Mauaji ya Malcolm X ya 1965: Hukumu za wanaume wawili kufutwa

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwendesha mashtaka mkuu wa Marekani anasema watu wawili waliopatikana na hatia ya mauaji mwaka 1965 ya kiongozi wa haki za kiraia wa Marekani Malcolm X watafutiwa hukumu dhidi yao

Muhammad Aziz na Khalil Islam hawakupata haki waliyostahili, Mwanasheria wa Manhattan anasema.

Mwendesha mashtaka Cyrus Vance Jr aliliambia gazeti la New York Times kwamba FBI na polisi wamezuia ushahidi ambao ungesababisha kuachiliwa kwao.

Malcolm X alipigwa risasi na kufa kwenye ukumbi wa New York City mbele ya familia yake.

Aziz na Islam - pamoja na mtu wa tatu, Thomas Hagan - walitiwa hatiani kwa mauaji hayo, na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Wanaume hao watatu - wanachama wa vuguvugu la kisiasa na kidini la Nation of Islam - wote wameachiliwa. Islam aliaga dunia mwaka 2009.

Katika mahojiano na gazeti la New York Times, Bw Vance aliomba radhi kwa niaba ya vyombo vya sheria, akisema wameiangusha familia za Aziz na Islam

"Hii inaashiria ukweli kwamba utekelezaji wa sheria juu ya historia mara nyingi umeshindwa kutekeleza majukumu yake.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malcolm X

"Watu hawa hawakupata haki waliyostahili."

Bw Vance aliandika kwenye twitter kwamba taarifa zaidi zitatolewa Alhamisi.

Mnamo 2020, Wakili wa Manhattan alizindua ukaguzi wa hatia baada ya kukutana na wawakilishi wa Mradi wa Kutokuwa na Hatia, kikundi cha kisheria kisicho cha faida kinachopigania haki kwa watu ambao ilisema walikuwa wamehukumiwa kimakosa.

Mapema mwaka huu mabinti wa Malcolm X waliomba uchunguzi wa mauaji ufunguliwe tena kwa kuzingatia ushahidi mpya.

Walitaja barua ya kifo kutoka kwa mtu ambaye alikuwa polisi wakati wa mauaji ya 1965, akidai polisi wa New York na FBI walikula njama katika mauaji hayo.

Malcolm X alikuwa mtetezi wa watu weusi. Baada ya miaka kama msemaji maarufu wa Nation of Islam - ambayo ilitetea kujitenga kwa Wamarekani weusi - maoni yake baadaye yalikua ya wastani