Je, nguvu ya mashambulizi ya Iran inalinganishwaje na ya Israel?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, By Arif Shamim
    • Nafasi, BBC News Urdu & BBC News Persian
  • Muda wa kusoma: Dakika 12

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limefanya mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani na roketi kaskazini mwa Israel katika kipindi cha wiki moja iliyopita, lakini linaonya kuwa hatua yake ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kamanda wa ngazi ya juu wa Israel mwezi Julai bado haijafika.

Mapema siku ya Jumanne, watu wanne waliuawa katika shambulio la nyumba moja katika mji wa Mayfadoun nchini Lebanon, karibu kilomita 30 kaskazini mwa mpaka, madaktari na chanzo cha usalama kimesema.

Mapigano hayo yanafuatia kuongezeka kwa mvutano kati ya Israel, Iran na Hezbollah, na kusababisha hofu ya kuzuka kwa mzozo mkubwa.

Kwa hivyo, pande hizi zingeegemea wapi iwapo vita vikubwa vingezuka?

Unaweza pia kusoma:
.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa katika shambulizi la anga katika mji mkuu wa Iran Tehran

Wiki iliyopita, Hamas ilisema kiongozi wake wa kisiasa, Ismail Haniyeh, aliuawa katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Israel haijathibitisha iwapo ilihusika na shambulio hilo.

Kumekuwa na mvutano mkubwa tangu Iran ilipoanzisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Israel tarehe 13 mwezi Aprili na ndege isiyo na rubani ya Israel ilishambulia eneo la kijeshi nchini Iran.

Ingawa hakukuwa na majeruhi wengi nchini Israel, mashambulizi ya mabomu zaidi ya 300 yalionyesha uwezo wa Iran wa kushambulia kutoka mbali.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwezo wa Iran kuunda makombora umeifanya kuwa na uwezo mkubwa kijeshi

Upande gani una udhibiti?

BBC imepima swali hili kwa kutumia vyanzo vilivyoorodheshwa hapa chini, ingawa kila nchi inaweza kuwa na uwezo mkubwa ambao umefichwa.

Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati (IISS) inalinganisha nguvu ya mashambulizi ya majeshi ya mataifa yote mawili, kwa kutumia njia mbalimbali rasmi na za wazi ili kupata makadirio bora iwezekanavyo.

Mashirika mengine, kama vile Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, pia hufanya tathmini, lakini usahihi unaweza kutofautiana kwa nchi ambazo mara nyingi hazitoi takwimu.

Hata hivyo, Nicholas Marsh, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Amani Oslo (PRIO), anasema IISS inaonekana kama alama ya kutathmini nguvu za kijeshi za nchi duniani kote.

g

IISS inasema Israel ina matumizi ya juu zaidi katika bajeti yake ya ulinzi kuliko Iran, na kuipa nguvu kubwa katika mzozo wowote unaoweza kutokea.

IISS inasema bajeti ya ulinzi ya Iran ilikuwa karibu $7.4bn mwaka 2022 na 2023, wakati Israel ilikuwa na zaidi ya mara mbili ya bajeti hiyo, karibu $ 19bn.

Matumizi ya ulinzi wa Israel ikilinganishwa na Pato la Taifa (kipimo cha pato lake la kiuchumi) pia ni mara mbili ya Iran.

F-35 plane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege aina ya F-35 ni moja ya ndege za kisasa zaidi duniani

Hatua inayofuata

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Israel na Hezbollah zimeongeza mashambulizi dhidi yao. Israel imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Hezbollah nchini Lebanon na kusema kuwa ilitekeleza mauaji ya kamanda wa ngazi ya juu Fuad Shukr tarehe 30 Julai 2024.

Hezbollah imerusha makombora kaskazini mwa Israel. Mfumo wa Israel wa Iron Dome wa kupambana na makombora ulizuia mengi kati ya mashambulio hayo.

Hata hivyo, Jeremy Binnie, mtaalamu wa Ulinzi wa Mashariki ya Kati katika jarida la uchambuzi wa ulinzi Janes anaonya, "Iron Dome ni mfumo wa ulinzi unaotetea dhidi ya makombora ya masafa mafupi na makombora yaliyorushwa kutoka Lebanon, ingawa inadhaniwa kwamba Hezbollah ina makombora mengi zaidi ya kuutatiza ulinzi wa anga wa Israel kwa muda mrefu.''

