Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nchi ambayo kuulizwa umri wako ni suala la lazima
Mara ya kwanza Muingereza Joel Bennett alipogundua kwamba alifanya makosa makubwa wakati wa safari yake ya kwanza kwenda Korea Kusini ndipo alipomshukuru mwenye mgahawa kwa chakula kizuri.
Mmiliki alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 60 na Bennett, ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 wakati huo, alimwita rubberwo, ambayo hutafsiriwa kwa furaha "asante" kwa Kiingereza. Alifikiri kuwa alikuwa mpole.
Ingawa Bennett hakujua, alikuwa ametumia toleo la kawaida na lisilo rasmi la "asante" ambalo lingetafsiriwa kuwa chuki na matusi ikiwa lingekuwa la Kikorea.
"Sikutambua kulikuwa na njia nyingi za kusema asante. Siku zote nilifikiri asante ni asante," alisema Bennett, ambaye sasa ana umri wa miaka 33.
Lakini katika utamaduni wa Korea Kusini, Bennett, akiwa mdogo kwa miongo kadhaa kuliko mmiliki wa mgahawa huo, angetarajiwa kutumia lugha ya heshima.
Lugha ya kikorea ina mfumo mgumu wenye viwango vingi vya usemi na imeelezewa kama moja ya lugha ngumu zaidi duniani, kwani inahitaji tathmini ya mara kwa mara ya umri, hali ya kijamii na kiwango cha urafiki katika uhusiano na mpokeaji.
Ndiyo maana nchini Korea Kusini, muda mfupi baada ya kukutana na mtu, utauliziwa umri wako kila mara.
Kusema umri wako au mwaka ambao umezaliwa kwa uhuru sio tu mkutano wa kijamii. Ni mkataba wa kijamii ambao huweka utaratibu na uongozi miongoni mwa wazungumzaji.
Na ni kwamba hata tofauti katika mwaka kunaweza kueleza kila kitu kutoka kwa jinsi watu walivyozungumza hadi njia ya kula na kunywa katika jamii fulani.
"Sababu kuu ya kuamua kuweka mtindo huo ni kutambua maneno sahihi kutumika kulingana na umri," alieleza Jieun Kiaer, profesa wa lugha ya Kikorea katika Chuo Kikuu cha Oxford.
"Ndiyo maana watu huwa wanaulizana wana umri gani. Sio kwa sababu wanavutiwa na umri wa mwingine, lakini kwa sababu wanahitaji kuja na mtindo sahihi wa kuwasiliana," aliongeza.
Swali la msingi
Kuuliza umri wa mtu ambaye ndio kwanza wamekutana kunaweza kuonekana kama sio ustaarabu kwa baadhi ya watu wa Magharibi.
Lakini ili kuelewa ni kwanini umri sio namba tu katika jamii ya Kikorea kwa kuwa ni muhimu kujua athari za mkanganyiko unaoweza kutokea .
Ni itikadi za kizamani iliyojikita katika imani, utofauti kati ya mzee na kijana, na mpangilio wa kijamii, ambao ulikuepo katika nchi zaidi ya miaka 500 katika Enzi ya Joseon (1392-1910) na zinazoendelea kutawala kanuni za kijamii.
"Mchanganyiko wote huo unaweza kujumlishwa kwa maneno mawili: ubinadamu na matambiko," alisema Ro Young-chan, profesa wa masomo ya kidini na mkurugenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu cha George Mason cha Mafunzo ya Korea huko Fairfax, Virginia (Marekani).
Ro alieleza kwamba mafundisho ya mwanafalsafa wa Kichina Confucius (551-479 BC) yaliibuka wakati wa msukosuko katika historia ya China.
Ili kurejesha utulivu nchini kote, mwanafalsafa aliamini kwamba ubinadamu unaweza kusaidia kuanzisha muundo wa kijamii wa kiutu kulingana na kanuni kali za tabia nzuri na sherehe za kimila , ambayo kila mtu alikuwa na jukumu fulani na kila mtu alielewa nafasi yao ndani yake.
Kwa upande wake, umoja wa kijamii unaweza kupatikana kwa kuheshimu utaratibu wa asili ndani ya mahusiano matano makuu yanayojulikana kama oryun : mfalme na mhusika; mume na mke; baba na mwana; kaka na kaka; na kutoka kwa rafiki hadi rafiki.
Wale walio na nafasi ya kuongoza (baba, mume, mfalme) wanapaswa kutendewa mambo kwa heshima na unyenyekevu, wakati kwa kurudi wale walio katika ngazi za chini za uongozi wa kijamii hutunzwa kwa ukarimu.
Lakini katika jamii ya kawaida, unapokutana na mtu, ambaye amepewa cheo cha juu zaidi na kupata heshima, adabu, na taratibu za heshima zinazoambatana nayo?
Hapo ndipo umri unapozingatiwa.
Mfumo mgumu wa matabaka
Mfumo wa Lugha ya heshima ya Kikorea una viwango saba vya mitindo ya kuzungumza na kuandika.
