Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Putin katika harakati ya kuunda silaha inayoweza kusafiri umbali wa kilomita 3.2 kwa sekunde
Likiwa ncha yake imeelekezwa kwenye jua katika uwanja wa gwaride huko Beijing, makombora ya Jeshi la Jamhuri ya China yalisogea polepole kupita umati wa watu waliokuwa kwenye kundi moja la lori kubwa lililofichwa
Yakiwa na Sindano yenye ncha kali mbele yake, yenye urefu wa mita 11 na uzani wa tani 15, kila moja lilikuwa na herufi na nambari: "DF-17".
China ilikuwa imezindua kwa ulimwengu safu yake ya makombora ya Dongfeng hypersonic.
Hiyo ilikuwa tarehe 1 Oktoba 2019 kwenye gwaride la Siku ya Kitaifa. Marekani ilikuwa tayari inajua kwamba silaha hizi zilikuwa zikiundwa, lakini tangu wakati huo China imeendelea mbele na kuziboresha.
Shukrani kwa kasi na ujanja wao - kombora hilo lenye uwezo wa kusafiri kwa zaidi ya mara tano ya kasi ya sauti - ni silaha ya kutisha, kiasi kwamba ingeweza kubadilisha jinsi vita vinavyopiganwa.
Ndio maana shindano la kimataifa la kuziendeleza linazidi kupamba moto.
"Hii ni sehemu moja tu ya taswira pana ya shindano ibuka la kisiasa la kijiografia ambalo tunaona kati ya watendaji wa serikali," anasema William Freer, mshirika wa usalama wa taifa katika Baraza la Utafiti wa Jiostratejia.
"[Ni moja] ambayo hatujaona tangu Vita Baridi."
Urusi, China, Marekani: mashindano ya kimataifa
Sherehe ya Beijing iliibua uvumi juu ya uwezekano wa tishio linalosababishwa na maendeleo ya China katika teknolojia ya hypersonic. Leo inaongoza kijeshi katika uwanja wa makombora ya hypersonic, ikifuatiwa na Urusi.
Marekani, wakati huo huo, inacheza-cheza, wakati Uingereza haina.
Bw Freer wa Baraza la Utafiti wa Jiostratejia, ambalo lilipokea baadhi ya ufadhili wake kutoka kwa makampuni ya sekta ya ulinzi, Wizara ya Ulinzi na nyinginezo, anasema kuwa sababu ya China na Urusi kuwa mbele ni rahisi kiasi.
"Waliamua kuwekeza pesa nyingi katika programu hizi miaka michache iliyopita."
Wakati huo huo, kwa sehemu kubwa ya miongo miwili ya kwanza ya karne hii, mataifa mengi ya Magharibi yalilenga kupigana na ugaidi unaochochewa na wanajihadi nyumbani, na vita vya kukabiliana na waasi nje ya nchi.
Wakati huo, matarajio ya kupigana na mzozo kati ya rika dhidi ya mpinzani wa kisasa, wa hali ya juu yalionekana kuwa mbali.
"Matokeo ya jumla ni kwamba tulishindwa kutambua kuimarika kwa China kama nguvu ya kijeshi," alikiri Sir Alex Younger, mara tu baada ya kustaafu kama mkuu wa Huduma ya Ujasusi ya Siri ya Uingereza mnamo 2020.
Mataifa mengine pia yanasonga mbele: Israeli ina kombora la hypersonic, Arrow 3, lilioundwa kwa lengo la udunguaji makombora yanayorushwa.
Iran imedai kuwa na silaha za hypersonic, na ilisema ilirusha kombora la hypersonic huko Israeli wakati wa vita vyao vifupi lakini vya vurugu vya siku 12 mnamo Juni.
(Silaha hiyo ilisafiri kwa kasi ya juu sana lakini haikuonekan kuwa na uwezo wa wa kutosha kufikia silaha za hypersonic).
Korea Kaskazini, wakati huo huo, imekuwa ikiundatoloe lake la silaha hiyo tangu 2021 na inadai kuwa na silaha inayofaa, inayofanya kazi (pichani).
Marekani na Uingereza sasa zinawekeza katika teknolojia ya makombora ya hypersonic, kama vile mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Japan.
Marekani inaonekana kuwa inaimarisha ulinzi wake, na imezindua silaha yake ya "Dark Eagle" ya hypersonic.
Kulingana na Idara ya Ulinzi ya Marekani, Tai wa Giza "huleta akilini nguvu na azimio la nchi yetu na Jeshi lake kwani inawakilisha roho na mauaji ya juhudi za Jeshi na Jeshi la Wanamaji".
Lakini Uchina na Urusi kwa sasa ziko mbele sana - na kulingana na wataalam wengine, huu ni wasiwasi unaoongezeka.
Hypersonic zenye kasi na zisizo na uhakika
Hypersonic ina maana ya kitu kinachosafiri kwa kasi ya Mach 5 au zaidi. (Hiyo ni mara tano ya kasi ya sauti au 3,858 mph.) Hii inawaweka katika ligi tofauti na kitu ambacho ni supersonic tu, kumaanisha kusafiri kwa kasi ya juu ya sauti (767 mph).
