Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Katika picha: Jinsi mwisho wa Ramadhani unavyosheherekewa duniani
Waislamu duniani kote wanasheherekea sikukuu ya Eid huku waumini wengi wakijitokeza kusali majira ya asubuhi.
Waamini hawa wanasheherekea kwa kuwa na karamu ya pamoja na familia pamoja na marafiki huku wakiwa wanapeana zawadi.
Eid al-Fitr ni siku ya mapumziko duniani kote.
"Eid al-Fitr" ikimaanisha sherehe za kumaliza mfungo wa ramadhani".
Waumini waliokuwa wanafunga kwa kuacha kula au kunywa kwa saa za mchana huku wakijiweka karibu na Mwenyezi Mungu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan.
Vilevile Ramadhani ni kipindi ambacho waislamu wanasisitizwa kutoa msaada kwa wahitaji na kuimarisha uhusiano na Mungu pamoja na kuonesha ukarimu na kuwa na subira.
Kama ilivyo kipindi cha Ramadan, Eid inaanza wakati ambao mwezi mpya unaanza kuonekana.
Mwaka huu , waumini wengi wa kiislamu wameitimisha kipindi cha ramadhani na wanasheherekea Eid wakati ambao kuna marufuku dhidi ya corona.
Hizi ni baadhi ya picha duniani kote wakisheherekea Eid kwa kusali na kufurahi kwa pamoja.
Waislamu kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania hii leo wamejitokeza kwa ajili ya swala ya Eidul Fitr.
Hii ni baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati huo huo swala ya Eid kitaifa imeswaliwa jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Baadae, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Dar es Salaam. Ni kawaida kwa waumini wa Kiislamu kusheherekea siku hii kwa kupika vizuri, kuvaa vizuri lakini pia kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki.
All photos subject to copyright.