Nicholas Marsh wa Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Oslo anasema "Iran imechapisha orodha kubwa ya maeneo itakayoyashambulia. Hii inaweza kuwa ni jaribio la kusumbua. Lakini itakuwa vigumu kwa Israel kufikia malengo yote yanayowezekana."

.

Chanzo cha picha, WAEL HAMZEH/EPA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Bango la kamanda wa ngazi ya juu wa Hezbollah Fuad Shukr likionyeshwa wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya wiki moja tangu alipouawa katika shambulio la anga la Israel nchini Lebanon

Je, kunaweza kuwa na shambulio kubwa?

Mhariri wa masuala ya ulinzi Tim Ripley ameiambia BBC kuwa wanaopanga mikakati ya kijeshi wanapaswa kufikiria "mbinu mbali mbali" kuhusu majibu ya Iran na Hezbollah.

"Lazima ujiingize katika mawazo ya Wairani, Hezbollah na Wahouthi (wanamgambo wa Kiislamu ambao wamekuwa wakishambulia meli za kimataifa katika Mashariki ya Kati). Kwa nini upoteze juhudi zako kufanya kitu kimoja tena?"

Ripley anasema kwamba Iran inaweza kuihamasisha Hezbollah kufanya mashambulizi ya mpakani - labda kwa sababu inaweza kuona jinsi mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7 yalivyoishangaza Israel, wakati mashambulizi ya kawaida ya makombora yanashindwa kuvunja ulinzi wa Israeli kwa urahisi.

Pia amesema Iran inaweza kufikiria kuzikamata meli za mafuta za kigeni.

Lakini Jeremy Binnie anaamini kuongezeka kwa mashambulizi haiwezekani:

"Kikosi cha Hezbollah cha Radwan kimekuwa kikitoa mafunzo kwa operesheni za mipakani, lakini hisia zangu ni kwamba hakitahusika katika ulipizaji kisasi," anasema.

"Kwa upande mmoja, IDF (Vikosi vya Ulinzi vya Israeli) vitakuwa tayari zaidi kwa hali hiyo kuliko ilivyokuwa mnamo 7 Oktoba; Kwa upande mwingine, utekaji nyara wa idadi ndogo ya raia wa Israel huenda ukachochea ongezeko kubwa la mashambulizi kama ilivyokuwa mwaka 2006."

Mwaka 2006, Israel ilifanya mashambulizi ya ardhini nchini Lebanon baada ya Hezbollah kuwateka nyara wanajeshi wawili wa Israel. Kulikuwa na mapigano makali na vifo vingi kwa pande zote mbili.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wafanyakazi wa uokoaji wakipekua vifusi vya jengo lililoshambuliwa na Israel katikati ya viunga vya mji wa Beirut uliotawaliwa na Washia tarehe 13 Agosti 2006.

Ripley anasema Israel inaweza kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Hezbollah ili kuivunja moyo, badala ya kuwa na athari kubwa kwa nguvu za kijeshi za kundi hilo.

"Hiki ndicho walichokifanya Lebanon mwaka 2006 na Gaza sasa," anasema.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wazima moto wakitembea juu ya paa la nyumba kaskazini mwa Israel ambapo lilitokea shambulio la moja kwa moja la roketi lililorushwa kutoka kusini mwa Lebanon tarehe 23 Julai 2006

Faida ya teknolojia

Takwimu za IISS zinaonyesha kuwa Israel ina ndege 340 za kijeshi tayari kwa mapambano, na hivyo kuifanya kuwa na makali ya mashambulizi ya anga.

Miongoni mwa ndege hizo ni ndege za F-15 zinazoshambulia maeneo ya masafa marefu , F-35s - ndege za hali ya juu za "stealth" ambazo zinaweza kukwepa rada - na helikopta za mashambulizi ya haraka.

Shirika la ndege la Iran linakadiria kuwa Iran ina ndege 320 za kivita . Ndege hizo zilianza kutumika miaka ya 1960 na zinajumuisha F-4s, F-5s na F-14s (ya mwisho ni ndege iliyopata umaarufu katika filamu ya Top Gun mwaka 1986).

