Jeremy Bowen: Mpango wa Trump kudhibiti Gaza hautafanyika, athari yake ni ipi?

    • Author, Jeremy Bowen
    • Nafasi, International editor
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Pendekezo la Rais Donald Trump kuchukua na kudhibiti Gaza, kuwapatia makazi mapya Wapalestina haitawezekana kutekelezwa.

Italazimu mataifa ya kiarabu kuunga mkono pendekezo hilo ambalo wamelipinga vikali.

Ikiwemo Jordan na Misri ambayo ni mataifa ambayo Trump analenga kuwapeleka Raia wa Palestiana bila kusahau Saudia Arabia ambao pia wanatarajiwa kugharamia hifadhi ya raia hao milioni 1.8.

Marafiki wa karibu wa Marekani pia baadhi yao wamepinga vikali wazo la Trump.

Japokuwa wengi wao wangependelea kuondoka Gaza kuanzisha maisha mapya haitakuwa rahisi kwa wengi ambao watabakia.

Labda Marekani itumie nguvu na mamlaka iliyonayo kuwafurusha wapalestina kutoka Gaza.

Tangu Marekani kujaribu kudhibiti Iraq mwaka 2003, hatua hii haitapigiwa upatu na Wamarekani.

Pia unaweza kusoma:

Hatua hii pia itakuwa ni mwisho wa matumaini yaliyokuwepo ya mataifa hayo mawili ya kusuluhisha mgogoro uliopo.

Hii ikiwa ni suluhu wa mgogoro ambao umedumu kwa miongo ambao ungeafika lengo la kuzindua Palestina iliyo huru kando na kutawaliwa na Israel.

Netanyahu ambaye ni waziri mkuu wa Israel amekuwa akilipinga suala hilo la Palestina kuwa huru na mazungumzo ya amani yakigonga mwamba yaliyoendekeza mataifa mawili yaliyo na ''watu wawili tofauti'' ikawa ni propaganda.

Ila ilikuwa imeanikwa katika sera ya mataifa ya nje ya Marekani tangu miaka ya 90.

Hatua hiyo ya Rais Trump ikiendela kutekelezwa itakiuka sheria za kimataifa.

Madai ya Marekani ambayo tayari yameenea kuwa inaamini katika utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria ungevunjwa.

Matarajio ya eneo la Urusi nchini Ukraine na Uchina huko Taiwan yatazuiliwa.

Hatua hiyo itakuwa na athari gani kwa eleo hilo?

Kwanini tamko hilo limezua hofu wakati pendekezo hilo halitarajiwi - hasa namna Trump anavyoieleza akiwa Washington, akisindikizwa na Benjamin Netanyahu.

Jibu ni kuwa Matamshi ya Trump huenda yasitekelezwe lakini yana athari kubwa.

Ni Rais wa Marekani , mtu mwenye ushawishi mkubwa duniani - na sio tu mwanamitindo anayetaka umaarufu kupitia kauli zenye utata.

Pendekezo lake linaweza kuathiri makubaliano ya kusitisha vita nchini Gaza ambayo yalikuwa yameanza.

Kutokuwa na mkakati wa mustakabali wa uhuru wa Gaza tayari umeingiza kiwewe ndani ya makubaliano yakusitisha vita vya Gaza.

Sasa Trump amekuja kivingine tena, ingawa haitatokea kama alivyosema lakini amewapa taswira mpya walowezi na Palestina namna wanavyojichukulia.

Itaimarisha mikakati na ndoto za uzalendo wa walio na msimamo mikali ya walowezi ambao wanaamini ardhi yote kati ya bahari ya Mediterranean na mto Jordan, ni mali waliobinafsishwa na Mungu.

Viongozi walio na msimamo kama huu ni miongoni mwa wajumbe wa serikali ya Netanyahu na wanaompa mamlaka zaidi na wanafurahia hilo.

Wanapendelea vita vya Gaza virejee vikilenga kuwafurusha Wapalestina na kutoa fursa kudhibiti Walowezi.

Waziri wa masuala ya fedha Bezalel Smotrich alisema wazo la Rais Trump limeeleza wazi mustakabali wa Gaza baada ya mashambulizi ya mwezi Oktoba tarehe 7.

Kupitia taarifa yake anasema ''aliyejaribu kuvamia Israel inamaana atajipata amepoteza ardhi yake milele.

Na hili linatupa fursa yakuzika wazo la kuipa uhuru Palestina.''

Upande wa upinzani ambao wako katika serikali ya Israel hawajaoneka kutoa msimamo thabiti wakiogopa kukemewa japo kwa kusita wamekaribisha wazo hilo la Trump.

Hamas na baadhi ya vikundi vilivyo na silaha vya Palestina wanatarajiwa kujibu kauli ya Trump kwa mpigo na labda kuishambulia Israel.

Kwa upande wa Palestina, mzozo kati yao na Israel unajikita katika mzizi ya kumbukumbu ya wanachokiita al- Nakba, kama janga.

Huo ulikuwa uhamisho wa Palestina huku Walowezi wakishinda vita vya kupigania uhuru mwaka 1948.

Zaidi ya Wapalestina 700,000 walitoroka au walilazimishwa kutoka makazi yao na Walowezi.

Wengi wao ambao waliruhusiwa kurejea walilazimika kufuata sheria za Israel zilizoidhinishwa ambazo wanazitumia kuwapokonya mali yao.

Sasa uoga unaowaingia raia wa Palestina ni kuwa jambo kama hilo huenda likatokea tena.

Huko Palestina wanaamini Israel ina njama ya kutumia vita hivi na Hamas kuharibu Gaza na kufuta kizazi cha Palestina.

Ni kati ya wanachodai kuwa Israel inatekeleza mauaji ya kimbari na sasa wanaeza anza kuamini kuwa Donald Trump anagongelea msumari njama hizo za Israel.

Je, ni kipi kimeshinikiza Trump kupendekeza kudhibiti Gaza?

Kauli ya Trump haina mashiko yoyote, na pia haipatii uzito kuwa itatekelezwa.

Huenda pia Trump anazua siutafahamu huku akijipanga na mkakati tofauti wa kudhibiti vita hivyo.

Inasemekana anatamani sana kushinda tuzo za amani.

Huku ulimwengu ukiendelea kupambanua pendekezo lake kuhusu Gaza, aliandika katika mtandao wa kijamii kuwa hamu yake ya "makubaliano ya amani ya nyuklia yaliyothibitishwa" na Iran.

Utawala wa Irani unakanusha kuwa unataka silaha za nyuklia lakini kumekuwa na mjadala wa wazi huko Tehran kuhusu ikiwa sasa wanatishiwa sana kwamba wanahitaji kizuizi cha mwisho.

Kwa miaka sasa, Netanyahu ametaka Marekani ikisaidiwa na Israel kuharibu maeneo yaliyohifadhiwa nyuklia.

Kuingia katika mkataba na Iran haikuwa kati ya mikakati yao.

Katika kipindi cha kwanza kama Rais wa Marekani, Netanyahu amekuwa akimshawishi Trump kwa muda akitaka Marekani ijiondoe katika mkataba uliotiwa saini katika utawala wa Barack Obama na Iran.

Iwapo Trump angetaka kuwafurahisha Israel kwa uamuzi wake, kwa hilo amefua dafu.

Lakini ameanzisha siutafahamu na kuchochea utovu wa amani katika eneo ambalo limekuwa likikumbwa na misukosuko kwa muda sasa.

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid