'Niliingia kwenye dunia ya siri ya ulevi wa ngono, nikageuka kuwa zombi'

ok
Maelezo ya picha, Chris, sio jina lake halisi, alianza kukosa kwenda kazini kwa sababu ya kujihusisha na ulevi wa ngono (chemsex)
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mwanaume aliyeingia katika dunia ya kufanya ngono huku akiwa amelewa (chemsex), ameeleza jinsi alivyogeuka kuwa "zombi" na maisha yake yalikuwa yakiharibika polepole.

Chris - jina lake limebadilishwa - ameiambia BBC alianza kushiriki katika matumizi ya dawa kabla ya kufanya ngono, ambazo zilimsaidia kuficha "aibu" na kuanza kuvutiwa na mapenzi ya jinsia moja.

Mkaazi huyo wa London anasema baada ya kuwa mraibu wa ngono na dawa za kulewa – utamaduni ambao kwa kawaida huhuhusishwa na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao - hutumia ulevi ili kuongeza hamu ya kufanya ngono - kwa Chris alikabiliwa na upweke.

Wanaharakati wanasema kuna unyanyapaa kwa sababu ya mapenzi ya jinsia moja. Serikali inasema inafahamu madhara yanayosababishwa na ngono za aina hiyo na imetoa mwongozo kwa serikali za mitaa kusimamia suala hilo.

Mwanzo wake, Chris alipewa dawa kwenye sherehe, lakini miezi michache baadaye ndipo alianza kuitafuta zaidi na kukutana na watu ambao walikuwa wakitumia dawa hizo za kulevya.

Anasema mwanzoni ilimwondolewa "aibu na kuingia kwenye mapenzi ya jinsia moja." Hata hivyo, hilo lilibadilika haraka.

"Hakuna mtu anayezungumza juu ya jambo hilo. Kila mtu ana aibu. Yote yako nyuma ya pazia. Hayazungumzwi katika dunia ya kawaida. Ni ya siri sana," anasema.

Chris anasema marafiki zake walimwambia anakaribia kuwa kama "zombi."

"Taratibu maisha yako yanaanza kuharibika kwa sababu unakosa kwenda kazini siku ya Jumatatu, halafu kazi zako zinakosa kuwa kwenye kiwango bora.

"Huwezi kufanya mengi ya mambo hadi Jumatano. Na kisha unatumia tena dawa siku ya Ijumaa," anasema.

Wanaharakati wanasemaje?

L
Maelezo ya picha, Ignacio Labayen De Inza anasema chemsex ni "mtego"

Ignacio Labayen De Inza, kutoka shirika la hisani lenye makao yake makuu mjini London la Kudhibiti Chemsex, anatoa wito kwa watu kuanzisha mazungumzo ili kusaidia kubadilisha mtazamo.

Anasema kuna unyanyapaa kwa sababu "inahusu ngono, inahusu ngono ya mashoga, inahusu madawa ya kulevya."

K
Maelezo ya picha, Philip Hurd alijihusisha na matumizi ya chemsex kwa miaka 12

Philip Hurd, mshauri katika shirika la Controlling Chemsex, kwa miaka 12 iliyopita, anasema alichukua dozi kubwa karibu kufa ndipo akatambua anahitajika kuiacha.

Anasema: "Unaanza kufanya mambo ambayo ni hatari."

Madaktari walisema nina bahati sana kuishi, na ilibidi niwahusishe wazazi wangu waliokuwa katika miaka yao ya themanini. Kufikia hapo, ndipo nilipofikiri sasa siwezi kuendelea hivi; "nitakufa."

Hurd, anaishi London na sasa anajitolea katika shirika la Controlling Chemsex, anatumia uzoefu wake kusaidia wengine.

Utafiti na usaidzi

FCV
Maelezo ya picha, Veronika Carruthers, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Portsmouth, anasema usaidizi unaopatikana sasa bado "ni mdogo sana"
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Utafiti wa Opinium Research kwa watu 2,000 umegundua kuwa 76% ya wale waliohojiwa hawajui lolote kuhusu chemsex.

Zaidi ya theluthi moja ya wale wanaojitambulisha kama mashoga/wasagaji, utafiti umegundua hawafahamu hatari za chemsex.

Veronika Carruthers, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Portsmouth, amekuwa akifuatilia saula hili na anasema kuna usaidizi mdogo sana.

Anasema baadhi ya watu hawajui huduma sahihi za kwendea.

"Kuhusiana na huduma za ushauri juu ya dawa za kulevya, mara nyingi tuna wafanyakazi wa afya ambao hawajawahi kusikia kuhusu chemsex na kwa hivyo hawawezi kutoa aina yoyote ya usaidizi.

"Matokeo yake watu hawataki kuomba msaada au usaidizi kutoka kwa mashirika fulani."

Msemaji wa Idara ya Afya ya Jamii anasema pamoja na kutoa mwongozo kwa serikali za mitaa, imeongeza ruzuku kwa idara ya Afya ya Umma kwa karibu pauni milioni 200.

"Serikali za mitaa zinaweza kutumia ruzuku hii kuboresha matibabu juu ya madawa ya kulevya na pombe, ikiwa ni pamoja na watu wanaojihusisha na chemsex," anasema msemaji huyo.

"Tunaendelea kufanya kazi na makamishna wa kupambana na matumizi mabaya ya dawa na makamishna wa masuala ya afya ya ngono ili kuboresha upatikanaji wa huduma na usaidizi kwa wale wanaotumia madawa ya kulevya katika muktadha huu."