Lakini Nicholas Marsh wa RIO anasema haijulikani ni ndege ngapi za zamani zinaweza kuruka, kwa sababu ukarabati utakuwa mgumu sana. Hii ni kutokana na vikwazo vya mataifa ya magharibi dhidi ya Iran.

The F-14 was featured in 1986 movie Top Gun

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege hiyo aina ya F-14 Tomcat iliondolewa na jeshi la wanamaji la Marekani miaka 20 iliyopita, lakini bado inahudumu nchini Iran

Iron Dome na Arrow

Uti wa mgongo wa ulinzi wa Israeli ni mifumo yake ya Iron Dome na Arrow.

Mhandisi wa makombora Uzi Rubin ni mwanzilishi wa Shirika la Ulinzi la Israel katika Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.

Pia ni mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Mkakati na Usalama ya Jerusalem, aliiambia BBC jinsi "salama" alivyohisi wakati alipoona Iron Dome na washirika wa kimataifa wakiharibu karibu makombora yote na ndege zisizo na rubani ambazo Iran ilizishambulia Israel siku ya Jumamosi.

"Nilikuwa na furaha na furaha sana... Ni mahsusi sana dhidi ya malengo yake. Ni ulinzi wa makombora ya masafa mafupi. Hakuna kitu kama hicho katika mfumo mwingine wowote."

Anti-attack missiles fired above Israel

Chanzo cha picha, Amir Cohen / Reuters

Maelezo ya picha, Mfumo wa ulinzi wa makombora wa Iron Dome wa Israel ulisaidia kuharibu zaidi ya makombora 300 na ndege zisizokuwa na rubani zilizofyatuliwa na Iran mwishoni mwa wiki

Iran iko mbali kiasi gani kutoka Israel?

Israel iko umbali wa zaidi ya kilomita 2,100 kutoka Iran. Makombora yake ndiyo njia kuu ambayo inaweza kushambulia nchi hiyo, mhariri wa masuala ya ulinzi Tim Ripley anasema.

g

Mpango wa makombora wa Iran unachukuliwa kuwa mkubwa na tofauti zaidi katika Mashariki ya Kati.

Mwaka 2022, Jenerali Kenneth McKenzie wa kikosi cha Central Command cha Marekani alisema Iran ilikuwa na makombora zaidi ya 3,000 ya masafa marefu.

Kwa mujibu wa mradi wa ulinzi wa makombora wa CSIS, Israel pia inauza makombora kwa nchi kadhaa.

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Iran ilirusha makombora zaidi ya 300 na ndege zisizokuwa na rubani nchini Israel Jumamosi Aprili 13

Makombora ya Iran na ndege zisizo na rubani

Iran imefanya kazi kubwa katika mifumo yake ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani tangu vita vyake na nchi jirani ya Iraq, kuanzia mwaka 1980 hadi 1988.

Imetengeneza makombora ya masafa mafupi na marefu na ndege zisizo na rubani, nyingi ambazo zilirushwa hivi karibuni nchini Israel.

Wachambuzi wanaochunguza makombora yaliyolengwa na waasi wa Houthi nchini Saudi Arabia wamehitimisha kuwa makombora hayo yalitengenezwa nchini Iran.

Jengo la ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria liliharibiwa katika shambulio la anga la tarehe 1 Aprili, na kuwaua wanajeshi wa ngazi ya juu wa Iran.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, .

'Adhibu' kupitia mashambulizi ya masafa marefu

Tim Ripley wa shirika la ulinzi la Israel amesema Israel ina uwezo mkubwa wa kuingia katika vita vya ardhini na Iran: "Faida kubwa ya Israel ni nguvu zake za anga na silaha zake zinazoongozwa. Kwa hivyo ina uwezo wa kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya shabaha muhimu nchini Iran."

Ripley anasema Israel ina uwezekano mkubwa wa kuwaua maafisa na kuharibu mitambo ya mafuta kutoka angani.

