Keith Davis: Mtunza bahari aliyetoweka ghafla 'pasipojulikana'

ggg

Keith Davis alitoweka baharini maelfu ya maili kutoka nyumbani. Mwili wake haujawahi kupatikana. Sasa fumbo la kifo chake limeangazia ulimwengu wa bahari ambao kwa kiasi kikubwa hauonekani, anaandika Rachel Monroe.

"Katika duka langu la vyakula huko Texas, ninaweza kununua mkebe wa tuna kwa chini ya dola moja. Lakini, kama vitu vingi vinavyoonekana kuwa vya bei rahisi, bei hizo za chini zinawezekana tu kwa sababu ya kazi hatari na isiyoonekana inayotokea mbali - kazi ambayo wengi wetu hatutawahi kujua kuihusu".

Davis, mpiga gitaa na mtu anayependa kusafiri kutoka Arizona, alifanya kazi ili kufanya ulimwengu usioonekana wa uvuvi wa samaki tuna wa bishara uonekane. Na huenda amelipia gharama yake.

"Alikuwa anajituma sana, mwenye mapenzi sana, alifanya jambo gumu bila ujuzi au uzoefu unaohitajika," Anik Clemens, rafiki yake na mfanyakazi mwenzake. "Alikuwa na shauku kubwa kwa kile alichokifanya. Alitaka kulinda bahari, alitaka kulinda wavuvi na sekta yao."

Mnamo mwaka wa 2015, katikati ya safari iliyoonekana kuwa ya kawaida kwenye Victoria 168, sehemu ya meli ya tuna inayomilikiwa na jumuiya ya Taiwan, mtu huyo mwenye umri wa miaka 41 alitoweka mamia ya maili kutoka pwani ya Ecuador.

Wafanyakazi walitafuta meli, lakini hawakupata dalili yoyote. Habari za kutoweka kwake zilipofika kwa marafiki zake na wafanyakazi wenzake bara, wengi walitilia shaka papo hapo.

"Alikuwa na miaka 16 ya utumishi wa kazi hiyo. Na hakukuwa na swali akilini mwangu kwani alikuwa mtaalamu na makini na salama kama mtu yeyote angeweza kuwa," alisema Bubba Cook, rafiki wa Davis na Meneja wa Programu ya Tuna ya Magharibi na Kati ya Pasifiki wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani WWF.

"Hitimisho lisiloweza kuepukika ni kwamba kuna jambo lilipaswa kumtokea. Hadi leo, nina hakika kwamba aliona kitu ambacho watu waliokuwa kwenye chombo hicho hawakutaka aone."

Unaweza pia kusoma

Davis alikuwa mwanabiolojia wa baharini ambaye alifanya kazi kama mwangalizi wa uvuvi, taaluma isiyojulikana sana ambayo inatoa matukio mazuri na katika hali nyingine, ni hatari kubwa.

Waangalizi wanaokadiriwa 2,500 ni macho na masikio yetu kwenye bahari. Wanaishi kwenye meli za uvuvi kwa miezi kadhaa kwa wakati mwingine, wakienda mamia ya maili nje ya pwani ili kulinda maji hayo dhidi ya uvuvi wa kupita kiasi na kukusanya uchunguzi wa kisayansi ambao hutusaidia kuelewa afya ya bahari zetu na viumbe vya baharini.

Waangalizi wanaishi miongoni mwa wafanyakazi, wakifanya kazi kwa saa zilezile za kuchosha katika hali zilezile ngumu. Lakini pia wakati mwingine hutazamwa kwa mashaka, kwa sababu sehemu ya kazi yao ni kuripoti shughuli haramu.

Lakini ni nini ambacho huenda Davis alishuhudia ambacho kingeweza kumweka hatarini?

Bahari kuu, ambako mamlaka ya kisheria ni ngumu na kuna uangalizi mdogo, inajulikana kwa shughuli haramu yaani biashara ya dawa za kulevya na silaha na hata wakati mwingine biashara ya usafirishaji binadamu.

Hata hivyo, kuweka wazi, hatujaona chochote kinachoonyesha kwamba Davis alishuhudia shughuli zozote kwenye Victoria 168.

Boti aliyokuwa akiifanyia kazi wakati wa kutoweka kwake ilikuwa inajishughulisha na kile kinachojulikana kama usafirishaji.

ggg
Maelezo ya picha, Keith Davis alikuwa anaipenda kazi yake, anasema rafiki Anik Clemens
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vyombo vya kusafirisha samaki vinatoa boti za samaki aina ya tuna na vifaa vipya na kuwasafirisha samaki wapya waliovuliwa kurudi Pwani.

