Kwanini nyota wa Westham huvalia jezi yenye muundo tofauti?

    • Author, Mariam Mjahid
    • Nafasi, BBC Swahili
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Shati ya jezi ya Antonio imekuwa ikionekana tofauti na za wachezaji wenzake wa timu ya Westham United.

Msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ulipoanza alikuwa akitumia makasi kukata kola ya jezi yake .kisa?ilikuwa ikimbana kwenye shingo kutokana na maumbile ya shingo yake kuwa pana.

Lakini baada ya wiki kadhaa watengenezaji wa jezi za Westham United wakaamua kumtengenezea jezi spesheli iliyo na mwanya katika shingo.

Mchezaji huyu ameonekana akivalia jezi hilo katika mchuano na New castle usiku wa Jumatatu.

Ingawa alilazimika kubadilisha shati kipindi cha kwanza kikiendelea baada ya shati yake kuraruka katika sehemu hiyo ya mwanya baada ya kuvutwa na mchezaji wa Newcastle.

Ni mshambuliaji wa klabu ya westham United akiwa amevaa jezi ya nambari 9 mgongoni.

Raia huyu wa uingereza amefungia west ham bao moja na kuzalisha bao moja katika mechi za Epl msimu huu.

Sababu za Antonio kuchezea timu ya Jamaica

Ingawa ni mzaliwa wa Uingereza anaiwakilisha timu ya taifa ya Jamaica.Je alijipataje akichezea taifa hilo.

Mnamo Machi 2016, Antonio alifichua kwamba alikuwa amekataa nafasi ya kuichezea Jamaika kimataifa na kwamba alikuwa na nia ya kuichezea Uingereza.

Mnamo tarehe 18 Juni 2021, Antonio aliteuliwa katika kikosi cha wachezaji 60 cha Jamaika kwa Kombe la Dhahabu la CONCACAF 2021, lakini alikosa nafasi katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kutokana na kuchelewa kupata pasipoti ya Jamaika.

Agosti 2021, alipopata pasipoti hiyo, alijumuishwa katika kikosi cha wachezaji 35 kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Mexico, Panama, na Costa Rica, ingawa vikwazo vya COVID-19 vilimzuia kucheza dhidi ya Mexico na Costa Rica.

Alifanya debut yake ya kimataifa tarehe 5 Septemba 2021 dhidi ya Panama, ambapo Jamaica ilishindwa 3-0, na alicheza kwa dakika 70.

Katika mechi yake ya pili, dhidi ya El Salvador, alifunga bao lake la kwanza, ingawa mchezo ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Tarehe 26 Juni 2024, Antonio alifunga bao la kwanza kwa Jamaika katika mashindano ya Copa América, ingawa timu yake ilishindwa 3-1 dhidi ya Ecuador.

Kiungo cha Antonio na asili yake ya soka isiyokuwa ya ligi ni cha muhimu, kulingana na Bosah.

Anasema: “Kiungo hicho kati yake na Tooting & Mitcham ni urithi ambao ni chanzo cha msukumo katika klabu na umeacha alama hapa.

“Tunaendelea kukuza wachezaji ambao wanapata nafasi katika ligi kubwa na bora. Alichowaachia kilimhamasisha mwenyekiti kuendelea na kazi yake. Wachezaji wamefika katika Ligi Kuu, League One na League Two.

“Kuna maendeleo mengi yanayoendelea kutokana na urithi wake – kwa hiyo tunajivunia sana kuwa na uhusiano na hilo. Anaonekana kuwa chanzo cha msukumo kwa kizazi kilichofuata.”

Maisha yake ya Utotoni

Ni mzaliwa wa wilaya ya Wandsworth ,Uingereza tarehe 28 mwezi machi 1990 .

Wazazi wake ni waingereza weusi ambao ukoo wao ni Jamaika.Akiishi Borough alikolelewa kuna kipindi eneo hilo lilikumbwa na kadhia ya magenge .Kulingana na ripoti kutoka Daily Mail,winga huyu aliwahi kushuhudia visa kadhaa vya watu wakidungwa visu nakuuawa na magenge hao akitaja ilikuwa ni jambo la kawaida kwake kukuana na visa kam hivyo."Baadhi ya marafiki zangu walidungwa visu hadi kufa,hata wengine walipigwa risasi na kuponea nikiwaona.Hakika nimeona mengi maishani mwangu"Antonio aliiambia gazeti la Sun

Kujihusisha na mpira kulimuepushia kuungana na magenge hatari ambao walikuw awamekithiri na kuteka vijana wengi wakati huo.

Kutokana na maisha yake na safari yake ya kuingia kwa spoti alijipatiwa jina "The Beast".

Amechezea vilabu kadhaa uingereza ikiwemo Reading,Sheffield Wednesday na Nottingham forest.

Je,jezi za awali zilikuwa spesheli?

Licha ya kuwa katika kikosi kinachoongozwa na Julen Lopetegui kwa miaka kadhaa ,jezi za wananyundo zimekuwa zikimfaa ila za msimu huu jezi ilikuwa ndogo shingoni.

Mnamo Februari 2019, Antonio alipendekeza kwamba vilabu ambavyo mashabiki wake hushiriki katika unyanyasaji wa rangi wanapaswa kukatwa pointi.

Wakati wa uchaguzi mkuu wa 2019 nchini Uingereza, Antonio aliidhinisha Sara Kumar, mgombeaji wa Chama cha Conservative katika eneo bunge la West Ham.