Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanawake wa Afghanstan wapigwa marufuku kwenda safari ndefu wenyewe bila wanaume
Taliban imesema wanawake wa Afghanistan wanaotaka kusafiri umbali mrefu kwa barabara wanapaswa kupatiwa usafiri ikiwa tu wataandamana na ndugu zao wa kiume.
Maagizo hayo, yaliyotolewa siku ya Jumapili, ni yakiwa ni marufuku ya hivi karibuni katika haki za wanawake tangu kundi hilo la Kiislamu kuchukua madaraka mwezi Agosti.
Shule nyingi za sekondari bado zimefungwa kwa wasichana, wakati wanawake wengi wamepigwa marufuku kufanya kazi.
Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch lilisema marufuku hayo mapya yanawapelekea kuwafanya wanawake kuwa wafungwa.
Heather Barr, mkurugenzi msaidizi wa kundi la haki za wanawake, aliliambia shirika la habari la AFP agizo hilo "kufunga fursa kwa [wanawake] kuweza kutembea kwa uhuru" au "kuweza kukimbia ikiwa kama wanakabiliwa na unyanyasaji majumbani".
Agizo la hivi karibuni, lililotolewa na wizara ya Kukuza Utu na kinga ya Makamu wa Taliban, lilisema wanawake wanaosafiri kwa zaidi ya maili 45 (72km) wanapaswa kusindikizwa na mwanafamilia wa karibu wa kiume.
"Nilijisikia vibaya sana," Fatima, mkunga anayeishi Kabul, aliiambia BBC, akijibu agizo hilo. "Siwezi kwenda nje kwa kujitegemea. Nifanye nini ikiwa mimi au mtoto wangu ni mgonjwa na mume wangu hapatikani?"
Aliongeza: "Taliban waliteka furaha yetu kutoka kwetu... Nimepoteza uhuru na furaha yangu."
Waraka huo unatoa wito kwa wamiliki wa magari kukataa kuwaendea wanawake wasiojifunika uso, au hijabu, ingawa haisemi ni aina gani ya vazi la kutumia. Wanawake wengi wa Afghanistan tayari wanavaa hijabu.
Pia ilipiga marufuku uchezaji wa muziki kwenye magari.
Tangu Taliban ichukue mamlaka baada ya kuondoka kwa majeshi ya Marekani na washirika wake, mamlaka hayo yawamewaambia wafanyakazi wengi wa kike kubaki nyumbani wakati shule za sekondari zikiwa zimefunguliwa kwa ajili ya wavulana na walimu wa kiume pekee.
Taliban wanasema vikwazo hivyo ni vya "muda" na viko mahali pekee ili kuhakikisha maeneo yote ya kazi na mazingira ya kujifunzia ni "salama" kwa wanawake na wasichana. Wakati wa utawala wao wa awali katika miaka ya 1990, wanawake walizuiwa kupata elimu na mahali pa kazi.
Mwezi uliopita, kikundi hicho kilipiga marufuku wanawake kuonekana katika tamthilia za televisheni na kuwaamuru wanahabari na watangazaji wa kike kuvaa hijabu kwenye skrini.
Mataifa wafadhili yamewaambia Taliban kwamba lazima waheshimu haki za wanawake kabla ya kurejesha msaada wa kifedha.
Nchi inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu na kiuchumi unaofanywa kuwa mbaya zaidi na kuondolewa kwa msaada wa kimataifa baada ya kundi hilo kuchukua madaraka.