Mapinduzi ya Sudan: Kwanini Jeshi linaweka rehani hatma ya taifa hilo?

General Abdel Fattah al-Burhan

Chanzo cha picha, AFP

Kiongozi wa mapinduzi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan amepiga hatua kuelekea gizani. Amehatarisha msimamo wa Sudan kimataifa, misamaha muhimu kwa madeni na misaada ya kimataifa na kuhujumu amani na waasi jimbo la Darfur na milima ya Nuba. Alikuwa mkuu wa baraza huru la Sudan na uso wa jeshi kwenye serekali ya pamoja ya jeshi na raia hadi Jumatatu wakati alitwaa madaraka yote.

Alivunja baraza la mawaziri la raia, akammkata waziri mkuu Abdalla Hamdok na watu wengine mashuhuri ambao jeshi lilikuwa limeafikiana nao kuwagawana madaraka hadi wakati uchaguzi ungeandaliwa mwaka ujao.Matamanio yake jenerali huyu hayakuwa siri. Miezi kadhaa iliyopita alionyesha kukosa uvumilivu kwa uongozi wa Hamdok, akiashiria kuwa mtawala mwenye nguvu alikuwa anahitajia kuiokoa nchi. Wakati wa maandamano ya hivi majuzi yaliyoungwa mkono na jeshi kwenye mji mkuu Khartoum, waandamanaji walimlaumu Bw Hamdok kwa kudorora viwango vya maisha.

Wanaounga mkono demokrasia nchini Sudan walikumbwa na wasi wasi kufuatia mienendo ya jesho ambayo ilionekana kunakiliwa kutoka kitabu kilichochangia jeshi la Abdul Fatah al-Sisi kutwaa madaraka nchini Misri mwaka 2013.Chama cha wasomi nchini Sudan kilichoongoza maandamano yasiyo yenye ghasia yaliyoangusha utawala wa miaka 30 wa Rais Omar al-Bashir mwaka 2019, walijiandaa kwa awamu mpya ya maandamano mitaani.

Wanadiplomasia wa kigeni nao walikuwa na wasiwasi. Mjumbe maalumu wa Marekani Jeffrey Feldman alizuru Khartoum mwishoni mwa wiki kushinikiza uwepo ya maelewano kati ya majenerali na raia. Aliondoka mjini humo siku ya Jumapili na kile alichofikirii ni mapatano yaliyokuwa yameafikiwa.

Sudanese

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Waandamanaji wameazimia kutoruhusu jeshi kufanya hila ya mapinduzi ambayo yalisababisha Omar al-Bashir kuondolewa madarakani 2019.

Mapinduzi yalifanyika saa chache baadaye na kuwaacha Wamarikani sio tu wameshangazwa lakini wamekasirika pia. Uongozi nchini Marekani sasa umesitisha msaada wa dola milioni 700. Na kubwa zaidi ni suala la kusamehewa deni lililofikia makubaliano kwa jitihada za Bw Hamdok.

Baada ya miaka miwili ya subira, msaada wa kimaifa wa kufufua uchumi uliafikiwa lakini unaonekana kuhujumiwa. Muungao wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Igad na wafadhili wote wa Sudan wa nchi za magharibi wamelaani mapinduzi hayo na kutoa wito wa kurudi kwenye utawala wa raia.

Saudi Arabia na Milki ya Nchi za Kiarabu waliotoa msaada muhimu wa kifedha kwa Gen Burhan mwaka 2019 wamesalia kimya. Mapendeleo yao yanaegemea upande wa Burhan lakini pia wajue kuwa hawawezi peke yao kuikomboa Sudan.

Gen Burhan tayari alikuwa mtu mwenye nguvu zaidi nchini humo na nafasi yake ilihalalishwa na makubaliano ya kugawana madaraka ya mwaka 2019 kati ya jeshi na makundi ya raia ya Forces for Freedom and Change (FFC)

Himaya za Kibiashara

Kulingana na makubaliano hayo, Gen Burhan angeng'atuka kama mwenyekiti wa baraza huru mwezi ujao. Wakati huo raia ambaye angeteuliwa na FFC angekuwa kiongozi na raia serikalini wangekuwa na nafasi nzuri ya kutekeleza yaliyokuwa kwenye ajenda zao. Moja ni uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Serikali imejitolea kumsalimisha rais wa zamani Omar al-Bashir kwenda mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Majenerali wake wa zanani wakiwemo Jenerali Burhan na mkuu wa kikosi kinachojulikana kama Rapid Support Forces, Jenerali Mohamed Hamdan "Hemeti" Dagolo - walitaka ashtakiwa nchini Sudan na sio Hague. Wana sababu nzuri ya kuhofu kuwa Bashir anaweza kuwataja kuwa wahusika kwenye ukatili uliotokea wakati wa vita kwenye jimbo la Darfur.

Gen Burhan na maafisa wenzake wana hata sababu zaidi za kuhofu kuwa uchunguzi kuhusu mauji ya watu wengi mjini Khartoum June 2019 utawanyooshea kidole cha lawama. Yalifanyika miezi miwili kabla ya kupinduliwa kwake Bashir wakati waandamanaji wenye amani waliitisha utawala wa kiraia.

Bw Hamdok alikuwa akilikosoa jeshi kwa kuingilia uchumi. Sio tu jeshi linasimamia mgao mkubwa wa bajeti, lakini kampuni zinazomilikiwa na jeshi hazilipi ushuru na zimekumbwa na ufisadi. Kuliweka jeshi chini ya udhditi wa raia ilikuwa ajenda kwa awamu ambayo ingefuatia ya kipidni ya mpito.

Hatari ya hatua kutoka kwa waasi

Gen Burhan anasema atadumisha mageuzi kwenda demokrasia na ameahidi kufanyika uchaguzi katika kipindi cha miaka miwli. Harakati za jeshi zimevunja vyama muhimu vya wafanyakazi na makundi ya wataalamu yaliyopanga maandamano ya awali.

Intaneti na mitandao ya kijamii imefungwa kwa kiwango kikubwa, wanajeshi wamewafyatulia risasi waandamanaji na kuripotiwa kuawa watu 10. Wanaharakati wameshinda hatua kama hizo awali na kulazimisha jeshi kulegeza kamba hasa baada ya mauaji ya Juni 2019.

Majenerali hawa pia lazima wajue kuwa vita vya wenyewe kwa wenye sehemu kadhaa za nchi bado havijakwisha.

Chairman

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jenerali Burhan na Waziri Mkuu Hamdok walikuwa sehemu ya uongozi wa mpito wa Sudan kabla Burhan kuongoza Mapinduzi

Makubaliano ya amani mwaka uliopita yaliyaleta makundi kadhaa yenye silaha ndani ya serikali lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa na makundi mawili makubwa ya waasi. Huko Darfur kuna kundi la Sudan Liberation Movement linaloongozwa na Abdel Wahid al-Nur, na katika milima ya Nuba, Kordofan Kusini lipo kundi la Sudan People's Liberation Movement-North, lnaloongozwa na Abdel Aziz al-Hilu.

Mwaka 2019 kufuatia harakati mbaya za jeshi kwa makundi ya waandamanaji, Marekani, Uingereza, Saudi Arabia na Milki ya nchi za Kiarabu walishinikiza kuwepo suluhu kwa njia ya mazungumzo suluhu iliyopatikana mwezi uliofuatia.

Mchakato sawa na huo unahitajika kuiokoa Sudan. Tatizo ni, baada ya Jumatatu, ni nani atamuani Jenerali Burhan ?