Mawakili wafungua kesi kupinga vipengele vya mkataba wa uboreshaji wa bandari Tanzania

Chanzo cha picha, Reuters
Sakata la uwekezaji bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World hatimaye limefika mahakamani leo jijini Mbeya nyanda za juu Kusini mwa Tanzania.
Kesi hiyo inayoongozwa na mawakili Boniface Mwabukusi na Philipo Mwakilima, imefunguliwa kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.
Kesi hiyo namba 05/2023 inawahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge.
Hapo awali nimezungumza na wakili aliyepeleka kesi hii mahakamani Boniface Mwabukusi na kwanza anaanza kwa kuelezea hoja ya msingi ya kesi hii ni ipi haswa?









