye kioo chake cha mbeke, nyuma na hata vya pembeni.

Chanzo cha picha, BMW
BMW pia ilitoa picha ya ndani ya gari hilo ikionyesha inchi 31 za paa ambalo linaloweza kufunguka nyuma. Katika picha hiyo, unaweza kuona kwamba dashibodi ya gari hilo inafanana kabisa na ile ya BMW ya umeme SUV inayoitwa iX, ambayo imetoka hivi karibuni sokoni.
BMW haijatoa maelezo ya kiufundi ya gari hiyo yenyewe inasema tu i7 ina nguvu zaidi ya farasi 600.
BMW inasema uzalishaji wa majaribio ya toleo jipya la Series 7 umeanza na gari la kwanza litatolewa mwishoni mwa mwaka huu.
Toleo jipya la Audi

Chanzo cha picha, AUDI
Audi na enyewe imezindua gari lake la umeme ikifanana kiasi na mfano wa gari la aina hiyo lililotolewa miaka mwiwli iliyopita. Audi imetumia dhana ya magari ya Porsche kutengeneza toleo hilo lilillopewa jina la A6 Avant.
Audi inasema gari hilo linaweza kukaa na chaji inayoweza kwenda hadi kilomita 700, na chaji yake ni ya kasi, ambayo inatosha kufanya kazi kwenda hata umbali wa kilomita 300 kwa dakika kumi tu.
Toleo hilo linafanana na Sedan A6 ambayo imepangwa kuingia sokono mwaka 2023. Urefu wa gari hiyo ni mita 5 na umbali kati ya magurumu mawili umeongezeka ili kupata nafasi ya kuweka betri. Huku abiria nyuma wakiwa na nafasi zaidi ya kujimwaga.

Chanzo cha picha, AUDI
Gari hili lina taa zenye muundo na aina mbalimbali. Dereva anaweza kubadilisha kwa namna anavyotaka yenewe. Pia kwa mbele kuna Projekta inayomuonyesha dereva kila pembe zikiwemo alama za barabarani.