Na kasi yao ni sehemu ya sababu ambayo makombora ya hypersonic yanachukuliwa kuwa tishio kama hilo.
Kombora lenye kasi zaidi la aina ya Hyspersonic ni lile la Urusi la - Avangard - linalodaiwa kuwa na uwezo wa kufikia kasi ya Mach 27 (takriban 20,700mph) - ingawa takwimu ya karibu Mach 12 (9,200mph) inatajwa mara nyingi zaidi, ambayo ni sawa na maili mbili kwa sekunde.
Kwa upande wa nguvu za uharibifu, hata hivyo, makombora ya hypersonic sio tofauti sana na makombora ya juu au ya chini ya baharini, kulingana na Bw Freer.
"Ni vigumu kuzigundua, kuzifuatilia na kuzidungua hiyo ndiotofauti."
Kwanini silaha za hypsersonic ni tishio
Kuna aina mbili za kombora la hypersonic: makombora ya kuongeza kasi yanategemea roketi (kama yale ya DF-17 nchini Uchina) ili kuyasukuma kuelekea na wakati mwingine juu ya angahewa ya dunia, kutoka ambapo yanakuja yakiruka chini kwa kasi hizi za ajabu.
Tofauti na makombora ya balistiki ambayo husafiri katika njia ya kawaida - mkondo kwa mfano - mengine yanaweza kuruka kwa njia isiotabirika, yakiongozwa katika safari ya mwisho kuelekea lengo lao.
Kisha kuna makombora ya cruise ya hypersonic, husafiri chini ya rada ili kuzuia kutambuliwa.
Hurushwa kwa pamoja kwa kutumia kiboreshaji cha roketi, kisha pindi zinapofikia kasi , huwasha mfumo unaojulikana kama "injini ya scramjet" ambayo inachukua hewa inaporuka, na kuipeleka kwenye lengo lake.
Hizi ni "silaha zenye matumizi mawili", ikimaanisha kwamba vichwa vyao vya vita vinaweza kuwa vya nyuklia au vilipuzi vya kawaida. Lakini kuna zaidi kwa silaha hizi kuliko kasi pekee.
Tahadhari kuhusu tishio la Urusi
Ukweli unasalia kuwa Urusi na Uchina ziko kifua mbele linapokuja suala la kutengeneza silaha hizi. "Nadhani programu za hypersonic za Kichina ... zinavutia na zinahusu," anasema Bw Freer.
Lakini anaongeza: "Inapokuja kwa Warusi, labda tunapaswa kuwa waangalifu zaidi juu ya kile wanachodai."
Mnamo Novemba 2024, Urusi ilizindua kombora la majaribio la masafa ya kati kwenye tovuti ya viwanda huko Dnipro, Ukraine, ikitumia kama uwanja wa majaribio wa moja kwa moja.
Kombora hilo, ambalo Ukraine ilisema lilisafiri kwa mwendo wa kasi wa Mach 11 (au 8,439mph), lilipewa jina 'Oreshnik', Kirusi kwa mti wa hazel.
Rais Vladimir Putin alisema kuwa silaha hiyo ilisafiri kwa kasi ya Mach 10.
Kichwa chake cha kivita kinaripotiwa kugawanyika kimakusudi wakati wa mteremko wake wa mwisho hadi katika makombora kadhaa, mbinu iliyoanzia Vita Baridi.
Mtu aliyeisikia ikitua aliniambia kuwa haikuwa kubwa haswa lakini kulikuwa na athari kadhaa: vichwa sita vilidondoshwa katika malengo tofauti lakini kwa vile havikuwa na madhara, uharibifu haukuwa mkubwa zaidi kuliko ule uliosababishwa na mashambulizi ya usiku ya Urusi katika miji ya Ukraine.
Kwa Ulaya, tishio la siri kwa nchi za Nato linatokana na makombora ya Urusi, ambayo baadhi yake yamewekwa kwenye pwani ya Baltic katika eneo la Kaliningrad la Urusi.
Je, ingekuwaje iwapo Putin angeamuru shambulizi la Oreshnik katika mji wa Kyiv ?
Kiongozi huyo wa Urusi alidai kuwa silaha hii inazalishwa kwa wingi na kwamba ilikuwa na uwezo, kugeuza shabaha kuwa "vumbi".
Urusi pia ina makombora mengine ambayo husafiri kwa kasi ya hypersonic.
Putin alitengeneza makombora mengi ya jeshi lake la wanahewa aina ya Kinzhal (Dagger), akidai yalisafiri kwa kasi ambayo haiwezekani kuyazuia.
Tangu wakati huo, ameyatumia kwa wingi huko Ukraine - lakini ikawa kwamba Kinzhal inaweza kuwa sio kombora la hypersonic, baada ya makombora kama hayo kuzuiliwa na mifumo ya anga ..