Je, Urusi inawahadaa raia wa kigeni kupigana Ukraine?

    • Author, Gurpreet Singh Chawla, Balla Satish & Oleg Boldyrev
    • Nafasi, BBC Punjabi, BBC Telugu & BBC Russian
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mohammed Asfan alikuwa amebeba matumaini na ndoto za familia yake pamoja naye alipoondoka katika mji wa kusini mwa India wa Hyderabad kuelekea Urusi.

Msimamizi wa duka la nguo alidhani angeenda kufanya kazi kama "msaidizi wa kijeshi".

Alikuwa ameona chapisho kwenye tovuti ya YouTube likiahidi kazi inayolipwa sana ya Rupia za India 100,000 (dola 1,207) kwa mwezi. Na baada ya miezi sita, angepata makazi ya kudumu.

"Hangetumwa kwenye mstari wa mbele na Ukraine, na angekuwa akifanya kazi katika makao makuu ya jeshi kama msaidizi," kaka yake Imran aliambia BBC.

Alisema Asfan aliwapigia simu kutoka mpaka wa Ukrain na kusema kuwa paspoti yake imechukuliwa, na alikuwa analazimishwa kupigana.

Imran hakusikia chochote kutoka kwa kaka yake kwa zaidi ya miezi miwili. Alipopiga simu kwa ubalozi wa India nchini Urusi kuuliza kuhusu Asfan, walimwambia kwamba alikuwa amefariki.

Asfan aliacha mke na watoto wawili, wote wakiwa chini ya miaka miwili.

Angalau wanaume wawili wa Kihindi ambao walikwenda Urusi wakitarajia kufanya kazi kama "wasaidizi" katika jeshi wamekufa walipokuwa wakipigana mbele ya vita hivi karibuni, kwa mjibu wa familia zao.

Video sawia ya kuajiriwa kwenye YouTube ilimvutia Hemil Mangukiya, mwenye umri wa miaka 23, hadi Urusi mnamo Desemba.

"Hemil aliambiwa atafanya kazi kama msaidizi katika jeshi na angefunzwa kwa miezi mitatu," kwa mujibu wa baba kutoka jimbo la Gujarat magharibi mwa India.

"Lakini baada ya kufika Urusi, aligundua kuwa alikuwa akifunzwa kupigana."

'Mtandao mkubwa wa biashara haramu ya binadamu'

Hivi majuzi India ilitangaza kwamba ilifichua "mtandao mkubwa wa biashara ya magendo ya watu" ambao uliwavutia vijana kwenda Urusi kwa ahadi ya ajira ili tu kuwalazimisha kupigana huko Ukraine.

Takriban wanaume 35 wametumwa nchini Urusi katika mpango huo hadi sasa, kwa mujibu wa Ofisi Kuu ya Upelelezi.

Wizara ya mambo ya nje ilisema kwamba kila kisa cha Wahindi kudanganywa katika vita hivyo "imechukuliwa kwa umakini mkubwa" na Moscow.

Video kadhaa za wanaume wanaoelezea masaibu yao zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika moja iliyosambazwa mwezi huu, ilionyesha kundi la wanaume saba waliomba usaidizi wa serikali ya India kurejea nyumbani, wakisema walisafiri hadi Urusi kwa visa vya kitalii lakini sasa wanalazimishwa kuhudumu katika jeshi lake.

Familia nyingine za Punjab ziliambia BBC kwamba watoto wao walikwenda Dubai kwa viza ya kitalii au walisafiri hadi Belarus kabla ya kufika Urusi baada ya kujipata katika kashfa hiyo.

Video za wanaume hao wakieleza jinsi walivyohadaiwa na maajenti wakiahidi kulipwa mishahara minono na kutumwa kwenye uwanja wa vita zimeshangaza familia zao, ambao wengi wao hufanya kazi kama madereva wa tuk-tuk au wauzaji chai.

Waathiriwa na familia wanadai kwamba maajenti walidai rupia 300,000 (dola 3,621) kwa safari hiyo, na kuahidi pasipoti ya Urusi baada ya miezi michache ya huduma ya jeshi.

