Mazungumzo ya kuwabadilisha wapenzi wa jinsia moja: Mamia ya viongozi wa kidini wataka yapigwe marufuku

Chanzo cha picha, Getty Images
Zaidi ya viongozi 370 wa kidini kutoka maeneo tofauti duniani wametoa wito wa kupigwa marufuku kwa mazungumzo -jaribio la kubadilisha mwelekeo wa kijinsia wa mtu au utambulisho wa kijinsia.
Waliotia saini azimio hilo wanawakilisha imani kuu zote ulimwenguni na wengi wanajulikana kama watetezi wa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia zao (LGBT).
Miongoni mwao ni Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu na Chief Rabbi wa zamani wa Ireland David Rosen.
Viongozi wengine wa kidini walisema marufuku hiyo huenda iwatia mashakani viongozi wa kidini.
Azimio la marufuku hiyo litazinduliwa katika mkutano uliofadhiliwa na Ofisi ya masuala ya kigeni, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) Jumatano.
Askofu wa kanisa la Kianglikana mjini Liverpool, Paul Bayes, na Mary McAleese, rais wa zamani wa Ireland, pia ni miongoni mwa wale waliyotia saini tangazo hilo.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameahidi tena kupiga marufuku dhidi ya mazungumzo yanayowahusu wapenzi wa jinsia moja , akisema mwezi Julai kuwa hatua hiyo "haifai kabisa" na "haina nafasi katika nchi hii".
Serikali haijachapisha maelezo kuhusu marufuku hiyo, lakini imesema imesema kuwa imeagiza utafiti kufanywa na itatoa muongozo wa mpango wake "hivi karibuni".
Neno The term "tiba ya uongofu" linamaanisha aina yoyote ya tiba ambayo inakusudia kubadilisha mwelekeo wa kijinsia ya mtu au kukandamiza kitambulisho cha jinsia ya mtu.
Inakjumuisha mafundisho ya kidini au mazungumzo yanayolenga kubadilisha jinsia ya mtu.
Mazungumzo hayo tayari yamepigwa marufuku Uswizi na katika baadhi ya maeneo nchini Australia, Canada na Marekani.
'Niliogopa'
Utafiti wa mwaka 2018 uliyojumuisha watu 108,000 kutoka jamii ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza ulibaini kuwa asilimia mbili ya watu wamepata tiba hiyo, wengine asilimia tano wameshawishiwa kuipata.
Imani nyingi duniani zikiwemo, Ukristo, Uislamu na Uyahudi zinatoa mafunzo yanayopinga ndoa ya watu wa jinsia moja.
Joe Hyman, 28, alilelewa katika familia ya Kiyahudi na Orthodox kaskazini mwa London. Anasema alipokuwa kijana mdogo alipewa manzo yanayowahusu wapenzi wa jinsia moja mtandaoni.
"Nilitaka wanibadilishe," aliambia BBC. "Sikutaka kufikiria kuwa shoga wakati nikiwa Myahudi. Sikudhani familia yangu ingelinikubali. Niliogoma sana."
Anasema alipewa tiba ya kubadilisha jinsia mtandaoni na ana kwa ana.
"Iliniacha nikijisikia mtupu kweli, niliyepungukiwa na wasiwasi, kila wakati nilikuwa na wasiwasi na hofu kwamba sikuwa nikifanya jambo sahihi," alisema.

Chanzo cha picha, Joe Hyman
Azimio hilo linatoa wito wa kupigwa marufuku " jaribio la kutaka kubadilisha,kukandamiza au kufuta mwelekeo wa kijinsia wa mtu, kitambulisho cha kijinsia au usemi wa kijinsia - unaojulikana kama 'tiba ya uongofu' - kumaliza, na mazoea haya mabaya kupigwa marufuku. "."
Hata hivyo, baadhi ya makundi ya hafidhina ya kidini kutoka imani tofauti yanasema marufuku hiyo huenda yakaingilia uhuru wa kidini,
Wanahofia marufuku hiyo itamaanisha serikali itabuni sheria ya kudhibiti mafunzo yatakayotolewa na viongozi wa kidini- kile wanachoweza kufunza au la
Peter Lynas, Mkurugenzi wa Uingereza wa Muungano wa Kiinjili unaojumuisha makanisha 3,000 nchini Uingereza, anesema anaunga mkono " kukomeshwa [kwa] tabia mbaya na ya kulazimisha bila kupiga marufuku mabadiliko mafundisho ya kidini, ambayo ni msingi wa Ukristo".
Aliambia BBC marufuku hiyo huenda " ikawatia mashakani washauri nasaha, wachungajina hata wale wanaoombwa kuwaombea watu."
'Tunataka kusaidia'
Sheikh Ramzy, mwanazuoni wa Kiislam na mwanzilishi wa Kituo cha Habari cha Kiislamu, amesema ni muhimu kwa maimamu kupewa nafasi ya "kusaidia" ikiwa Waislamu mashoga wanataka kubadilisha muelekeao wao wa kijinsia.
"Tunataka kuwasaidia sio kuwadhuru," aliambia BBC.
Lakini Joe, anasema tiba hiyo inastahili kupigwa marufuku mara moja.












