Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kipindupindu: Ugonjwa rahisi kuupata, rahisi kuukwepa na rahisi kukuua
Yusuph Mazimu, BBC Swahili
Mjadala kuhusu ugonjwa kipindupindu umerejea tena ulimwenguni. Wtaalamu wanasema ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuua kwa masaa tu kama mgonjwa hajapata huduma inayostahili hasa kwa wale walioathirikia zaidi.
Licha ya athari kubwa za ugonjwa huo unaotapakaa kwa kasi, Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuna uhaba mkubwa wa chanjo ya ugonjwa huo duniani.
Nalo kundi la kimataifa la kuratibu usambazaji wa chanjo nyakati za dharura (ICG) limeamua kusitisha kwa muda mkakati wa utoaji wa dozi mbili za chanjo dhidi ya ugonjwa huu kutokana na hofu ya uwezekano wa uhaba wa chanjo hiyo.
Pengine hili linazifana mamlaka za serikali mbalimbali ulimwenguni kuanza kutoa tahadhari mapema ili kupunguza madhara ya vifo kwa wananchi wake.
Nchi za Tanzania na Kenya, ni miongoni mwa nchi ambazo mamlaka zake za afya hivi karibvuni zilizotoa tahadhari ya ugonjwa huo. Lakini unaujua kwa kina ugonjwa huu unaoathiri mpaka watu milioni 4 kwa mwaka na kuua maelfu ya watu duniani.
Historia na Chimbuko la ugonjwa huu
Kila ugonjwa una mahali unaanzia. Covid_19 ulianzia China, dunia nzima inajua. Kipindupindu wenyewe ulianzia bara la Asia katika nchi ya India. Janga la kwanza liliibuka karne ya 18 kwenye mkoa wa Bengal, nchini India.
Katika karne ya 19, mlipuko huu uliathiri maeneo mengi duniani, ukianzia tena kwenye delta ya Ganges au Bengal delta ambayo ndiyo delta kubwa zaidi ya mto duniani. Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO) mlipuko wa sita wa ugonjwa huu uliua mamilioni ya watu duniani.
Mlipuko wa sasa wa saba ulianzia kusini mwa Asia mwaka 1951 na kufika Afrika 1971 na bara la Amerika mwaka 1991. Ugonjwa huu unaororodheshwa kama magonjwa hatari yanaoshughulikiwa kwa dharura kutokana na athari zake za muda mfupi.
Ukubwa wa tatizo kwa sasa
Mwaka 2017, shirika hilo lilipitisha mkakati wa kukabiliana na ugonjwa huo, ukilenga kupunguza vifo vitokanavyo na kipindupindu kwa asilimia 90% ifikapo mwaka 2030.
Lakini bado vifo vinaendelea kutokea na wengi wakiathirika. Kwa sasa kinakadiriwa kuua watu mpaka 143,000 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Kituo cha Ulaya cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (ECDC), Mpaka Agosti 24, 2022, inakadiriwa kuwepo kwa visa 39,857 vya kipindupindu na vifo 114.
Afghanistan, Bangladesh, DRC, Ethiopia, Nigeria na Malawi ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Nchini Nigeria, mamlaka zinataja watu 256 wamepoteza maisha, katika kipindi cha miezi 10, wakiwemo 80 waliofariki mwezi Septemba.
Malawi inashuhudia athari zaidi, visa 4,420 vikiripotiwa tangu kuanza kwa mwaka na kuweka rekodi katika muongo mmoja uliopita, vikigharimu maisha ya watu 128.
Nchini Kenya wizara ya afya ilithibitisha visa 61 vya ugonjwa huo, huku kaunti za Kiambu, Nairobi na Kajiado zikiathirika zaidi.
Kipindupindu ni tatizo kubwa duniani na linapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari, kwa mujibu wa WHO.
Maelezo muhimu kuhusu kipindu pindu
1. Kinasababisha na nini?
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya vibrio cholera kwenye utumbo mwembamba, ambaye hutoa sumu inayosababisha kutolewa kwa maji mengi ndani ya utumbo, kwa njia ya kuhara, wakati mwingine kutapika na homa kali.
Bakteria huyu anapatikana katika chakula au maji machafu na kinyesi kutoka mtu aliye na maambukizi. Kwa ujumla unaweza kuambukizwa kupitia maji machafu, mboga zilizopandwa kwenye maji taka¸ samaki na dagaa waliovuliwa kwenye maji machafu, vyakula na vinywaji vilivyo na bakteria huyu kutokana na uchafu
Daktari mwandamizi kutoka Hospitali ya taifa ya Kenyatta nchini Kenya, William Sigilai aameiambia BBC kuhusu sababu za mlipuko wa sasa akiasi pia yanayoendelea nchini kwake, ‘ugonjwa huu umechochewa na hali ya sasa ya kiangazi , ukosefu wa maji safi ya kunywa, kunawa mikono, na pia kuishi kwa watu wengi katika mazingira duni yasiyokuwa na maji safi tiririka na pia sehemu isiyokuwa na mbiundo mbinu msingi muafaka ya vyoo’.
2. Dalili za kipindipindiu
Dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni chache na ni rahisi kwa mtu kuweza kuzibaini na zinaweza kuonekana ndani ya masaa machache au siku tano baada ya maumbukizi. Dalili hizo ni:
- Kuharisha maji maji yanayofanana na maji ya mchele
- Kutapika
- Kujisikia mlegevu, kukosa nguvu
- Wakati mwingine kusikia maumivu ya misuli
- Upungufu wa maji mwilini
- Kuna wakati mgonjwa anakuwa na ngozi iliosinyaa na mdomo kukauka
Inakisiwa kwamba karibu asilimi 10 tu ya watu wanaoambukizwa kipindipindu ndio wanaonyesha dalili za ugonjwa huo, lakini wengi hawaonyeshi na wengine hawajui.
Lakini Dokta William anasisitiza ‘watu wengi wanaooambukizwa na kipindupindu hawataonyesha dalili zotezote, lakini ni muhimu kwamba watambue (hizo dalilia) na wachukue hatua haraka iwezekanavyo’.
Hatua hizo zinazoshauriwa na wataalamu ni pamoja na kunywa ama kumpa maji (ORS) mgonjwa aliyeonyesha dalili mkiwa bado nyumbani.
‘Maji haya ya ORS ni mchanganyiko wa chumi na sukari na lita maji ya maji’ yanaweza kurudisha maji mwilini haraka’, hasa kwa watoto na wazee wanaoshindwa kuhimili hali a kupoteza maji mengi mwilini.
3. Namna ya kujilinda, kudhibiti na tiba ya kipindupindu
Kwakuwa ni ugonjwa unaohusishwa na mazingira duni ya uchafu, wataalamu wanapendekeza uzingatiwaji wa usafi kama hatua muhimu ya kwanza ya jamii kuchukua
‘Hatua muhimu zaidi ya kudhibiti au kuzuia kipindupindu ni kuimarisha hatua za upatikani wa maji, kunawa mikono kila wakati, na pia kusaidia jamii kupata maji safi’, anasema Dokta Sigilai.
Unywaji wa maji safi, maji yaliyochemshwa, kuepuka vakula vya mtaani, vinavyopikwa na kutaarishwa katika mazingira duni ya usafi, inaweza kukusaidia
Japo inaawathiri watu wengin, kipindupindu kinaepukika kwa kuwahi hospitali mara unapohisi dalili zozote. Wengi wanaolazwa kwa sababu ya kupungukiwa zaidi maji, hutibiwa kwa kuongezewa maji kwenye mishipa.