"'Adhibu' iko katika moyo wake... Viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Israel hutumia neno hilo kila wakati. Ni sehemu ya falsafa yao, kwamba wanapaswa kuleta maumivu ili kuwafanya wapinzani wao wafikirie mara mbili juu ya upinzani wao kwa Israeli."

Katika siku za nyuma, wanajeshi wa ngazi ya juu wa Iran na raia wameuawa katika mashambulizi ya anga, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa jengo la ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa Syria, ambao ulisababisha shambulio la Iran.

Israel haijadai kuhusika na mashambulizi hayo au mashambulizi kadhaa yanayowalenga maafisa wa ngazi ya juu wa Iran.

Hata hivyo, hakukanusha kuwajibika.

.

Chanzo cha picha, IRGC handout / Reuters

Maelezo ya picha, Wachambuzi wanasema jeshi la wanamaji la Iran halina uwezo wa kupigana katika vita - Jeshi la wanamaji la Iran lina meli 220, wakati Israel ina takriban meli 60, kwa mujibu wa ripoti za IISS

Vikosi vya majini

Jeshi la majini la Iran lina meli 220, wakati Israel ina takriban meli 60, kwa mujibu wa ripoti za shirika la habari la IISS.

Wachambuzi wanasema jeshi la majini la Iran halina uwezo wa kupigana katika vita.

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, IISS inasema jeshi la majini la Israel lina meli 60

Mashambulizi ya kimtandao

Israel ina mengi ya kupoteza kuliko Iran katika shambulio la kimtandao.

Mfumo wa ulinzi wa Iran ni wa hali ya juu zaidi kiteknolojia kuliko ule wa Israel, hivyo shambulio la kieletroniki dhidi ya jeshi la Israel linaweza kufikia mengi zaidi.

Kurugenzi ya Taifa ya Mtandao ya serikali ya Israeli inasema, "kiwango cha mashambulizi ya kimtandao ni cha juu kuliko hapo awali, angalau mara tatu zaidi, na kwa mashambulizi katika kila sekta ya Israel.

Ushirikiano kati ya Iran na Hezbollah (wanamgambo wa Lebanon na shirika la kisiasa) uliongezeka wakati wa vita."

Ripoti hiyo inasema kulikuwa na mashambulio 3,380 ya kimtandao kati ya mashambulizi ya Oktoba 7 na mwishoni mwa mwaka 2023.

Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Raia la Iran, Brigedia Jenerali Gholamreza Jalali, alisema Iran ilizuia karibu mashambulizi 200 ya kimtandao katika mwezi huu kuelekea uchaguzi wa bunge wa hivi karibuni.

Mwezi Disemba, Waziri wa Mafuta wa Iran, Javad Owji, alisema shambulio la kimtandao lilisababisha usumbufu mkubwa katika vituo vya mafuta.

.

Chanzo cha picha, Iranian government / Getty Images

Maelezo ya picha, Mwaka 2008, Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alitangaza kuongeza uzalishaji wa madini ya urani katika kiwanda cha nyuklia cha Natanz

Tisho la Nyuklia

Israel inadhaniwa kuwa na silaha zake za nyuklia, lakini inashikilia sera rasmi ya utata kwa makusudi.

Iran haifikiriwi kuwa na silaha za nyuklia na licha ya shutuma dhidi yake, inakanusha kuwa inajaribu kutumia mpango wake wa nyuklia wa kiraia kuwa taifa lenye silaha za nyuklia.

Kijiografia na idadi ya watu

Iran ni nchi kubwa kuliko Israel na idadi ya watu wake (karibu milioni 89) ni karibu mara tisa ya ile ya Israeli (karibu milioni 10).

Pia ina askari mara sita zaidi ya wanajeshi wa Israeli. Kuna wanajeshi 600,000 nchini Iran, wakati Israel ina wanajeshi 170,000, inasema IISS.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kombora la masafa marefu liko ufukweni mwa Bahari ya Chumvi, baada ya Iran kurusha ndege zisizokuwa na rubani na makombora kuelekea Israel siku ya Jumamosi

Je, Israel inaweza kulipiza kisasi vipi?

Mtafiti wa Mashariki ya Kati mwenye uhusiano na Chuo Kikuu cha Tel Aviv, Dkt Eric Rondsky anasema Israel ilikubali kuwajibika kwa kushindwa kutangaza hali ya tahadhari wakati Iran iliposhambulia.

Wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika nchi jirani mara kwa mara huanzisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya Israel na wanaweza kuwa walengwa.

Jeremy Binnie, Mtaalamu wa Ulinzi wa Mashariki ya Kati huko Janes, anaamini Israel haiwezi kulipiza kisasi mara moja: "Kwa kweli, wana chaguzi kadhaa ikiwa wanataka kulipiza kisasi, kama vile maeneo ya mabomu nchini Lebanon au Syria."

Binnie ana shaka kutakuwa na vita vya kawaida vya kiwango kamili. "Jeshi haliendi kupigana, jeshi la majini haliendi vitani, wao (Iran na Israel) hawako karibu.

"Tunaangalia hali ambapo pande zote mbili zina uwezo wa mashambulio ya muda mrefu dhidi ya ulinzi wa anga wa upande mwingine. Tuliona upande mmoja wa hilo na uwezo wa Iran wa mashambulizi ya masafa marefu dhidi ya ulinzi wa Israeli Jumamosi na Jumapili."

Amesema Israel italazimika kukiuka anga ya nchi huru kama Syria, Jordan na Iraq.

Israel ina huduma ya siri yenye uzoefu ambayo inaweza kufanya operesheni za siri ndani ya Iran, hata hivyo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani imeishutumu Iran kwa kuwapa silaha waasi wa Houthi wa Yemen kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani

'Kadi ya Iran'

Mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati Tariq Sulaiman ameiambia BBC Urdu kuwa kuna wanachama wanaounga mkono vita katika bunge la Israel na baraza la mawaziri ambao wanataka vita, na kumshinikiza waziri mkuu wa Israel kuchukua hatua. "Kila wakati Netanyahu anapojikuta katika hatari ya kisiasa, mara moja anatumia kadi ya Iran."

Kura ya maoni iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Israel mwezi Aprili ilibaini kuwa karibu robo tatu ya umma wa Israel wanapinga shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Iran ikiwa hatua hiyo itaathiri muungano wa usalama wa Israel na washirika wake.

Taarifa ya chuo kikuu inasema utafiti huo ulifanywa tarehe 14 na 15 Aprili kwa njia ya mtandao na simu, na ulihusisha wanaume na wanawake 1,466 wanaowakilisha watu wazima wa Israel, Wayahudi na Waarabu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Houthi waliteka nyara meli inayomilikiwa na Uingereza na Japan katika Bahari ya Shamu mnamo 19 Novemba 2023

Vita vya Israel na Iran ni vita vya aina gani?

Ingawa Israel na Iran hazijapigana vita rasmi hadi sasa, nchi zote mbili zimekuwa katika mgogoro usio rasmi.

Kundi la wanamgambo na la kisiasa la Hezbollah linapigana vita vikubwa zaidi vya wakala wa Iran dhidi ya Israel kutoka Lebanon. Iran haikatai kuliunga mkono kundi la Hezbollah.

Uungwaji mkono wake kwa Hamas katika Ukanda wa Gaza ni wa hakika. Hamas imetekeleza mashambulizi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel, na imerusha roketi kutoka Ukanda wa Gaza na kuingia katika ardhi ya Israel kwa miongo kadhaa.

Israel na mataifa ya magharibi yanaamini kuwa Iran inatoa silaha, risasi na mafunzo kwa Hamas.

.

Chanzo cha picha, Houthi militants handout / EPA

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Houthi wamekuwa wakizidisha mashambulizi dhidi ya meli katika bahari ya Shamu

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanatazamwa kama wakala mwingine wa Iran. Saudi Arabia inasema makombora ya Houthi yaliyofyatuliwa dhidi yake yalitengenezwa nchini Iran.

Makundi yanayoungwa mkono na Iran yana nguvu kubwa nchini Iraq na Syria pia. Iran inaiunga mkono serikali ya Syria na inasemekana kutumia ardhi ya Syria kwa mashambulizi dhidi ya Israel.

Ripoti ya ziada ya Ahmen Khawaja, Carla Rosch na Reza Sabeti na Chris Partridge

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na Seif Abdalla