Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hivi ndivyo nyumba zinavyoibiwa Canada
Wenza kutoka Canada waligundua hivi majuzi kwamba nyumba yao iliuzwa na wadanganyifu bila idhini yao walipokuwa nje ya mji. Wataalamu wanasema wizi wa aina hii ni nadra, lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la visa kama hivyo katika jiji lenye watu wengi zaidi nchini.
Mapema mwaka huu, polisi wa Toronto walisema walitaka usaidizi wa umma katika kuwanasa watu wawili ambao walihusika katika mpango tata wa ulaghai.
Watu hao, kwa mujibu wa polisi, walikuwa wametumia vitambulisho bandia kujifanya wamiliki wa nyumba katika jiji hilo. Kisha walifanikiwa kuuza nyumba hiyo, na kuwapa funguo wamiliki wapya ambao hawakuwa na wasiwasi.
Wamiliki halisi wa nyumba hiyo, wakati huo huo, walikuwa nje ya nchi kikazi tangu Januari 2022.
Wanandoa hao wanaoishi nje kidogo ya mji waligundua tu kwamba nyumba yao ilikuwa imeuzwa bila wao kujua ikiwa ni miezi kadhaa baadaye.
Tukio hilo lilivutia hisia za watu wengi nchini Canada, haswa katika eneo la Greater Toronto Area na Vancouver, ambapo mali isiyohamishika inaonekana kuwa mzigo kwa watu na kuanishwa kama chuki ya kitaifa kwa sababu ya gharama yake ya juu - wastani wa gharama ya nyumba ni zaidi ya C$1m sawa na dola $749,000 - kuna uhaba wa makazi.
Simulizi kama hizo kutoka kwa wamiliki wengine wa mali huko Toronto zimeibuka, na wachunguzi wanasema visa hivi vya mara moja vya ulaghai wa umiliki wa mali vinaonekana kuongezeka.
Kwa maveterani wa tasnia, aina hizi za kesi "ni za kipekee kwa wakati huu," alisema Trevor Koot, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Mali isiyohamishika ya Briteni, ambaye amekuwa kwenye biashara hiyo kwa karibu miaka 20.
"Ningesema sijawahi kuona kitu kama hicho," alisema, haswa linapokuja suala la kiwango cha kisasa kinachotumika kutekeleza uhalifu huu.
Wizi huu unafanyikaje hasa?
Wanaolaghai na kuiba nyumba hizi wanachokifanya ni kutumia hati za kitambulisho feki. Wtaatafuta nyumba ambazo ziko wazi labda mwenye nyumba kasafiri ama nyumba ambazo ziliwekwa rehani inayokaribia kwisha ama iliyokwisha.
Ulaghai wa hatimiliki, unavyofanyika kwa upande mwingine, unahusisha wapangaji wa nyumba isiyo na watu wanaojifanya wamiliki ama mmiliki na kuiuza nyumba hiyo kwa wanunuzi waaminifu. Hii inasababisha uhamisho wa jumla wa hatimiliki ya mali.
Mara nyingi, mmiliki halisi na mnunuzi wa nyumba wanaweza kurejeshewa pesa zao kwa kiasi kikubwa kama nyumba itakuwa imekatiwa bima ya hatimiliki. Bima husaidia kuanzisha upya umiliki na kugharamia ada za kisheria zinazotozwa wakati wa mchakato.
Bwana King alisema ameona ulaghai wa aina hii ukiongezeka mara kwa mara tangu 2020.
Mmoja wa wateja wake, Bw King alisema, walikuwa wanandoa ambao walihamia Uingereza kufanya kazi kutoka Toronto mnamo 2018. Nyumba yao huko Canada iliuzwa bila wao kujua mnamo 2022.
Iliuzwa kwa C$1.7m na ilikuwa imekarabatiwa kabisa walipogundua kuwa ilikuwa imeibiwa Juni mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, bado wanandoa hao wanahaha kurejesha majina yao kwenye umiliki wa nyumba hiyo.
Kwa nini ripoti za utapeli huu wa umiliki wa nyumba zinongezeka
Wataalam wanashangaa kwa nini kumekuwa na ongezeko la kesi zilizoripotiwa, haswa huko Toronto.
Bwana King alisema inawezekana kwamba mikataba ya mali isiyohamishika wakati wa janga inaweza kuwa ngumu zaidi kugundua hati za kitambulisho bandia.
Wakati wa Corona, aliongezea, ilimewalazimu watu wengine kukaa mbali na nyumba zao kwa muda mrefu kwa sababu ya vizuizi vya kusafiri.
Wengine wameelezea kuongezeka kwa hali ya juu ya wahalifu - ambao baadhi yao wamehusishwa na uhalifu wa kupangwa - ambao wanaonekana kufahamu vyema mfumo wa mali isiyohamishika wa Canada.
Bw Rider aliongeza kuwa vitambulisho vya ulaghai vinavyotumiwa katika shughuli hizi mara nyingi huonekana kuwa halisi, na wahusika wataajiri watendaji wenye ujuzi kujifanya wamiliki wa nyumba na kutekeleza mpango huo.
"Vitambulisho ni rahisi kughushi sasa hivi kwamba haviwezi kutegemewa kama njia pekee ya kuingia mkataba wa mali ya kama C$3m," Bw Rider alisema.
Pia kuna asili ya faida ya uhalifu huu. Mali isiyohamishika huko Toronto zimepanda thamani kwa kiasi kikubwa katika miongo michache iliyopita - wastani wa nyumba mnamo 1996 uligharimu C $198,150. Mwaka jana, ilikuwa C$1.18m.
"Inaleta maana kuna mkazo mkubwa ambapo mali isiyohamishika ni ya thamani," alisema Ron Usher, mshauri mkuu wa Society of Notaries Public katika British Columbia.
Lakini Bw Usher alionya kidogo kinachojulikana kuhusu visa hivi vilivyoripotiwa vya ulaghai wa hatimiliki, ambao mara nyingi huwa tata.
"Uhalifu huu si rahisi kufanya, na mara nyingi hukamatwa na mara nyingi hukomeshwa."
Yeye na wengine wametaka uchunguzi wa kitaifa kubaini sababu za msingi na ikiwa zaidi inaweza kufanywa ili kuwalinda wamiliki wa nyumba nchini Canada.