Habari njema na mbaya kuhusu Omicron zina maana gani kwetu?

Dunia imepigwa na tsunami ya Omicron. Wanasayansi, wanasiasa na kila mmoja wetu anapambania kujua hii hali ina maana gani katika maisha yetu.

Vikwazo vinaongezeka katika sehemu za Uingereza na nchi nyingine za Ulaya ili kukabiliana na aina hii mpya ya virusi vya corona.

Kuna mfululizo wa taarifa mpya - nyingine zikiwa zinatisha, nyingine zikiwa nzuri. Je, tunasimama wapi?

Huu sio msimu wa baridi uliopita

Ni rahisi kusahau, lakini tuko mahali pazuri zaidi kuliko wakati kama huu mwaka jana ambapo wengi wetu hatukuweza kukutana na familia Siku ya Krismasi.

Sheria za "kusheherekea sikukuu ya Krismasi" zilimaanisha kuwa katika sehemu za nchi unaweza kutumia siku hiyo kwa kuwa na wale unaioishi nao. Lakini kulikuwa na mipaka juu ya kiwango cha mikusanyiko kote Uingereza.

Kuibuka kwa wimbi la Alpha mwishoni mwa mwaka 2020 kulisababisha marufuku ya kutoka nje mwezi Novemba na muda mrefu katika Mwaka Mpya kwani mpango wa chanjo ulikuwa unaendelea tu.

Omicron si kali sana

Ukipata Omicron basi kuna uwezekano mdogo wa kuwa mgonjwa sana kuliko aina nyingine za virusi vya corona zilizopita.

Uchunguzi kutoka duniani kote unatoa taswira thabiti kwamba Omicron ni dhaifu kuliko virusi vya Delta, na uwezekano wa chini wa 30% hadi 70% wa watu walioambukizwa kulazwa hospitalini.

Omicron inaweza kusababisha dalili za wakati wa baridi kama vile maumivu ya koo, mafua na maumivu ya kichwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa hali itakuwa nyepesi kwa kila mtu, wengine bado watakuwa wagonjwa sana.

Mabadiliko ya virusi vya corona yanaonekana kuifanya kuwa hatari kidogo, lakini ukali mwingi uliopunguzwa ni kutokana na matokeo ya chanjo na vipindi vya hapo awali vya corona.

Lakini Omicron inaenea haraka sana

Wasiwasi wa kulemewa na maumivu itakuwepo ikiwa hospitali zinaweza kustahimili.

Kama nusu ya watu waliopata maambukizi ya Omicron wataenda hospitalini, lakini mara mbili ya watu wengi wameambukizwa na kughairi kwenda kwenye tiba basi tutakuwa tumerudi kwenye hatua ya kwanza tu.

Na talanta halisi ya Omicron ni kuambukiza watu.

Huenea kwa kasi zaidi kuliko virusi vingine na inaweza isithibitiwe na baadhi ya ulinzi wa kinga dhidi ya chanjo na maambukizi ya awali.

Uingereza ina viwango vya rekodi vya Covid na kesi zilizothibitishwa mnamo Alhamisi kufikia karibu 120,000 - na hii inatokana na kuwa si kila mtu anapimwa na watu wanaoipata zaidi ya mara moja hawajajumuishwa kwenye takwimu.

Hatuna uhakika kitakachotokea Omicron itakapowapata wazee

Wazee mara zote huwa katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa sana wakipata Covid.

Huko Uingereza, wagonjwa wengi wa Omicron waliofika hospitalini wako chini ya umri wa miaka 40 kwa hivyo hatujui kwa hakika nini kitatokea wakati itafikia wazee na makundi ya watu wanaoishi na magonjwa ya muda mrefu.

Uwezo wa Omicron kukwepa kinga kwa sehemu inamaanisha kuwa kuna uwezekano wa watu wazee zaidi kuambukizwa kuliko wakati wa wimbi la Delta.

Idadi kubwa imeimarishwa, lakini ulinzi unapungua

Dozi mbili za chanjo hutoa ulinzi mdogo dhidi ya kuambukizwa Omicron, ambayo ilisababisha ongezeko kubwa la kampeni ya nyongeza.

Sasa zaidi ya watu milioni 31 nchini Uingereza wameimarisha ulinzi wao wa kinga.

Hata hivyo, ulinzi dhidi ya Omicron unaonekana kupungua baada ya takriban wiki 10.

Kinga dhidi ya ugonjwa huo inaweza kudumu kwa muda mrefu.

Lakini tuna dawa za kuzuia virusi sasa

Dawa mpya zinapaswa kuwaweka wagonjwa wengi zaidi nje ya hospitali.

Zinatolewa kwa watu walio katika hatari kubwa ya Covid, pamoja na wagonjwa wa saratani na watu ambao wamefanyiwa upandikizaji.

Molnupiravir ni dawa ya kuzuia virusi ambayo uondoa uwezo wa Omicron ndani ya miili yetu na kupunguza idadi ya watu kulazwa hospitalini kwa 30%.

Sotrovimab ni tiba ya kingamwili inayopunguza ukali wa virusi na kupunguza watu kwenda hospitali kwa 79%.

Dawa zote mbili hukandamiza virusi kwa muda huku mfumo wa kinga ukipambana.

Wiki chache zijazo ni muhimu

Swali ni ikiwa kila kitu kinaenda kwa kutuzingatia sisi - maambukizi yasiyo na ukali, kuwa na dawa ya kuzuia virusi, uboreshaji wa kinga - inatosha kukabiliana na aina ya kirusi inayoenea kwa kasi zaidi kuliko kitu chochote ambacho tumeona hapo awali.

Au itachukua vikwazo zaidi kudhibiti wimbi la Omicron?

Kasi hii inayotokea inamaanisha tutajua haraka sana jinsi itakavyoishia.