Je, madai ya uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita vya Ukraine ni ya kweli?

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa "muungano wa pamoja" unaundwa kati ya Urusi na tawala kama vile Korea Kaskazini. Amedai kuwa Pyongyang ilituma silaha na wanajeshi nchini Urusi ili kuimarisha jeshi la nchi hiyo.
Rais wa Ukraine alitoa matamshi hayo wakati wa ziara yake ya hivi karibuni katika miji mikuu ya Ulaya, kwa lengo la kuomba msaada zaidi wa kijeshi.
Kumekuwa na ripoti nyingi kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini ndani ya Ukraine kusaidia jeshi la Urusi. Wiki iliyopita, shirika la habari la Ukraine Interfax na gazeti la Kyiv Post, wakinukuu vyanzo vya habari katika mashirika ya ujasusi ya Ukraine, viliripoti kuwa mnamo tarehe 3 Oktoba , maafisa sita wa jeshi la Korea Kaskazini waliuawa katika shambulio la kombora la Ukraine kwenye uwanja wa mafunzo ya kijeshi katika eneo linalokaliwa na Urusi la Donbas. Watu wengine watatu walijeruhiwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kundi la maafisa wa Korea Kaskazini walikuwa huko "kubadilishana uzoefu" na wenzao wa Urusi.
Mashirika ya ujasusi ya Ukraine yaliripoti mwaka jana kwamba kundi dogo la vikosi vya kijeshi vya Korea Kaskazini, hasa vitengo vya uhandisi, viliingia katika maeneo yaliyokaliwa na Ukraine. Urusi haikujibu madai hayo.
Mnamo tarehe 8 Oktoba , waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Kim Yong-hyun alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Korea Kaskazini imetuma wanajeshi katika maeneo yaliyokaliwa ya nchi hiyo kuisaidia Urusi nchini Ukraine.
Anaamini kwamba madai kuhusu kifo cha maafisa wa kijeshi wa Korea Kaskazini katika eneo linalokaliwa na Urusi la Donbass "labda ni kweli."
Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini ameliambia shirika la habari la Yonhap kuwa : "Kwakuwa Urusi na Korea Kaskazini zimefikia makubaliano sawa na muungano wa kijeshi, uwezekano wa kutuma wanajeshi katika maeneo ya vita ni mkubwa sana."
Anazungumzia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati yaliyotiwa saini mwezi Juni mwaka huu kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Katika siku za nyuma, kulikuwa na ripoti juu ya uwezekano wa ushiriki wa vikosi vya Korea Kaskazini nchini Ukraine kuisaidia Urusi. Mnamo Septemba 2023, wakati Vladimir Putin alipokutana na Kim Jong Un katika kituo cha anga cha Vostochny cha Urusi, alizitaja ripoti hizo kuwa "hazina msingi wowote."
Mnamo Juni 2024, wakati Putin alipotia saini mkataba na Kim Jong Un ambao ulijumuisha kifungu cha ulinzi wa pamoja, aliulizwa juu ya uwezekano wa kupeleka vikosi vya Korea Kaskazini nchini Ukraine.
Rais wa Urusi alijibu: "Hatumuomba mtu yeyote, hakuna mtu aliyetoa pendekezo kama hilo."
Kuongezeka kwa ushirikiano

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Moscow na Pyongyang hazifichi kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi.
Mnamo Julai 2023, waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alisafiri kwenda Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, "kuimarisha uhusiano wa kijeshi kati ya pande hizo mbili," kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi. Mwezi Septemba, Kim Jong Un alisafiri kwenda eneo la Mashariki ya mbali la Urusi.
Mnamo Septemba 2023, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol, katika hotuba yake ya kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alitaja uwezekano wa kutuma silaha kutoka Korea Kaskazini kwenda Urusi badala ya kupokea teknolojia ya kijeshi ya Urusi.
Mnamo Oktoba 16, 2023, Taasisi ya mafunzo ya ulinzi ya Uingereza ilichapisha ripoti juu ya usafirishaji mkubwa wa silaha kwa Urusi. Ripoti hii ilijumuisha picha za satelaiti za eneo la kuhifadhi silaha hizi.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amekanusha madai hayo.
"Sio tu intelijensia ya Uingereza, bali ni ujasusi wa Marekani," Peskov alisema. "Wanaendelea kuchapisha taarifa hizi, lakini hawatoi ushahidi wowote."
Mwishoni mwa 2023, sifa za kiufundi za makombora ya Korea Kaskazini na migodi inayotumiwa na vitengo vya Urusi nchini Ukraine zilivutia umakini na zilijadiliwa katika duru za kijeshi za Kirusi (matokeo ya hakiki yalikuwa hasi zaidi).
Tunafahamu nini kuhusu jeshi la Korea Kaskazini?

