LGBTQ: 'Nilipogundua kijana wangu amebadili jinsia, nilifikiria kujiua lakini ...'

'Alikuwa anazeeka, na alikuwa akiniambia kitu kimoja - Mama, nipeleke kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili. Nahitaji msaada. Sitaki kujua chochote. "
Nilikuwa nikimwambia, "Wewe ni mwanaume wa aina yako, una shida gani? Ninahitaji msaada. Sijaolewa, mimi ni mjane. Lazima uwe mkweli ... Mama usijali, mimi ni msaada wako. "
Supriya Gosavi ananiambia katika makazi yake huko Goregaon lakini masahibu yaliyomtokea zamani yanaonekana wazi machoni mwake. Katika sehemu hii nzuri ya Mumbai, hata kama ndogo kiasi gani, bado wanahaha kuishi vizuri. Na bila shaka safari yao ilikuwa tofauti na zile zingine.
Mume wa Supriya alikufa wakati Supriya alikuwa na umri wa miaka arobaini. Akiwa na watoto wa kiume wawili, mmoja ana umri wa miaka kumi na sita na mwingine ana umri wa miaka sita. Safari ya kuwa mzazi pekee kulea watoto wake ilianza. Mambo yalianza kuwa ya wasiwasi, muda unavyozidi kwenda. Lakini aliamini kwa sababu yuko na kijana wa kiume pengine shida na matatizo yangepungua kutokana na kusaidiwa na kijana huyo.
Kama ilivyo kwa mzazi yoyote, alikuwa na ndoto juu ya mtoto wake. Asome, apate kazi, apate msichana mzuri wa kumuoa na maiesha yaendelee.
Lakini mtoto wake Nishant wakati huo alikuwa njia panda kiakili. Mateso yake hayakuvumilika. Siku moja alipata tatizo na kuanguka barabarani. Supriya alimpeleka kijana wake katika Hospitali ya KEM huko Mumbai. Daktari aligundua kuwa kijana yule alikuwa na shida ya akili. Siku moja daktari huyo alimwita Supriya na kumwambia "Sasa ni lazima ukubaliane na ukweli."
Supriya bado hakujua chochote. Daktari alimwambia "Mtoto wako ana jinsia tofauti. Yeye ni mwanamke lakini katika mwili wa mwanaume. Lazima ukubali hii."
Akikumbuka siku hiyo, uso wa Supriya bado unaonekana kukunjamana.
"Sikuelewa hata maana ya kubadili jinsia ndio nini. Nilichoweza kuelewa ni kuwa, msichana-msichana. Mwanaume-mwanamke," alisema Supriya.
Mara nyingi tunasikia na kuona kuhusu jamii ya kijana huyu, aliyejibadilisha jinsia, ama wenye jinsia tofauti (LGBTQ) na mara nyingi hawakubaliki nyumbani kwao. Lakini nini safari ya wale wanaowakubali?
Je nini kiko kichwani mwa wazazi walioamua kubadili dhana yao na kuendelea kuonyesha upendo kwa watoto wao? Simulizi ya Marathi wa BBC inajaribu kupata jibu la swali hili.
Ni ngumu hali hii kukubalika kirahisi. Siku moja Supriya alikuwa matembezini. Wakati huu, alikuwa na ugomvi na mtoto wake.
"Mama yangu alifanya maisha yangu kuwa magumu sana. Kila siku tulikuwa tunagombana. Kulikuwa na ugomvi kila siku na ugomvi huo ulikuwa kwa sababu nilikuwa jinsia tofauti," anasema binti Nistha (Nishant wa Purvashram).

