Ilikuwaje mbwa wakawa 'marafiki zetu wa karibu'?

Uhusiano wetu na mbwa unaturudisha nyuma sana.

Waulize tu wanaakiolojia ambao wamebaini kwamba binadamu walikuwa tayari wanazika mbwa pamoja na wamiliki wao kabla ya miaka 14,000 iliyopita.

Lakini asili ya uhusiano wetu na mbwa bado ni chanzo cha mjadala mkubwa, licha ya ushahidi mwingi kwamba mbwa walikuwa wanyama wa kwanza kuwahi kufugwa na binadamu.

Hadithi za asili

Kuna nadharia mbili kuu zinazoshindana kuhusu jinsi muungano wa binadamu na mbwa ulianza kwa mara ya kwanza kati ya miaka 15,000 na 40,000 iliyopita huko Ulaya au Asia.

Nadharia ya kuasili spishi-tofauti inaeleza kwamba kwa bahati mbaya tulifuga mbwa mwitu wa kijivu hapo kale na mababu zetu waliwatunza mbwa aina zote ila walipenda kuwalea na mbwa wadogo wa mbwa.

Nadharia ya commensalism inasisitiza kwamba mbwa mwitu kimsingi walijitunza wenyewe kwa kuzunguka makazi ya watu kutafuta mabaki ya chakula kilichotupwa.

Mtetezi mmoja wa hoja hii ya pili ni Krishna Veeramah wa Chuo Kikuu cha Stony Brook huko New York.

''Wale mbwa mwitu ambao walikuwa wastaarabu na wasio na fujo walifanikiwa zaidi katika hili," alieleza.

"Ingawa wanadamu hawakupata manufaa ya aina yoyote kutoka kwa mchakato huu kwa muda, wangekuwa na aina fulani ya uhusiano wa karibu na wanyama hawa, hatimaye kugeuka kuwa mbwa tunaowaona leo."

Pat Shipman, profesa mstaafu wa Anthropolojia na mtaalamu katika historia ya mwingiliano wa binadamu na wanyama, anasema kwamba uhusiano wenye nguvu kisha ukastawi kati ya spishi ambazo hapo awali hazikuwa na hamu ya kuheshimiana katika kati ya kila mmoja wao.

"Tunapofikiria uvumbuzi wote ambao tumeunda na njia za mkato ambazo tumechukua ili kuweza kufuga wanyama ni mfano wa ajabu."

"Lakini kufuga mbwa mwitu halikuwa jambo la kawaida. Sio tu kwamba walikuwa hatari, lakini pia walishindania rasilimali na wanadamu," Shipman anaongeza.

Shipman even proposed in her recently released book Our Oldest Companions that the collaboration with dogs was one of the reasons that could explain how homo sapiens prevailed over the Neanderthals, our closest known relatives.

Profesa huyo mstaafu anaeleza kwamba mbwa-mwitu na wanadamu hatimaye waliona manufaa ya pande zote za ushirikiano - kwa wanadamu, mbwa mwitu wakawa walinzi muhimu dhidi ya maadui na vilevile washirika wa kuwinda ambao hutoa mkono wa kusaidia katika kutafuta wanyama wakubwa.

Kama vile akiolojia inavyoonesha, mbwa mwitu/mbwa wakawa wanafamilia wa karibu wa familia ya binadamu - pamoja na maeneo ya mazishi, kuna michoro ya mapango ya kabla ya historia inayowaonesha kwa njia kama ya kipenzi.

Shipman hata alipendekeza katika kitabu chake cha Our Oldest Companions kilichotolewa hivi majuzi kwamba ushirikiano na mbwa ulikuwa mojawapo ya sababu zinazoweza kueleza jinsi homo sapiens walivyoshinda Neanderthals.

"Muungano wa mbwa mwitu wa binadamu ulitawala msururu wa chakula," anaamini hivyo.

Nadharia ya kuvutia hivi karibuni imepata msukumo mwingine: katika utafiti uliochapishwa mwishoni mwa Desemba, watafiti walieleza kuwa wawindaji waliwagawia mbwa mwitu, nyama za ziada walizopata.

Vilevile jinsi wanadamu wanavyoweza - na bado hawawezi - kuishi kwa protini pekee.

