Malkia Elizabeth II: Kitakachofanyika siku chache zijazo

Hatua ya kwanza ya safari ya mwisho ya mwili wa Malkia Elizabeth itaanza baadaye jeneza lake litakapohamishwa kutoka Balmoral na kusafrishwa hadi Edinburgh.

Wacha tuangazie kitakachofanyika katika siku zijazo.

Jumapili

Mwili wa Malkia utaondoka Balmoral, ukisafiri zaidi ya maili 175 kupitia miji ya Perth, Aberdeen na Dundee kabla ya kuwasili kwenye Ikulu ya Holyroodhouse.

Jumatatu

Alasiri, jeneza la Malkia litasafiri kwa maandamano hadi Kanisa kuu la St Giles, likisindikizwa na Mfalme na washiriki wa Familia ya Kifalme.

Jumanne

Bintimfalme Anne ataandamana na jeneza la mama yake kwenye ndege kuelekea London. Kutoka hapo litasafiri hadi Buckingham Palace, na kushuhudiwa na Mfalme Charles na Malkia Consort, Camilla.

Jumatano

Jeneza litachukuliwa kwa maandamano katikati mwa London, na kisha litawekwa Ukumbi wa Westminster ili kuuaga mwili. Hafla hiyo ya kuuaga mwili itachukua siku nne zijazo.

Jumatatu 19 Septemba

Siku ya Jumatatu asubuhi hafla ya kuuaga mwili wa Malkia itamitimishwa, na jeneza litachukuliwa kwa maandamano hadi Westminster Abbey kwa mazishi ya serikali, siku am bayo itakuwa ya mapumziko nchini Uingereza.

Malkia Elizabeth II, aliyehudumu muda mrefu zaidi nchini Uingereza, alifariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70.

Familia yake ilikusanyika katika Jumba lake la Uskochi baada ya wasiwasi kuongezeka juu ya afya yake mapema Alhamisi.

Malkia alishika kiti cha ufalme mnamo 1952 na alishuhudia mabadiliko makubwa ya kijamii. 

Kutokana na kifo chake, mwanawe wa kwanza Charles, mwanamfalme wa zamani Wales ataongoza nchi kwa maombolezo kama Mfalme mpya na mkuu wa nchi kwa milki 14 za Jumuiya ya Madola.