'Unawaachia watekaji nyara wanichukue, sasa unataka kura yangu'

Aisha Mama (kushoto) alilazimika kutoroka nyumbani kwake kwenda kwa nyumba ya mama yake katika jiji la Katsina kwa sababu ya mashambulizi katika kijiji chake.

Chanzo cha picha, Nduka Orjinmo/BBC

Maelezo ya picha, Aisha Mama (kushoto) alilazimika kutoroka nyumbani kwake kwenda kwa nyumba ya mama yake katika jiji la Katsina kwa sababu ya mashambulizi katika kijiji chake.

Wanaijeria wengi wanaishi katika hofu ya mara kwa mara ya kutekwa nyara na kushikiliwa na magenge yenye silaha, hasa kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, ambako maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao. Ukosefu wa usalama unamaanisha wengi katika eneo hilo, ambalo lina idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha nchini humo, huenda wasishiriki katika uchaguzi wa tarehe 25 Februari.

Barabara hii isiyo na lami ambayo inaishia kwenye kisiki cha mti ndiyo njia pekee ya magari kuingia katika kijiji cha Bakiyawwa katika jimbo la Katsina kaskazini mwa Nigeria.

Jamii hii ya wakulima wadogo wadogo si mahali ambapo ungetarajia wahalifu wanaofanya biashara ya utekaji yara nchini Nigeria ambapo wahasiriwa wanalazimika kulipa kikombozi ili kuwanusuru jamaa zao.

Kwa hiyo haikuwa jambo la kushangaza wakati watu waliokuwa wamejihami kwa pikipiki walipovamia Septemba iliyopita na kuwateka nyara wanakijiji 57.

"Walimshikilia mke wangu kwa siku 38," alisema Abduljabara Mohammed, mtumishi wa serikali na mmoja wa wale wanaofikiriwa kuwa matajiri. Alilipa naira milioni moja sawa na (dola 2,100; £1,700) kwa ajili ya kuachiliwa kwake.

Zaradeen Musa

Chanzo cha picha, Nduka Orjinmo/BBC

Maelezo ya picha, Zaradeen Musa hakutaja alitoa kiasi gani cha pesa kwa watekaji nyara, lakini alisema ni pesa nyingi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Niliwapa pesa zangu zote na pikipiki, kisha nikawasihi wasinichukue," alisema Zaradeen Musa, 30, ambaye mlango wake ulipigwa teke mwendo wa saa 01:00 huku watu wenye silaha, wanaojulikana kama majambazi, wakiendesha shughuli zao bila kupingwa. saa nne baada ya kushinda nguvu kitengo cha polisi kilichoitwa na wanakijiji.

Maria Sani, mwenye umri wa miaka 45, alikamatwa lakini alifanikiwa kutoroka huku majambazi wakiwapeleka waathiriwa kwenye maficho yao ya msituni.

Alibaki akiwaza nini kingempata ikiwa hangetoroka kwani, kama watu wengi waliotekwa siku hiyo, asingeweza kumudu fidia.

Wale wote waliotekwa nyara hatimaye waliachiliwa lakini baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo ambayo yalisababisha walipe kwa pesa taslimu au vitu vya thamani kama vile pikipiki. Utekaji nyara huo unaonyesha ni kwa kiasi gani tatizo la utekaji nyara limeenea - hata maskini zaidi hawajasalimika.

Hata hivyo, wale wa Bakiyawwa wangejiona kuwa wenye bahati kwani mashambulizi wakati mwingine hugeuka kuwa mbaya, kama vile kuripotiwa kuuawa kwa zaidi ya wanakijiji 100 na watu wenye silaha Ijumaa iliyopita katika sehemu nyingine ya Katsina.

Makundi kama hayo yenye silaha kaskazini-magharibi na wanaotaka kujitenga kwa jeuri kusini-mashariki yanaleta vitisho vya kweli kwa uchaguzi wa Februari 25, wachambuzi wanasema.

Mashambulio dhidi ya afisi za Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inic) yalisababisha uchaguzi kusogezwa mbele kwa wiki moja mwaka wa 2019, na kuchomwa moto kwa ofisi ya INEC hivi majuzi kusini-mashariki kumezua hofu ya kuahirishwa tena, ingawa maafisa wamesema hilo halitatokea.

Mnamo Disemba, IEC ilitangaza kuwa ilikuwa hatari sana kufanya uchaguzi katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Katsina lakini haijabainika nini kitatokea siku ya uchaguzi.

Profesa wa sheria Chidi Odinkalu anahoji kuwa uchaguzi huu unaweza kukumbwa na kizungumkuti wa kisheria endapo ukosefu wa usalama utatatiza upigaji kura na mgombeaji kuamini kuwa amepoteza uungwaji mkono muhimu.