Gagandeep Singh is one of the men making the appeal.

He was told to serve in the Russian army or be sentenced to 10 years in jail, according to his mother Balwinder Kaur.

"We wait until late at night for any message or phone call from our son," she told BBC Punjabi. “He says they are being sent to the front in the Ukraine war. We are all very upset.”

Other Punjabi families told the BBC that their children went to Dubai on tourist visas or travelled to Belarus – before reaching Russia -- after getting caught up in the scam.

Videos of the men explaining how they were tricked by agents promising high salaries and sent to the battlefield have shocked their families, who mostly work as tuk-tuk drivers or tea-sellers.

Victims and families allege that agents demanded 300,000 rupees ($3,621) for the trip, promising a Russian passport after a few months of army service.

Karibu raia 254 wa kigeni waluawa

Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anakadiria kuwa vita vya Ukraine vimeigharimu Urusi wanajeshi 350,000 bila kutaja idadi ya waliofariki au kujeruhiwa.

Idhaa ya Kirusi ya BBC imethibitisha kuwa wanajeshi 46,678 wamefariki. Muktadha huu unaelezea kwa nini vikosi vya jeshi la Urusi vinazidi kugeukia raia wa kigeni ili kujiimarisha.

Mnamo 2022, raia wa kigeni ambao walikuwa wametia saini mkataba wa angalau mwaka mmoja na Wizara ya Ulinzi na wakapigana kwa miezi sita, walipewa haki ya kuomba uraia wa Urusi bila hitaji la kushikilia kibali cha makazi au kuishi nchini Urusi kwa miaka mitano iliyopita.

Mnamo Januari, Rais Putin alitia saini amri mpya ya kurahisisha zaidi utaratibu huo.

Wapiganaji wengi wa kigeni ni wahamiaji wanaotafuta riziki, ambao wengi wao wanatoka nchi za Asia ya Kati, hasa Uzbekistan, Tajikistan na Kyrgyzstan.

Raia wa kigeni wanaopigania Urusi pia wanajumuisha raia wa Cuba, Nepal, India, Syria, Iraq, Serbia, Afghanistan, Somalia, Sri Lanka na Malaysia. Idadi yao inakadiriwa kuwa maelfu.

Kufikia mwisho wa Desemba 2023, takriban wageni 254 waliopigana katika jeshi la Urusi walikuwa wameuawa, kulingana na takwimu zilizojumuishwa na BBC Russian.

Mnamo Desemba, Nepal iliomba Urusi iwarudishe mamluki rai wan chi hiyo baada ya sita kati yao kufa kwenye mapigano nchini Ukraine.

Walanguzi hao wanadaiwa kutoza kila mtu hadi dola 9,000 ili kuingia Urusi kwa viza ya watalii, kwa mujibu wa polisi wa Kathmandu.

BBC imethibitisha kuwa wahamiaji wanaoshikiliwa nchini Urusi kwa makosa ya viza pia wako hatarini.

Siku chache tu baada ya raia ya kigeni kuzuiliwa kwenye mpaka wa Urusi na Finland kwa kukiuka sheria za uhamiaji Novemba mwaka jana, walihamishwa hadi kambi ya kijeshi kwenye mpaka na Ukraine.

Awad, sio jina lake halisi, anatoka Somalia na yuko katika umri wa miaka ya 40.

Alikamatwa katikati ya mwezi Novemba, akatozwa faini ya rubles 2,000 (dola 22) na kuzuiliwa akisubiri kufukuzwa, utaratibu wa kawaida kwa mtu yeyote asiye na visa sahihi.

Awad anasisitiza kwamba alidanganywa kujiandikisha kwa jeshi la Urusi. Utetezi wake unategemea ukweli kwamba hakuelewa kikamilifu ofa aliyopewa.

Bado yuko kizuizini akisubiri kufukuzwa nchini na hakuna tarehe ya kusikilizwa kesi yake iliyowekwa.

BBC iliuliza wizara ya mambo ya ndani ya Urusi kwa maoni yake kuhusu madai kwamba wafungwa wa kigeni walikuwa wanapewa kandarasi za jeshi ili waachiliwe lakini hawakupata jibu.