Wote Nishtha na Supriya hawakuwa na afya nzuri ya akili. Hakujua jinsi ya kukabiliana na mabadiliko yanayotokea katika mwili na akili yake, alikuwa akihangaika kujua kuhusu utambulisho wake, kwa hivyo Supriya angeweka wapi sura yake mbele ya jamii?
Hatukujua nini cha kufanya kutokana maadili tuliyoyafuata kwa miaka mingi. Kuna wakati Supriya aliwaza kuwaacha watoto wake na kutokomea kwingine.
"Nilifikiria hata kujiua," anasema.
Maisha yasioeleweka yalikuwa yakiendelea na mambo yaliyohusu familia hii yalikuwa burudani kwa wengine, waliwacheka.
Familia ya Supriya ilikuwa ikiishi kwenye kibanda kimoja huko Dadar. Watu walikuwa wakifika kuangalia nini kilikuwa kikiendelea nyumbani mwao.
"Kama tulikuwa tunapitia hali kama hiyo ya akili, watu wangekuwa wadadisi sana. Halafu angetoka nyumbani saa 1 usiku kwenda kwenye mihangaiko yake. Utafikiri ni uwongo. Kwanini umevaa viatu virefu vyenye visigino? nilitaka kuiona vizuri. Ilinisumbua sana. "
Kijana wa Supriya anakumbuka siku hizo, "Alikuwa akinifuata. Alikuwa akinitazama na kuangalia watu wananichukuliaje. Ikiwa mwanaume yoyote angejaribu kunitazama, na yeye alifuatilia kwa macho yake. Nilijua alikuwa akijaribu kunilinda. , Lakini hakuona shida yangu. "
Supriya alifanya kazi kwa bidii kuhakikisha anamtambulisho mtoto wake kama mwanaume.
Tangu kijana wake awe wa jinsia tofauti, Supriya pia hakutaka kusikiliza upuuzi . Malezi yake kama mama yalikuwa yakihojiwa. Baba wa mtoto hayupo, na mtoto inaonekana hakulelewa vyema, Supriya anasema mtoto alizaliwa hivyo hivyo alivyo.
Kila siku alikuwa akisikia maneno ya kejeli, hata ndugu zake pia walikuwa tofauti. Lakini hakufikiria hata siku moja kumfukuza mtoto wake huyo wa jinsia tofauti.

"Nani atamlea mtoto ambaye mama yake hamjali?", alisema na kuongeza "mkono mmoja umevunjika (baba wa mtoto amefariki). Nitakua nani mie bila ya watoto hawa wawili?"
Supriya alijiuliza, kwanini ndugu zake hawasemi kitu, kwanini jamii aisemi kitu ... Tunataka kuwaweka watoto wetu kwenye ulimwengu kwa namna tulivyo na tusikate tamaa.
Changamoto kubwa kwa familia ya Supriya ilikuwa ni kuhama kutoka kwenye kibanda chao cha Dadar kwenda mahali pengine. Familia ilikuwa inateseka kwa sababu ya mawazo ya watu wa huko. Lakini pia tatizo la pesa.
"Sikujua nguvu zilitoka wapi , tulithubutu na kuhamia kwenye nyumba hii. Baada ya kuja hapa, tumepata utulivu wa akili."
Katika eneo hilo, wakakutana na taasisi inayoitwa 'Accept - The Rainbow Parents' ambayo inawasaidia wazazi ambao watoto wao ni wajinsia tofauti, au wamebadilisha jinsia au wanashiriki mapenzi ya jinsia moja, na utambulisho huo umekuwa mgumu kwao kuukubali ama kukubalika.

Katika taasisi hiyo wazazi ambao hawaukubali utambulisho wa watoto wao wanashauriwa hapa.
Kijana wa Supriya alimlazimisha mama yake kwenda kwenye mikutano kadhaa ya shirika hili. Japokuwa Supriya hakuwa tayari.
"Alipokwenda kwenye mikutano, nilivyomuuliza, nini kimeendelea, hakujibu, alienda kwenye mkutano mwingine mmoja ama miwili, lakini hakusema lolote. Siku moja nilifungua Facebook na kuona picha za mikutano hii, nikamuona na mama yangu akilia karibu katika kila picha."
"Siku moja alikuja na kuniomba msamaha. Alikuwa hajanielewa vizuri, sikujisikia vizuri wakati huo, hata kama mama yangu amekubaliana na nilivyo, kabla ya hapo najua hakuwa anakubali." Lakini siwezi kueleza namna nilivyojisikia baada ya mama yangu kunikubali. "
Kwa sasa kijana huyo anaamini anaweza kuushinda ulimwengu baada ya mama yake na kaka yake kumuunga mkono na kuwa nyuma yake. Kijana wa miaka 16 au 17 aliyekuwa hajielewi, kijana aliyechanganyikiwa sasa amebadilika na kuwa mwanamke anayejiamini.
Nyumbani kwo sasa, kuna alama ya upinde wa mvua kuonyesha kukubaliana na hali hiyo na mtoto wake wa kiume ambaye sasa ni binti, amekuwa akifanya kazi na kupata heshima. wale waliokuwa wanamtazama vibaya barabarani sasa wanatamani kumpongeza na wengine wanampongeza.
Imekuwa afueni kwa mama yake, Supriya.
Awe ni mtoto wa kuiume, wa kike, ama jinsia ya tatu, mzazi yeyote angetamani kuona akiishi kwa furaha.













