Matumizi ya magari ya umeme Rwanda yaanza kwa kusuasua

g

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Watengenezaji wa magari ya umeme wamekuwa wakivutiwa kwenda Rwanda

Ikifahamika kama ardhi ya milima elfu moja, huenda Rwanda isiwe sehemu bora kuzindua matumizi ya magari ya umeme.

 Ardhi ngumu ya vijijini ni mbaya kwa gari lolote, lakini hususan ni kwa miundo ya magari yenye betri nzito.

Lakini rais wa Rwanda Paul Kagame anataka kubadilisha uchumi wa taifa hilo dogo, lisilopakana na bahari.

Sehemu muhimu ya mpango huo ni kupunguza utoaji wa hewa chafu na kupunguza kiwango cha uagizaji wa taifa wa mafuta, ambayo yanaigharimu nchi hiyo 40% ya matumizi ya fedha za kigeni.

Kwahiyo, serikali imeanzisha mpango wa motisha mbali mbali kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya magari ya umeme.

 Magari ya umeme, vipuli vyake, betri na vifaa vya kuchaji vimeondolewa kodi ya ongezeko la thamani VAT, na ushuru wa uangizaji pia umeondolewa.

 Wakati huo huo, magari ya umeme yanaweza kuchajiwa kwa umeme ulioondolewa ushuru kwa kiasi kikubwa. Serikali pia hutoa eneo la bure kwa ajili ya kuegesha magari ya umeme.

g

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Volkswagen ilizindua magari yake ya umeme ya Golf - e-Golf nchini Rwanda

Kwa mara ya kwanza uzinduzi wa matumizi ya gari za umeme ulipendekezwa mwaka 2019, lakini ukakwamishwa na janga la Covid , utoaji wa motisha ulianza kutekelezwa mwezi Aprili 2021.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Kampuni ya magari ya Volkswagen ya Ujerumani ilikuwa ya kwanza kunufaika na mpango wa serikali. Ilizindua muundo wake wa magari ya umeme e-Golf nchini Rwanda mwaka 2019. Mradi wa majaribio ulianza kwa magari manne na vituo viwili vya kuchaji mjini Kigali.

 Mpango wa awali wa VW ulikuwa ni kupanua huduma hiyo hadi kufikia magari 50 na vituo 15 vya kuchajia umeme.

 Hatahivyo, miaka mitatu baadaye ni magari 20 pekee ambayo yanaendeshwa barabarani kwenye safari zake za kawaida. Na badala yake huwasafirishwa wasafiri kutoka kwenye hoteli za kifahari, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali na Kigali Convention Centre.

 "Ukosefu wa usawa wa miundo mbinu ya barabara na urefu wa vizuizi vya kasi ya mabari barabarani vimegeuka kuwa changamoto kwa magari ya e-Golf, ambayo kwa akwaida huwa ni mafupi ," anasema Allan Kweli, mkuu wa Volkswagen Mobility Solutions Rwanda.

 Kuna hofu moja kubwa kuhusu kuharibika kwa sehemu ya chini ya gari, iliko betri.

 Licha ya hayo, VW bado ina matumaini kuhusu Rwanda. Inapanga kuagiza magari yake ya ID.4 ya umeme, ambayo yako juu zaidi ya ardhi.

"Uzuri wa Rwanda ni kwamba serikali imebuni eneo la majaribio ambapo unaweza kuthibitisha kazi yako katika eneo la Afrika," Anasema Bw Kweli.

Getty

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, EvPlugin ya Rwanda inatarajia kujenga maeneo 200 ya umma ya kuchaji betri za magari ya umeme kote nchini

Tatizo moja kubwa linalokabili watengenezaji wa magari ni ukosefu wa huduma ya kuchaji nje ya mji wa Kigali.

 Katika nchi inayoendelea kama Rwanda, ni vigumu kuhalalisha uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu ya kuchaji kote nchini.

 Hatahivyo, kwa ushirikiano wa serikali na makampuni ya nishati kampuni ya Rwanda ya EvPlugin inapanga kujenga vituo 200 vya kuchajia magari kote nchini kwatika kipindi cha miaka miwili ijayo.