Utaratibu huu umeweza kuwawezesha baadhi ya wasafirishaji wa tuna kukaa baharini kwa miaka kadhaa, ambayo inaweza kusaidia kuokoa gharama. Waangalizi wanaoshuhudia shughuli haramu wako katika hali hatarishi sana. Wakati Davis alipokuwa akifanya kazi kwenye Victoria 168, njia yake pekee ya mawasiliano hadi ufukweni ilikuwa kupitia kompyuta ya nahodha.

Watu wanaofanya kazi yake wakati mwingine hufunzwa kuzungumza kwa lugha maalumu ikiwa wataona kitu ambacho ni nyeti sana kusema kwa sauti kubwa.

Ingawa Davis alipenda kuwa mwangalizi, pia alijua sana hatari za kazi hiyo.

"Wengi wetu ambao tumehudumu tumeshuhudia shughuli za bunduki, mapigano ya visu, utumwa... mengi ambayo inabidi tuyameze kama 'sehemu ya kazi," aliandika kwenye Facebook mwaka mmoja kabla ya kutoweka.

Hata cha kushtua zaidi, kifo cha kudhaniwa cha Davis sio tukio la pekee. Idadi ya waangalizi kadhaa wametoweka au walifariki katika hali isiyoeleweka.

Kesi nyingi kati ya hizi hazionekani sana kuliko hata Davis alivyofanya. Hiyo ni kwa sababu waangalizi wengi si wanaume wasafiri wa Marekani kama Davis, lakini ni wakazi wa Visiwa vya Pasifiki wanafanya kazi ili kutunza familia zao.

Mara nyingi wanatoka katika jamii zilizo na historia dhabiti ya uvuvi - sekta ambayo, mara nyingi, imeharibiwa na uvamizi wa meli za uvuvi za utandawazi ambazo zinategemea usafirishaji.

Wakati wanaume kama Charlie Lasisi, mwangalizi kutoka Papua New Guinea, au Eritara Aati Kaierua kutoka Kiribas, walipofariki katika mazingira ya kutiliwa shaka, hawakuzungumziwa sana. Lakini ni waangalizi kama hawa ambao wanabeba mzigo mkubwa wa hamu zetu za kununua tuna kwa bei nafuu.

ggg

Mwili wa Davis bado haujapatikana. Uchunguzi wa mamlaka ya Panama na FBI haukukamilika.

"Tunaona kukosekana kwa utatuzi kuhusu kile kilichotokea kwa Keith kuwa kunasikitisha sana, hakuna kitu kingine ambacho tunaweza kufanya," mwajiri wake, MRAG Americas, alisema katika taarifa.

"Tunaendelea kujitahidi kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa waangalizi wetu waliosambazwa baharini na nchi kavu."

Kundi la Gilontas, mmiliki wa Victoria 168, amekataa kutoa maoni yake kuhusu kesi hiyo, ambayo bado iko wazi kiuhalisia na pia alibainisha kuwa "Kundi la Gilontas limeshirikiana na mamlaka zilizofanya uchunguzi".

Rasmi, hatujui ikiwa Davis alikufa kwa bahati mbaya, alijiua, au aliuawa. Lakini tunachojua ni kwamba shughuli nyingi haramu zinazofanyika baharini zinategemea wazo la kile kinachotokea mbali na Pwani, ambapo hakuna mawimbi ya simu za mkononi au kamera za usalama, kimsingi hakionekani kwa sisi wa bara.

ggg
Maelezo ya picha, Victoria 168, siku baada ya Davis kutoweka

Kazi ya waangalizi, kushuhudia kinachotokea baharini, inaweza kuwafanya wawe hatarini.

"Waangalizi hawana msaada kutoka sekta ya uvuvi. Hawana msaada kutoka kwa mashirika. Hawana msaada kutoka kwa waajiri wao, wakandarasi. Mwishoni, wako peke yao," alisema Liz Mitchell rais wa zamani wa Chama cha Waangalizi wa Kitaalam.

Bubba Cook wa WWF amekuwa akifuatilia vifo visivyoelezeka vya waangalizi kwa zaidi ya muongo mmoja. "Moja ya shida kubwa ni kwamba hatujui ni waangalizi wangapi wamepotea," alisema.

"Hapa tu katika Pasifiki, imekuwa kama mwangalizi mmoja kwa mwaka. Na hiyo ni [tangu] tu kuanza kuweka kumbukumbu. Ni wangapi kabla ya waliokufa baharini katika hali mbalimbali au hawakurudi kabisa nyumbani?"

Kwa kuzingatia hadithi kama za Keith Davis na Charlie, Eritara na kwa kujifunza kuhusu kile kinachotokea kwenye bahari kuu, tunaweza kufanya mambo kuwa salama kwa waangalizi, kwa wafanyakazi, na kwa bahari zetu.