Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini Misri inahofia mpango wa Uturuki kuiuzia ndege zisizo na rubani Ethiopia?
Ethiopia imeomba kununua ndege ya kijeshi isiyokuwa na rubani (drones), aina ya Biraktar TB2 kutoka Uturuki, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Mbali na Ethiopia, Uturuki imeshauza ndege zisizo na rubani kwa nchi kadhaa ikiwemo ya Kaskazini mwa Afrika, iliripoti Reuters.
Mwanadiplomasia mmoja aliye karibu na anayelijua suala hilo alisema Morocco ilipokea duru ya kwanza ya ndege zisizo na rubani zilizoagizwa mwezi Mei mwaka jana. Alisema Ethiopia ina mpango wa kuagiza ndege hizo ingawa hakuna maelezo zaidi juu ya rubani iliyoagizwa na Ethiopia.
Makubaliano ya uuzaji wa ndege hiyo yanahusu pia utoaji wa vipuri na mafunzo ya nguvu kazi; ingawa, vyanzo vya habari havijaeleza zaidi kuhusu idadi ya ndege hizo ambazo Ethiopia inakusudia kununua kutoka Uturuki, kulingana na Reuters.
Ethiopia, Moroko na Uturuki hazijasema lolote kuhusu mpango huo wa ndege hizo zisizo na rubani. Serikali za nchi hizo hazikujibu maoombi kutoka kwa Reuters ya kuzungumzia suala hilo. Wakati huo huo, takwimu za usafirishaji wa bidhaa kwenda nje ya nchi, unaonyesha kuwa usafirishai wa bidhaa za nje za Uturuki kwenda Ethiopia na Morocco umeongezeka katika miezi michache iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Mkutano wa wafanyabiashara wanaouza nje Uturuki, uagizaji wa vifaa vya ulinzi na anga wa Ethiopia katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha uliongezeka kutoka dola $ 203,000 hadi $ 51 milioni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa nini Misri imejaa na hasira dhidi ya mpango huu wa Ethiopia?
Mpango wa Ethiopia kununua ndege ya kijeshi isiyo na rubani kutoka Uturuki umeibua hasira nchini humo, Reuters imeripoti. Maafisa waweili wa Ulinzi Misri wameiambia Reuters: Cairo imezitaka Umoja wa Ulaya na Marekani kuingilia kuzuia uwezekano wowote wa makubaliano ya Ethiopia na Uturuki Turkey. Wasiwasi wa Misri dhidi ya Ethiopia unatokana na mzozo uliopo katika ya nchi hizo kuhusu ujenzi wa bwawa katika mto Nile. Uhusiano wake pia Uturuki hauko sawa.
Chanzo kingine cha tatu kutoka Misri ameiambia Reuters kwamba Uturuki na Ankara wanahitaji kushauriana na Uturuki kabla yakufikiwa kwa makuabliano yoyote na Ethiopia.
Biractar TB 2
Ndege hizi za TB2 zinasemekana kuwa zag haram za juu kabisa hasa zinazotengenezwa nchi zingine. Ndege hizo zinazalishwa na Bairaktar na zimebuniwa na mkwe wa rais wa Uturuki, Rais Tayyip Erdogan. Baadhi ya nchi mashariki ya kati ikiwemo watengenezaji wa Bayraktar TB2, ni wanachama wa NATO au wana mkataba na Uturuki kutengeneza ndege hizo.
Watengenezaji wa ndege hizo wanasema karibu ndege 160 za TB 2 kwa sasa zinatumika Uturuki, Qatar, Ukraine NA Azerbaijan. Mwezi Mei mwanachama mwingine wa NATO, Poland waliingia makubaliano ya kununua ndege zisizo na rubani 24. Waziri wa ulinzi wa Poland aliiambia Radio 2 ya nchini kwake, kuwa ndege hizo zimeonyesha "thamani yake kwenye vita", limeripoti Reuters.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema Saudi Arabia pia wameonyesha nia ya kununua ndege gizo zisizo na rubani za Uturuki.
Bayraktar TB2 kwenye uwanja wa vita
Bayraktar TB2 imebuniwa kwa ajili ya kufanya mashambulizi. Ndege hizi zenye uzito wa mpaka kilo 150, zinawezakuendeshwa kutoka umbali wa mpaka kilometa 300 km. Kwa mujibu wa mtandao wa watengenezaji wa ndege hizo, zina urefu wa mita 12, kwa juu zina urefu wa mita 2.2 na uwezo wa kuchukua mafuta ya mpaka lita 300.
Ndege hizo zinaweza kupaa na kutua zenyewe bila kuendeshwa na mtu. Ndege hizi zinaweza kubebwa na makombora manne makubwa. Iliripotiwa kwamba ndege zisizo na rubani za Uturuki ilikuwa kifaa muhimu cha ushindi wa Azerbaijan katika vita kati ya Azerbaijan na Armenia. Uturuki ilitumia pia ndege zake hizo katika vita huko Syria na Libya.
Matumizi ya ndege zisizo na rubani kwenye vita ya Tigray
Tangu kuanza kwa vita vya Tigray kaskazini mwa Ethiopia, kumekuwa na taarifa kwamba, majeshi ya serikali yalitumia ndege hizi dhidi ya wanamgambo wa TPLF.
Katika mahojiano na Televisheni ya taifa mwaka 2013, Meja Jenerali Yilma Merdasam, kamanda jeshi la anga la Ethiopian, alithibitisha kwamba walitumia ndege hizo zisizo na rubani.