Lakini mazungumzo ya kila siku yanaweza kugawanywa katika namna mbili: njia ya kawaida na isiyo rasmi; na iliyo rasmi zaidi ambayo kwa ujumla huoneshwa kwa kuongeza "I" mwishoni mwa sentensi.
In fact, the whole thing is so confusing that even native Korean speakers can get it wrong .
"Inahitaji umakini na majadiliano ili kupata mitindo sahihi ya kuzungumza. Na ikiwa unatumia isiyo sahihi, inaweza kuleta migogoro mingi na hutaweza kushiriki katika majadiliano yenye mafanikio," Kiaer alisema.
Alifafanua kwamba ingawa umri una jukumu muhimu katika kuamua namna ya kuzungumza , sio sheria kali na inayoongoza.
Kuna idadi ya vitu vya kuzingatia: muktadha; hali ya kijamii na kiuchumi ya wazungumzaji; kiwango cha faragha; na kama wako katika mazingira ya umma au ya faragha.
Kiaer alibainisha kuwa kutokana na umaarufu wa kimataifa wa Hallyu au wimbi la Kikorea - inaonekana katika umaarufu wa K-pop, filamu ya hivi karibuni ya Netflix "The Squid Game" - kanuni zinakuwa rahisi kufundisha, lakini bado zinaweza kuchanganya.
Kwa uhalisia, jambo zima ni la kutatanisha kwamba hata wazungumzaji asilia wa Kikorea wanaweza kukosea.
"Ili kupata mtindo sahihi wa kuwasiliana, hatua ya kwanza ni kujadiliana. Kwa sababu ukibadilisha mtindo mwingine bila mazungumzo, hiyo ndiyo huwafanya watu kuchukizwa," alisema.
Kabla ya kuhamia Korea Kusini mnamo Agosti, Delia Xu wa Toronto alikuwa na mkakati wa kuamua kujifunza Kikorea ili kuepuka kufanya hivyo.
"Nadhani ni muhimu sana kujifunza miundo rasmi ya sarufi, kwa sababu hutaki kusikika kama mkorofi kwa bahati mbaya," alisema.
Kadhalika, kuna ishara mbalimbali na tabia zisizo za maneno ambazo zinalingana na kile kinachotarajiwa kwa wale walio katika nafasi ya chini kabisa ya daraja la kijamii.
Katika video ya YouTube ya mwaka wa 2016 ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni 1.2, Bennett alipata somo la unywaji pombe nchini Korea Kusini alipokuwa na watu wazee.
Sheria zinakufanya uwe na kizunguzungu: kama onyesho la heshima, lazima uimimine kinywaji kwa mikono yote miwili; kugeuza kichwa chako upande wa pili wa mtu mzee unapokunywa; kamwe usiruhusu glasi ya mtu mzee kubaki tupu kwa muda mrefu; na umngoje aweke glasi yake chini kabla ya kuweka yako chini.
"Huna wasiwasi, lakini unajua," Bennett alisema. "Naangalia kiwango chao wanakunywa bia yao na nitaendana na hicho, nahakikisha glasi zao zimejaa ili tunapoenda kwenye kugonga, isiwe wakati wa shida."
Xu pia anakubali kwamba kujifunza kanuni za maadili kuhusu unywaji pombe kunaweza kuwa jambo la kuelemea.
"Hakika ni presha kubwa kwani ghafla unapewa majukumu mengi, ukiwa umekunywa pombe na hukuangalia upande mwingine, umemkera mtu ghafla, hakika inaweza kunichosha, lakini mimi 'nina uhakika ni kitu cha kufanya unazoea," aliongeza.
Katika hatua hii, inaweza kuwa rahisi kuashiria muundo wa kijamii wa Korea Kusini kama aina dhalimu ya ubaguzi wa rika na ubaguzi wa kijinsia, kwani wanawake pia wanatarajiwa kutii na kujinyenyekeza kwa waume zao, kulingana na mafundisho ya jadi .
Lakini, kama vile Bennett alijifunza hivi karibuni, jukumu la mtu mzee pia lina jukumu lake lenyewe.
"Mamlaka mengi yanahusiana na utumishi. Ikiwa mimi ndiye mtu mzee zaidi, ambaye nimeendelea zaidi katika masuala ya kazi yangu na maisha, nitakutunza mpaka kuwa mkubwa," alisema.
Katika Korea ya kisasa, hiyo inaweza kumaanisha kulipia chakula cha jioni cha mtu mdogo au kutumika kama mtaalamu na mshauri wa kibinafsi.
Njia za kuonesha heshima
- Wakati wa kutoa na kupokea pesa, fanya hivyo kwa mikono miwili.
- Unapokuwa na shaka, tumia kila mara mtindo wa kuzungumza kwa heshima na rasmi, bila kujali umri wako.
- Kwa ujumla, kumalizia sentensi na "yo" na "nida" kunaonyesha adabu, fomu ya jondaemal.
- Ongeza kiambishi nim kwa majina na mada ili kuonesha heshima.