Fahamu kuhusu wanaigeria wanaotaka Israel iwatambue kama wayahudi

A Nigerian Jewish man

Chanzo cha picha, Irums

Maelezo ya picha, Shlomo Ben Yaakov anataka kuwa mwanazuoni wa kwanza kutoka Nigeria.

Shlomo Ben Yaakov anaonekana akisoma kitabu cha torati akiwa kwenye nyumba ya ibada ama hekalu la wayahudi nje kidogo ya mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Kwa upole sauti yake laini laini kwa lugha ya Kiebrania akifuatishwa na kuitikiwa na makumi kadhaa ya watu nyuma yake.

Wengi hawaelewi kabisa lugha hiyo, lakini jamii hii ndogo ya Nigeria inadai asili ya Kiyahudi iliyoanzia mamia ya miaka huko nyuma - na wakikatishwa tamaa kwa kuachwa na kutotambuliwa na Israeli.

"Najiona kama myahudi," anasema Yaakov.

Nje ya nyumba hiyo ya ibada ya Kiebrania ya Gihon katika kitongoji cha Jikwoyi meza imewekwa ndani ya hema lililojengwa kwa majani ya mitende kusherehekea Sukkot, sikukuu inayokumbusha miaka ambayo Wayahudi walikaa muda mrefu jangwani wakiwa njiani kwenda Nchi ya Ahadi.

"Kama tunavyofanya hivi sasa, Israeli nao wanafanya hivi," anasema Bw Yaakov, wakati watu wanagawiana mkate wa jadi wa cholla (uliookwa katika sinagogi) na divai kwenye vikombe vidogo vinavyopitishwa.

Yeye anatoka katika jamii ya Igbo - moja ya makabila matatu makubwa nchini Nigeria ambayo yanatokea kusini mashariki mwa nchi hiyo . Jina lake la kikabila (Igbo) anafahamika kama Nnaemezuo Maduako.

Jewish women

Chanzo cha picha, Irums

Maelezo ya picha, Tofauti na wazazi wao, wayahudi wengi vijana wa Nigeria hawajui dini nyingine

Watu wengi wa kabila la Igbo wanaamini kwamba wana urithi wa Kiyahudi kama mojawapo ya makabila 10 yanayoelezwa yalipotea kutoka Israeli, ingawa wengi hawatekelezi ya kiyahudi kama anavyofanya Yaakov. Watu hawa ni chini ya 0.1% ya watu milioni 35 wa jamii ya Igbo.

Makabila haya yalisemekana kutoweka baada ya kupelekwa utumwani wakati ufalme wa kaskazini wa Israeli uliposhindwa katika Karne ya 8 KK - na jamii ya Kiyahudi ya Ethiopia, kwa mfano, inatambuliwa kama moja yao. Makabila haya yanasemekana yalitoweka baada ya kutekwa kama watumwa wakati utawala wa kifalme Kaskazini wa Israeli ulipoangushwa katika Karne ya 8 . Jamii ya Kiyahudi ya Ethiopia, kwa mfano, yenyewe inatambuliwa kama sehemu ya wao.

Mila ya Igbo kama vile tohara kwa wanaume, kuomboleza msiba (wafu) kwa siku saba, kuadhimisha mwezi mpya na kufanya sherehe za harusi chini ya dari zimeimarisha imani hii juu ya urithi wao wa Kiyahudi.

'Hakuna ushahidi'

Lakini Chidi Ugwu kutoka kabila la Igbo ambaye ni mtaalam kutoka Chuo Kikuu cha Nigeria huko Enugu, anasema kitambulisho hiki na Uyahudi kiliibuka tu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Biafra.

Watu wa Igbo walikuwa wakipigania kujitenga kutoka Nigeria, lakini walishindwa katika mmoja wa mizozo mikali kati ya 1967-1970.

Biafran

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu wanaamini chimbuko la jamii ya Igbo ni Uyahudi na liliibuka zaidi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu milioni 1.

"Ni kama matusi kusema Igbo ni kabila la wapotevu, hakuna ushahidi wa kihostori kuthibitisha hilo," ameiambia BBC.Anasema kuwa kama ushahidi unaonyesha Waigbo walikuwa miongoni mwa wale waliohama kutoka Misri miaka elfu kadhaa iliyopita, huenda Wayahudi walichukua mila za Igbo walipokwenda huko.

Miaka kadhaa iliyopita juhudi za kutatanisha zilifanywa kuthibitisha ukoo wa maumbile, lakini vipimo vya vinasaba (DNA), havikuonyesha uhusiano huo wa Kiyahudi.Rabi Eliezer Simcha Weisz, mwenyekiti wa idara ya maswala ya kigeni ya Baraza la Rabbinate la Israeli - chombo kinachoamua madai ya ukoo wa Kiyahudi, anasema pia chombo hicho hakina shaka na hilo.

Wanadai kuwa ni sehemu ya kizazi cha baba yetu Jacob - lakini hawawezi kuthibitisha kwamba babu na nyanya zao walikuwa Wayahudi, "aliiambia BBC."Na mila wanayozungumzia, unaweza kuipata kila mahali na kwa watu wengi ulimwenguni kote ambao wana 'Gadi', tabia moja ya Kiyahudi."