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Korea Kaskazini, kama nchi yenyewe, lina muundo uliofungwa na machache sana yanayojulikana kuhusu muundo wake. Kwa sababu hii, tathmini juu ya uwezo wake wa vita ni chini ya utata.
Sifa yake kuu ni idadi kubwa ya wanajeshi.
Huduma ya jumla ya kijeshi ni lazima katika nchi hii na inajumuisha wanawake pia. Muda wa utumishi wa kijeshi ni kati ya miaka 3 na 10, kulingana na kitengo cha jeshi.
Kwa mujibu wa taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya kimkakati, mwaka 2018, majeshi ya Korea Kaskazini yalikuwa jeshi la nne kwa ukubwa duniani na takriban watu milioni 1.2 walihudumu katika jeshi hilo.
Andrei Gubin, mtaalamu katika taasisi ya mafunzo ya mkakati ya Urusi, anasema kuwa takwimu hii inaweza kuwa ya juu sana. Katika makala kuhusu uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini, anaandika: "Kwa sasa, idadi ya wafanyakazi katika Jeshi la Watu wa Korea ni zaidi ya 850,000, na kuna makadirio ya 650,000 katika vitengo vya mapambano."
Lakini wakati huo huo, anasisitiza kuhusu uwezo wa uhamasishaji mkubwa wa wanajeshi kutumikia jeshini na kusema: "Angalau watu milioni nne wako katika kikosi cha akiba, na rasilimali za jumla za uhamasishaji zinafikia huo ni takriban za uwezo wa kufikia hadi watu milioni 2.6."
Aidha, kuna makundi mengi ya wanamgambo nchini Korea Kaskazini, ambayo yanaitwa wanamgambo wa watu.
Andrey Gorbin anasema: "Mashirika ya kijeshi ni pamoja na Wafanyakazi-Peasant Red Guards (senior reserves) na watu milioni 1.5, Vijana Red Guards na watu 700,000 (wanafunzi wa shule ya sekondari), na vikosi vya wizara ya usalama wa umma na usalama wa taifa na vikiwa na jumla ya watu 30,000. "
Korea Kaskazini, chini ya vikwazo na inahitaji sana fedha, na kwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa kijeshi waliofunzwa, inaonekana kuwa haina shida kutuma baadhi ya vikosi vyake kusaidia mmoja wa washirika wake wachache.
Lakini suala hili si rahisi sana.

Chanzo cha picha, Reuters
Haiwezekani kuficha usamabazaji wa vikosi
Jeshi la Korea Kaskazini linatokana na mfano wa zamani wa Soviet na hutumia teknolojia ya kijeshi ya Usovieti, lakini tofauti na jeshi la Urusi, haina uzoefu katika vita halisi.
Haijulikani ni jukumu gani jeshi la Korea Kaskazini linaweza kuwa nalo katika vita vya Urusi nchini Ukraine, na iwapo linaweza kufanya kazi kwa kujitegemea kama sehemu ya vitengo vikubwa vya mitambo kwa njia ambayo majeshi yake yanafundishwa.
Je, wanaweza kufanya kazi katika vikundi vidogo? Hii inahitaji kiwango tofauti cha uratibu na mwingiliano, na angalau hakuna kizuizi cha lugha.
Katika hali zote mbili, hasara haziepukiki na sababu hii inaweza kuwa muhimu.
Haiwezekani kuficha ushiriki wa Pyongyang katika operesheni za kijeshi za Urusi.
Idadi kubwa ya wanajeshi wa Korea Kaskazini huenda wakauawa au kukamatwa - kitu ambacho Ukraine hakika itaweka hadharani - na hii itadhoofisha taswira ya kutoonekana kwa jeshi la Korea Kaskazini linalokuzwa na propaganda za serikali.
Andrey Gobin anaandika: "Katika wakati wa amani, ni vigumu sana kujaribu roho ya mapigano na utayari wa kujitolea kwa vikosi. " Mifano ya kihistoria ya ushujaa wa kibinafsi uliofanywa na wanajeshi katika vita vya Korea kati ya 1950 na 1953 sio ushahidi wa kutosha kwa hili."
Kupoteza udhibiti wa wanajeshi kunaweza pia kusababisha hatari fulani kwa uongozi wa Korea Kaskazini. Hii inaweza kutokea wakati vikosi vya nchi hii havifanyi kazi kama vitengo tofauti na ni sehemu ya vitengo vya Urusi.
Aidha, licha ya umoja wa nchi hizo mbili, itikadi ya viongozi wa Urusi na Korea Kaskazini ina utofauti mkubwa.
Wafanyakazi wa gharama rahisi

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Korea Kaskazini linategemea mfano wa jeshi la Sovieti
Sababu hizi zote hazimaanishi kuwa ushiriki wa jeshi la Korea Kaskazini katika vita vya Urusi nchini Ukraine unaweza kupuuzwa.
Pyongyang inahitaji fedha na teknolojia, wakati Moscow inahitaji wanajeshi na risasi, na pande zote mbili zina nia ya kuendeleza ushirikiano wa kijeshi.
Kwa miaka mingi, jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likitumika kama kazi gharama nafuu.
Vingi kati ya vitengo vyake vikifanya kazi ya uhandisi wa Soviet na ujenzi.
Wataalamu wa kijeshi mara nyingi hupima ubora wa miundo ya ulinzi iliyojengwa na wahandisi wa Korea Kaskazini na vitengo vya ujenzi.
Inawezekana kwamba vitengo kama hivyo vitakuwa na manufaa kwa jeshi la Urusi.
Wanaweza kupelekwa nyuma ya mstari wa mbele wa mapigano na kutumika kujenga miundombinu ya kijeshi, kama vile mahandaki ya chini ya ardhi, ngome, barabara na madaraja.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