"Kufuatia kipindi hiki cha awali, mbwa wadogo wangekuwa watulivu, wakitumiwa kwa njia nyingi kama vile ya kuwinda, kuwa wasindikizaji na walinzi," watafiti waliandika.

Jinsi ya kuwafuga

James Serpell, mtaalamu wa muingiliano wa binadamu na wanyama katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, anahoji manufaa ya pamoja ya kufuga mbwa.

Lakini katika utafiti uliochapishwa mwezi Aprili mwaka jana katika jarida la Frontiers katika Sayansi ya Mifugo, Serpell anasema kuwa kuasili kwa spishi-tofauti ni maelezo yanayokubalika zaidi ya jinsi mbwa mwitu alivyopelekewa kuwa mbwa wa kawaida.

Kwa kuanzia, mtaalam huyo anaonesha kuwa idadi ya watu ilikuwa ndogo sana makumi ya maelfu ya miaka iliyopita na watu walielekea kuishi katika vikundi vidogo na vilivyotawanyika, ambayo haingeweza kusababisha takataka nyingi.

"Pia, unapoangalia wawindaji wa kisasa, unaona kwamba hawatupi vitu," Serpell anasema.

"Kuna mifano mingi katika maandiko ya wawindaji-wakusanyaji kwa makusudi kuficha mabaki ya wanyama ili wanyama wengine wasiweze kuwafikia."

Serpell anaamini kwamba babu zetu "hawakutaka wanyama wakubwa wanaokula nyama mara kwa mara kwenye makazi yao".

"Kusini mwa Afrika, wawindaji wa kisasa wa msituni hufanya juhudi maalum kuwatisha simba, kwa mfano," anasema.

"Kwa hivyo, jambo la mwisho ambalo watu zamani wangetaka lilikuwa ni kuhimiza wanyama hatari kuwa kwenye kingo za jamii zao."

Hata hivyo, Serpell na wafuatiliaji wengine wa nadharia ya kuasili ya spishi-tofauti wanashuku kwamba mababu zetu hawakuwa tofauti sana na sisi katika kupenda kwao watoto wa wanyama.

Wanasema kuwa wanadamu wa kale walikuwa wanawakamata watoto wa mbwa mwitu na mara nyingi walipokuwa wakubwa walirudi porini.

Lakini watoto wengine wa mbwa mwitu walioweza kufurahia kuishi na binadamu, wangekuwa tayari kuzurura.

"Mara tu wananapoanza kuzaliana kutoka kwa mbwa mwitu hawa waliofugwa isivyo kawaida kwa urafiki, unapata aina hii mpya ya mnyama ambaye ni tofauti sana na aina ya mwitu," Serpell anasema.

"Lakini hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na sio kwa kupanga."

Mnyama anayefaa kwa wakati unaofaa?

Ufugaji wa asili wa mbwa ulifanyika zamani sana kwa uwezekano kwamba siku moja tutapata ushahidi wa uhakika wa jinsi ilivyotokea, kwa hivyo itabaki kuwa siri.

Lakini kile ambacho wataalam kutoka kambi za "kuasili" wanaonekana kukubaliana ni kwamba hakuna mnyama mwingine isipokuwa mbwa mwitu ambaye angeweza kuwa "rafiki wetu wa zamani".

"Jinsi tulivyohusiana na mbwa mwitu ilikuwa kama wawindaji wenzetu," Pat Shipman anasema.

"Tulichotaka kwa ajili ya maisha yetu kwa wakati huo hakikuwa na tofauti kabisa na kile ambacho mbwa mwitu walitaka."

"Wanyama wengi ambao tumefuga wakati wa kale, ni kwa sababu tulitaka kuwala au kuwatumia kubeba vitu," anaongeza.

James Serpell pia anakubali kwamba mbwa mwitu na wanadamu "walilingana kabisa".

"Baadhi ya wanasayansi wamesema kwamba mbwa mwitu na wanadamu au karibu kuzoea maisha pamoja: walikula vitu sawa, walikuwa na aina sawa ya ukubwa wa jamii na aina sawa ya utunzaji wa wazazi," anasema.

"Mambo mengi kuhusu sisi na wao yalikuwa sawa kabisa."