Alisema Wayahudi wa Nigeria watatambuliwa kwa kugeukia Uyahudi wa Israel kama watafuata mchakato ambao unajumuisha mila na kufika mbele ya mahakama ya Kiyahudi (ambayo haipatikani nchini Nigeria)

Kuongezeka kwa wanaojitenga

Washirika ama waumini wa Gihon wanachukulia imani zao kwa uzito - na wao na jamii ya wayahudi inayokadiriwa kufikia 12,000 wanaotekeleza imani ya Kiyahudi - wanaungwa mkono na vikundi vingine vya Kiyahudi vya Orthodox ulimwenguni kote, ambao huwachangia, hufanya ziara za mshikamano na kufanya kampeni ya kutambuliwa.

Mmoja wa watu mashuhuri anaowaunga mkono ni Dani Limor, wakala wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) ambaye wakati fulani aliendesha operesheni ya siri ya kuwachukua Wayahudi wa Ethiopia na kuwapeleka Israeli kupitia Sudan. Amekuwa akitembelea jamii za Kiyahudi nchini Nigeria tangu miaka ya 1980 na anasema kuwa uyahudi katika taifa la Afrika Magharibi ulikuwepo kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Men

Chanzo cha picha, Irums

Maelezo ya picha, Inakadiriwa kuwa wanigeria 12,000 wanajitambulisha kama wayahudi.

Anaamini katika shule ya mawazo ambayo inasema wayahudi hao walitoka Morocco katika miaka 500 iliyopita, kwanza wakiweka makazi eneo la Timbuktu kabla ya kusafiri zaidi kuelekea kusini - na ana matumaini kwamba mwisho wa siku watapata kile wanachostahili cha kutambuliwa.

"Uyahudi ni zaidi ya rangi ya ngozi, uyahudi uko moyoni," aliiambia BBC.

Hekalu la Gihon, inayosemekana kuwa ya zamani zaidi nchini Nigeria, lilianzishwa miaka ya 1980 na Ovadai Avichai na watu wengine wawili ambao walikuwa wamelelewa kama Wakristo.

Marafiki hao waliamua kuugeukia Uyahudi baada ya kugundua kuwa Agano la Kale la Biblia lilikuwa msingi wa dini ya Kiyahudi.

Alisema kufanana kwa mila za Kiyahudi na utamaduni wa Waigbo kuna mfanya aamini kwamba Uyahudi ndio njia ya kweli.

Nnamdi Kanu

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Many Nigerian

Hekalu la Kiyahudi la Gihon huko Abuja kwa sasa lina mchanganyiko wa makabila mbalimbali kati ya familia zaidi ya 40 zinazoabudu hapo.Katika miaka michache iliyopita idadi ya watu wanaoabudu kama wayahudi kusini mwa Nigeria imeongezeka kwa kiasi kikubwa, anasema mtaalam wa BBC kuhusu masuala ya dini Chiagozie Nwonwu.

Hii inatokana uwepo wa watu wa Asili wa Biafra (Ipob), kikundi ambacho kilianzisha tena kampeni ya Igbo ya kujitenga mnamo 2014. Kikundi hiki kinaongozwa na Nnamdi Kanu, ambaye alikuwa akiwakumbusha wafuasi wake juu ya unaodaiwa kuwa urithi wao wa Kiyahudi na kuwahimiza waikubali imani hiyo. Kiongozi huyo mwenye haiba, aliwahi kuonekana kwenye picha akisali kwenye Ukuta wa Magharibi huko Yerusalemu.

Lakini wafuasi wake hawachukuliwi kama Wayahudi halisi na jamii zilizoimarika zaidi za Nigeria kwani wengine wanachanganya mambo ya Uyahudi na Ukristo katika ibada zao inayohusishwa zaidi na Uyahudi wa Kimesiya. Bwana Kanu sasa yuko kizuizini akikabiliwa na kesi ya uhaini na Ipob, kimepigwa marufuku kikionekana kama kikundi cha kigaidi.

"Mara ya kwanza Ipob alipoibuka, nililia hekalu. Nikasema: 'Kijana huyu mdogo amekuja kutusababishia shida kwa sababu anachofanya sio lazima," anasema Bw Avichai, mkongwe wa vita wa Biafra.

Anaogopa shughuli za Ipob zinatishia ibada ya amani kwa jamii za Kiyahudi 70

Map of Nigeria

Hili ilitokea mapema mwaka huu wakati kiongozi wa jamii ya Kiyahudi kusini-mashariki aliposwekwa gerezani kwa mwezi mmoja baada ya mkutano wake wa kupokea wageni watatu kutoka Israeli.Walikuwa wamekuja kupiga picha ya mchango wa kitabu cha Torati - mara nyingi huwa ghali sana kwa vikundi vya mitaa kununua - lakini walishukiwa kuwa na uhusiano na Ipob hivyo walirudishwa kwao.

Mmoja wa waumini kwenye hekalu la Gihon alieleza kwamba, Kanu alimshawishi na kuamua kujiunga na hekalu hilo - lakini mabadiliko ya hivi karibuni ya kampeni ya Ipob iliyohusisha silaha yalikwenda kinyume na imani ya Uyahudi.

Yaakov yeye anasema hataki siasa kwenye Uyahudi - kwake anasema muhimu ni jambo la kiroho. "Kama wakristo na waislamu wanaunga mkono imani zao nafikiri wayahudi pia wanapaswa kutiwa moyo."