Wafahamu 'vigogo' wa Idara za ujasusi wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani

Wataalamu wa usalama wanapozungumza kuhusu kulinda nchi, kipaumbele chao cha kwanza ni kuwa na wakala Shirika imara wa kijasusi. Ndio maana nchi zote duniani hutumia pesa nyingi zaidi kuyawezesha kisasa na kuimarisha uwezo wa mashirika haya ya Kijasusi.

Ujasusi ndio kiini cha kila nchi na ujasusi wake wa nje na wa ndani unazingatia masilahi na usalama wa kitaifa.

Shirika la Kitaifa la Ujasusi ndilo ulinzi wa kwanza wa taifa unaweza kusema usalama wa taifa, na ndilo shirika linalohusika na kupata taarifa za siri, na dhana za udukuzi zinazofanywa na nchi, lakini si nchi zote zinazoweza kuwa na nguvu sawa za kiuchumi na kijasusi.

Marais wanapochagua wakuu wa kijasusi wa kitaifa huzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uzoefu binafsi pamoja na uaminifu na ushirikiano kati ya rais na mteule wake. Katika ripoti hii, tunaangazia kwa karibu wakuu wa taasisi ama mashirika matano ya kijasusi wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani.

Mkurugenzi wa CIA Marekani

Mkurugenzi wa sasa wa CIA ni William Burns. Kabla ya kuteuliwa Januari 2021, Bwana Burns alikuwa mwanadiplomasia kwa miaka 30 ambaye alihudumu katika nchi kadhaa.

Bw. Burns alikuwa mwanadiplomasia aliyeongoza mazungumzo na Iran wakati wa utawala wa Obama yaliyofikia makubaliano ya kihistoria kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran mwaka 2015.

Bwana Burns kwa muda mrefu amekuwa mshirika wa karibu wa Rais Biden kutokana na uteuzi wake.

Viongozi hao wawili walifanya kazi kwa karibu wakati wa Bw Biden kama makamu wa rais wa Obama na pia katika Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni.

Bw Burns aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya nje chini ya Rais wa zamani Barack Obama, balozi katika nchi za Urusi na Jordan, na naibu waziri wa mambo ya nje wa maswala ya mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa MI5 wa ujasusi wa Uingereza

Ken McCallum ni mkurugenzi mkuu wa idara ya ujasusi ya MI5 ya Uingereza na ameshikilia wadhifa huo kwa miaka mingi.

Yeye ndiye mkurugenzi wa 18 wa MI5 tangu kuanzishwa kwake mnamo 1909.

Ken McCallum amekuwa na idara ya ujasusi ya Uingereza kwa zaidi ya miaka 20 ambayo ina maana kwamba ana uzoefu mkubwa katika masuala ya kijasusi.

Alikuwa mmoja wa maafisa walioshtakiwa kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi kaskazini mwa Ireland na vile vile uchunguzi wa michezo ya Olimpiki ya London ya 2012.

Mnamo 2018, McCallum aliongoza uchunguzi kuhusu majibu ya MI5 kwa jaribio la mauaji la Sergei Skripal.

Mkuu wa FSB ya Urusi

Alexander Bortnikov, mkuu wa sasa wa Usalama wa Urusi (FSB). Bortnikov ametumikia kwa muda mrefu katika huduma ya ujasusi ya Urusi katika nyadhifa mbalimbali.

Ni mmoja wa watu wa karibu sana na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Alihitimu kutoka Taasisi ya Wahandisi wa Reli ya Leningrad mnamo 1973 akitunukiwa shahada ya uhandisi.

Alijiunga na huduma ya ujasusi ya Soviet, KGB mnamo 1975, na ilikuwa mwanzo wa kazi yake ya ujasusi. Ripoti zinasema yeye na Putin walikutana kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1970.

Mkuu wa ujasusi wa Uturuki MIT

Idara ya ujasusi ya Uturuki inaongozwa na Hakan Fidan, mshirika wa karibu wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Bw Fidan alisomea sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Maryland.

Pia alikuwa afisa mdogo katika jeshi la Uturuki kuanzia 1986 hadi 2001 alipostaafu. Hakan Fidan alikuwa mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo la Uturuki kutoka 2003 hadi 2007.

Hakan Fidan kwa sasa anaelezewa kuwa "mtu mwenye nguvu sana" na mtu wa mkono wa kulia wa Rais Erdogan.

Shirika la kijasusi la Israel Mossad

David Barnea ni mkuu wa Mossad, shirika la kijasusi lenye nguvu zaidi la Israel.

Barnea alihitimu kutoka chuo cha kijeshi huko Tel Aviv mnamo 1983, na baadaye akaenda Merika kusoma katika Taasisi ya Teknolojia ya New York.

David Barnea alijiunga na Mossad ya Israel mwaka 1996 kwa mafunzo.

Asili ya David Barnea katika kujiunga na ujasusi wa Israeli inaonekana kuwa ilichaguliwa kwa msingi wa uzoefu wake katika uwanja huu.