 Katika ya vituo hivyo, 35 vitafaa kwa ajili ya kuchaji magari na vingine vitakuwa ni vya kuchaji pikipiki.

G

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Pikipiki za umeme zimekuwa na mafanikio nchini Rwanda

Kampuni ya Japan ya Mitsubishi inaepuka tatizo kwa kuanzisha utengenezaji wa magari ya petroli nchini Rwanda.

 Ina magari 135 ya aina ya Outlander katika barabara za mji wa Kigali - 90 kati yake yamekodishwa , huku mengine yaliendeshwa kwa huduma ghali ya kukodishwa.

 Wakosoaji wanahoji athari chanya za mazingira za magari ya Outlander , kwani katika mji wenye milima wa Kigali , gari la aina hii linaweza kumudu kuendeshwa kwa kilomita zipatazo 50 hadi 70 (maili 30 hadi 44 ) kwa kutumia nguvu ya betri pekee.

Getty

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Paul Mugambwa anasema magari haya ni nafuu kwa zaidi ya dola 100 kwa mwezi akilinganisha na gharama ya mafuta

Hilo sio tatizo kwa Paul Frobisher Mugambwa, anayefanya kazi katika kampuni ya kimataifa mjini Kigali. Gari lake la kukodi la Outlander hutumia zaidi betri iliyochajiwa, kwa ajili ya safari yake ya kilomita 7 kati ya nyumbani kwake na ofisini

Anasema mafuta ya petroli yalikuwa yanamgarimu $150 (£128) kwa mwezi, kuchaji gari lake la Outlander humgarimu $40 kwa mwezi.

Kawaida, angependa kutumia gari la umeme, lakini ana wasiwasi kuhusu ukosefu wa mafundi wa magari ya umeme nchini Rwanda ambao wangeweza kuitengeneza gari ya aina hiyo.

"Kama ukiagiza gari la umeme la Kichina -SUV, ni nani atakayelitengeneza litakapoharibika" Bw Mugambwa aliuliza.

Huenda pingamizi kubwa la kutengeneza soko la magari ya umeme ni gharama.

Getty

Chanzo cha picha, JEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Katika maeneo ya vijijini ya nchi inayoendelea kama Rwanda watu wengi hawana uwezo wa kununua gari

Ingawa Rwanda imepata mafanikio kwa kipindi cha zaidi ya muongo uliopita takriban nusu ya watu wake wamefikia kiwango cha Umoja wa Mataifa cha masikini - wakiishi kwa chini ya $2.15 kwa siku.

 Huku umasikini ukiwafanya wengi washindwe kumiliki gari la umeme , inawezekana kwa wengi wao kupanda pikipiki ya umeme.

 Kampuni ya Ampersand tayari imeweza kuuza zaidi ya pikipiki 700 za umeme- e-motorbikes nchini Rwanda, ambako usafiri wa pikipiki ni muhimu sana.

 Pikipiki hizi zinazoitwa e-motos, zenye mfumo wa kubadilisha betri, ni maarufu sana, kwasababu ni nafuu na hufanya kazi zaidi ya pikipiki za kawaida.

Getty

Chanzo cha picha, VEROEN VAN LOON

Maelezo ya picha, Licha ya changamoto , wengi wanaamini kuwa Rwanda inapaswa kuendelea na mipango yake ya matumizi ya magari ya umeme.

Michelle DeFreese, ni afisa wa ngazi ya juu katika taasisi ya mazingira ya Global Green Growth Institute, inayoisaidia serikali ya Rwanda kutoa mafunzo na ushauri kuhusu mpango wa matumizi ya mabasi ya umma ya umeme.

 Anaamini kwamba Rwanda , ambayo tayari imepunguza 53% ya hewa chafu kutokana na kutumia vyanzo vya nishati safi , iko katika nafasi nzuri kuelekea mabadiliko.

 "Kuwekeza pakubwa katika nishati safi na kuhamia katika matumizi ya magari ya umeme kwa pamoja ni jambo kubwa inapokuja katika suala la kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa mazingira," anasema.