Katika siku za nyuma, watu hawakujitokeza kupiga kura kwa kuhofia huenda ghasia zikatokea katika majimbo ya kusini kama Imo, Anambra, Lagos na Rivers, lakini sasa, mgogoro wa utekaji nyara kaskazini umewaacha wengi kutovutiwa na uchaguzi.

“Unawaachia watekaji nyara wanichukue, sasa unataka kura yangu,” alisema Bi Sani kupitia mkalimani.

Kama ilivyo kwa wengi hapa awali alimpigia kura Rais Muhammadu Buhari lakini amekaa nje.

Maria Sani hana nia ya uchaguzi ujao baada ya shambulio la kijiji chake

Chanzo cha picha, NDUKA ORJIMO/BBC

Maelezo ya picha, Maria Sani hana nia ya uchaguzi ujao baada ya shambulio la kijiji chake

Rais Buhari anaondoka madaraka baada ya kuhudumu kwa mihula miwili na Bola Tinubu anawakilisha chama tawala cha All Progressives Congress (APC).

"Unawezaje kukabilia na mateso haya yote na bado upigie kura APC?" alisema Lawal Suleiman, mwanachama wa zamani wa chama lakini sasa ni sauti ya pekee kijijini akimfanyia kampeni Peter Obi wa Chama cha Labour.

Wengine wengi huko Bakiyawwa wanasema pengine wangeunga mkono chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP), ikiwa watapiga kura kabisa.

"Ikiwa Buhari hangeweza kutatua matatizo ya nchi hii, hakuna mtu mwingine anayeweza," Nana Samaila, ambaye alikimbia kijiji chake cha Batsari miaka mitatu iliyopita baada ya mashambulio ya makundi yenye silaha, aliiambia BBC.

Binti yake, Aisha Mama, pia hivi majuzi alitoroka na mumewe kutoka kijiji cha Dangyya baada ya mashambulizi ya mara kwa mara ya usiku na kulazimisha familia yake kulala katika shamba lao kwa wiki.

Bi Samaila alikuwa na matumaini makubwa kwamba Rais Buhari, mtawala wa zamani wa kijeshi ambaye anatoka Katsina, angetatua masuala mengi ya Nigeria alipompigia kura kwa mara ya kwanza mwaka 2003, lakini kama wengine wengi, sasa amekatishwa tamaa na kushindwa kwa serikali yake.

Mamia ya watoto wa shule wametekwa nyara na kuachiliwa, na gavana wa jimbo aliwahi kuwataka wakaazi kujihami dhidi ya majambazi hao ishara kwamba hana jinsi ya kukabiliana na majambazi hao.

Wagombea wakuu katika uchaguzi huo wanatambua kwamba ukosefu wa usalama, ambao unaambatana na kupanda kwa bei ya vyakula ambayo imesababisha viwango vya juu vya mfumuko wa bei, ndiyo changamoto kubwa inayokumba Nigeria kwa sasa.

Atiku Abubakar wa PDP, Bw Tinubu wa APC na Bw Obi wa Chama cha Labour wanapendekeza mageuzi katika idara ya polisi, kurekebisha jeshi na kuboreshwa kwa ustawi, miongoni mwa masuala mengine.

Mipango yao haina tofauti kubwa na kile Rais Buhari, ambaye alichaguliwa kwa ahadi ya kukabiliana na makundi ya Kiislamu kaskazini-mashariki, amefanya kwa mafanikio madogo tu.

Ingawa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti waasi wa Kiislamu, ghasia kaskazini-magharibi na kusini-mashariki zimeongezeka sana kwenye saa yake.

"Alitawanya [aliharibu] uchumi, kuna ukosefu mkubwa wa usalama," alisema Mohammed Yusuf, mkulima mwenye asili ya Katsina ambaye sasa analazimishwa kuuza chai na tambi zilizopikwa katika mitaa ya jiji kubwa la eneo hilo, Kano.

Mohammed Yusuf (kushoto) anasema atapigia kura PDP wakati huu

Chanzo cha picha, Nduka Orjimo/BBC

Maelezo ya picha, Mohammed Yusuf (kushoto) anasema atapigia kura PDP wakati huu

Kano, Katsina na Kaduna, waliopewa jina la Ks watatu, wanachukuliwa kuwa majimbo muhimu kwa yeyote anayetaka kujitokeza kama rais wa Nigeria kwa sababu ya idadi kubwa ya wapiga kura. Kuna wapiga kura wengi waliojiandikisha hapa kuliko katika majimbo matano ya kusini-mashariki.

Kambi ya Bw Buhari ya kura katika majimbo matatu ilimsaidia kushinda chaguzi mbili mfululizo, na wakati baadhi bado wataendelea kuunga mkono APC, kuna hisia kwamba chama hicho kimepoteza mwelekeo katika eneo lililokumbwa na ukosefu wa usalama.

Wiki mbili tu zilizopita, helikopta ya rais ilipurwa mawe wakati wa ziara yake mjini Kano.