Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je wanasayansi wamezingatia jinsi ngono inavyoweza kufanyika nje ya dunia?
Mapenzi na ngono lazima vifanyike angani ikiwa tunatarajia kusafiri umbali mrefu na kutoka sayari moja kwenda nyingine.
Lakini mashirika ya anga za mbali hayajatafakari kuhusu wazo hilo.
Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA) na kampuni za kibinafsi kama vile SpaceX, zina malengo ya kuwapeleka wanadamu kuishi kwenye sayari ya Mars lakini mahitaji ya kujamiana kwa wanaanga au viumbe kutoka duniani watakaoishi hapo siku za baadae bado hayajaangaziwa.
''Hali hii lazima ibadilike kama tuna matarajio ya kuanzisha dunia mpya na kuendelea katika kuiongeza'', alisema mmoja wa wataalamu wanaoshinikiza wanasayansi kuzingatia suala hilo.
''Tutajifunza jinsi ya kuzaliana kwa usalama na kuweza kujenga mahusiano mazuri katika maisha ya angani.''
Ili kufanikisha hilo, mashirika hayo yanahitaji kuweka mikakati mipya ya kuangalia mahitaji muhimu ya binadamu katika maisha ya angani.
Kama watafiti wanaochunguza saikolojia ya binadamu katika ngono na kusoma masuala ya saikolojia ya binadamu angani, tunaamini kwamba ni wakati muafaka kwa mpango wa anga kuja na mikakati mizuri ya nafasi ya ngono katika anga za mbali, vilevile kuja na utafiti kamili wa kisayansi kuhusiana na suala hilo.
Mpaka wa mwisho unaotenganisha mahusiano
Pamoja na hayo, mashirika ya anga za mbali yanaendelea na mpango wa muda mrefu wa kuwa Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS), Mwezini na katika sayari ya Mars bila ya kuwa na utafiti wowote thabiti na mpango wa kushughulikia mahitaji ya kingono kwa binadamu watakaoishi huko.
Ni suala moja kufika kwenye sayari nyingine au kuzindua safari ya mabilionea kwenda anga za mbali lakini ni suala lingine kwa binadamu kuishi katika anga hzio kwa kipindi cha muda mrefu.
Kiuhalisia, sayansi ya anga za mbali inaweza kutupeleka katika anga hizo lakini itakuwa vigumu kubaini ikiwa mahusiano ya binadamu yanaweza kukuzwa na kudumishwa katika eneo hilo.
Kwa maana hiyo basi, tunaamini kwamba kuweka kiwango cha faragha angani kunaweza kuhatarisha afya ya akili na ngono ya wanaanga, pamoja na utendaji wao wa kazi ili mpango uweze kufanikiwa.
Kwa maana nyingine ni kwamba, kuruhusu ngono angani kunaweza kusaidia wanadamu kuzoea maisha ya anga za mbali na kuboresha ustawi wa wenyeji wa anga ya baadaye.
Pia ni vyema kuzingatia kwamba mazingira katika anga za mbali nimagumu, na maisha kwenye anga hizo ukiwa kwenye chombo maalum au makazi ni changamoto kubwa kwa mahusiano ya binadamu.
Hii inajumuisha mionzi, mabadiliko ya mvuto, kujitenga kijamii, na mfadhaiko wa kuishi katika makazi ya mbali na yaliyofungwa.
Katika siku za usoni, maisha katika anga yanaweza pia kupunguza upatikanaji wa wenza wa karibu, kuzuia faragha, na kuongeza mivutano kati ya kikosi hicho na hivyo kuhatarisha hali ya ushirikiano ambao ni muhimu.
Baadhi ya tafiti zimehusisha mada hii kwa kuzingatia zaidi athari ya mionzi kupitia uzazi wa wanyama (kama panya na wadudu).
Furaha na miiko
Lakini ngono kwa binadamu huenda zaidi ya kuzaliana. Inajumuisha mienendo tata ya saikolojia, mihemko na mahusiano.
Hivyo, uchunguzi wa anga unahitaji ujasiri wa kushughulikia mahitaji muhimu ya wanadamu kwa upande wa mahusiano.
Kuzuia sio chaguo sahihi, Kinyume chake, itawafanya watu kujichua wakati ngono na mwenza inaweza kusaidia wana anga kupumzika, kulala, na kupunguza maumivu.
Itawasaidia kujenga na kudumisha uhusiano wa kimapenzi au wa kingono na kuzoea maisha ya angani.
Ni muhimu kushughulikia masuala ya kijinsia ya maisha ya mwanadamu angani kwa kuwa inaweza kusaidia kupambana na ujinsia, ubaguzi na udhalilishaji ambao kwa bahati mbaya unaendelea kushuhudiwa katika vitengo vya kisayansi na kijeshi, ambavyo ni nguzo ya mpango wa anga za mbali.
Kwa sababu ya miiko na maoni tofauti kuhusu ngono, baadhi ya mashirika yanaweza kuchagua kupuuza hali halisi ya mahusiano angani.
Wengine wanaweza kuhisi kuwa hili si tatizo au kuna masuala mengine muhimu zaidi ya kuzingatia masuala ya ngono.
Lakini mtazamo huu hauna tija, kwani kutengeneza sayansi bora kunajumuisha muda na rasilimali, na afya ya kijinsia, pamoja na raha kunaimarisha utambuzi wamasuala kama haki za binadamu.
Hii inamaanisha kuwa mashirika ya anga na kampuni za kibinafsi yanaweza kuwajibika kwa ustawi wa kijinsia na uzazi wa wale wanaoenda angani.
Mahusiano ya kimapenzi nje ya dunia
Ili kuendelea mbele, mashirika ya anga lazima yaache kukwepa mada za ngono na yatambue umuhimu wa mapenzi, ngono, na uhusiano wa karibu katika maisha ya mwanadamu.
Kwa hivyo, tunawahimiza wataalamu wa anga za mbali kuzingatia mahusiano kama sehemu ya sayansi na mpango wa utafiti - ambao unakusudia sio tu kuangalia ngono angani, lakini pia kubuni mifumo na kuweka mipango ya mafunzo ambayo ni rafiki kwa mahusiano angani.
Kwa kuongezea, tunaamini kwamba kutokana na utaalamu wake na hali ya kisiasa na kijamii ya Canada, Shirika la Anga la Canada lina nafasi nzuri ya kuwa kiongozi wa ulimwengu katika masuala ya ngono angani.
Tuna kila kitu kinachotuwezesha kuona namna ambavyo safari za anga za mbali zitakuwa na maadili na ya kufurahia, wakati tukiendelea kuwa na ujasiri wa kwenda sehemu ambayo hakuna aliyewahi kufika.