Shule ambapo wanafunzi wanabuni sheria na hata kuwaajiri waalimu

f

Chanzo cha picha, MECCHAI PATTANA SCHOOL

Maelezo ya picha, Shule ya Bamboo ni mpango wa kibinafsi ambao unalenga kufundisha wanafunzi kuwa 'watu bora'.

Wakati wanafunzi 150 katika shule ya bweni ya Mecchai Pattana iliyopo nchini Thailand, wanapomaliza kula, husimama kwenye foleni moja ndefu kwa ajili ya kuosha vyombo – na kila mmoja hulazimika kujioshea sahani yake.

Kwa kawaida, wanafunzi wawili wenye umri mkubwa (mmoja mvulana na mwingine msichana) – huwasimamia wenzao kuhakikisha kwamba wamesafisha masahani yao vyema, alibaini mwandishi wa BBC William Kremer anayeandaa kipindi cha Fixing the Wolrd alipotembelea shule hiyo.

Kulingana na Kremer, wasimamizi huwa wakali wakati mwingine.

‘Mvulana anaonekana akiwaamrishwa wanafunzi wote walio kwenye foleni yake kurejea na kuosha sahani yao upya. Baadhi ya wanafunzi wanacheka, huku wengine wakilalamika,’ ‘Aaneleza kremer akiwa ndani ya shule hiiambapo mambo yanafanyika tofauti.

Unaweza pia kusoma:

"Shule ina kamati ndogo 10, na wanafunzi wanaweza kuchagua kujiunga na yoyote inayowavutia," anasema Kramer, "ikiwa ni pamoja na kamati ya nidhamu, kamati ya kukuza mboga na kamati ya ununuzi."

'Watu wazuri na wenye heshima'

f

Chanzo cha picha, MECCHAI PATTANA SCHOOL

Maelezo ya picha, Shuleni, kazi zote za kila siku hufanywa na wanafunzi.

Shule ya Bamboo ilibuniwa na mwanaharakati na mwanasiasa mstaafu wa Thailand Mecchai Viravaidya, anayejulikana pia kama "mfalme wa kondomu" nchini Thailand.

Viravaidya alipata umaarufu nchini miaka ya 1970 na kampeni zake za kuhimiza matumizi ya kondomu nchini, ambao viwango vyao vya kuzaliwa vilikuwa vikiongezeka huku kukiwa na umaskini uliokithiri.

Taifa ambalo pia lilikuwa likishuhudia jinsi janga la VVU/UKIMWI lilivyoanza kuenea kwa kasi.

Kwa miaka mingi, alijitolea kusafiri kupitia watu maskini zaidi katika Asia ya Kusini-mashariki, akicheza michezo na michezo ya aina mbalimbali ili watu wahusishe kondomu na furaha.

Wazo lake lilikuwa kwamba, kwa kuwafahamisha watu na kondomu, kondomu ingegeuka kuwa bidhaa nyingine kwenye kikapu cha ununuzi, kama vile dawa ya meno au sabuni:

"Kama naweza kufanya hivyo, kuzijaza au kuzijaza maji (kondomu), nitafanya hivyo!"

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kampeni za Viravaidya zilikuwa kuhusu kuhalalisha matumizi ya kondomu katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Kampeni za Viravaidya zilikuwa kuhusu kuhalalisha matumizi ya kondomu katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Akiwa na uhakika wa umuhimu wa elimu kama chombo cha maendeleo, miaka 15 iliyopita Viravaidya alianzisha shule ya Mecchai Pattana akiwa na lengo lililo wazi:

"Tunataka watu binafsi wanaojua jinsi ya kuwa watu wazuri, wenye heshima, waaminifu, walio tayari kushiriki na wanaojua jinsi ya kutatua matatizo."

"Ninaamini kuwa shule hazifanyi kile wanachopaswa kufanya ili kutoa mafunzo kwa watu wazuri na wenye heshima: haitoshi kujua kusoma na kuandika, kufaulu mitihani, kuwa na udaktari", anaongeza.

Akiwa na umri wa miaka 83, Viravaidya anaendelea kujihusisha kwa karibu na shule na, kupitia shirika la hisani, hutoa fedha zinazohitajika kwa ajili ya uendeshaji wake.

Kubadilisha mfumo

f

Chanzo cha picha, MECCHAI PATTANA SCHOOL

Maelezo ya picha, Huduma kwa jamii ni sehemu muhimu ya itikadi ya shule ya Bamboo

"Shule hii inaweza kuwa ya kawaida kabisa katika baadhi ya vipengele, lakini yenye msimamo mkali katika vingine," anaelezea William Kremer, mwandishi wa BBC.

"Kwa mfano, shule inafuata mtaala wa kitaifa wa Thai, na wahitimu wote hufanya mitihani ya kitaifa. Wakati huo huo, kila mwanafunzi anapaswa kufanya masaa 2 ya huduma ya jamii kwa wiki."

Wazo hili la huduma ya jamii ni sehemu ya msingi sana ya shule ya mianzi kwamba ikiwa mwanafunzi atakubaliwa katika taasisi hiyo, malipo ambayo wazazi wao wanapaswa kufanya hayatakuwa ya pesa. Badala yake, wanapaswa kukamilisha saa 400 za huduma ya jamii na kupanda miti 400 kwa mwaka.

Lakini dhana ambayo bila shaka ndiyo yenye msimamo mkali zaidi ni kwamba wanafunzi wanapaswa "kuendesha" shule yao wenyewe, anasema Kremer.

"Unaweza kufikiria kuwa kuuliza watoto kuendesha shule ni sawa na kuwauliza wafungwa kuendesha gereza: machafuko yatatawala hatimaye."

f

Chanzo cha picha, MECCHAI PATTANA SCHOOL

Maelezo ya picha, Maagizo ya shule hutolewa kupitia kamati ndogo

"Lakini Shule ya Bamboo ni haina machafuko. Ni mahali tulivu na penye mpangilio sana, ambapo wanafunzi wana busara na kwa ujumla huingia darasani. Na silaha yake ya siri ni nguvu ya chombo hiki: kamati ndogo."

Kila kamati ndogo kati ya 10 ambazo wanafunzi wako sehemu yake hufanya maamuzi kuhusiana na majukumu tofauti ambayo uongozi wa shule unahitaji, ikiwa ni pamoja na masuala ya msingi kama vile kuwaadhibu wanafunzi wengine, kuainisha bajeti na kuamua nani anakubalika katika taasisi.

Na ingawa maamuzi yote ya kamati ndogo lazima yaidhinishwe na bodi ya shule, cha muhimu ni kuwapa wanafunzi sauti katika masuala yanayowahusu moja kwa moja, kama vile ubora wa walimu au huduma zinazotolewa na taasisi.

"Au sivyo itakuwa kama kwenda kwenye mkahawa na kutoweza kusema chochote kuhusu ubora wa chakula," anaeleza Viravaidya.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed & Dinah Gahamanyi